Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapishi ya maandazi.

Discussion in 'JF Chef' started by Mamndenyi, Jul 8, 2011.

 1. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,234
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  [h=3]Nawaachia mapishi haya (nimedesea mahali) kwa weekend hii, hasa wale mabinti zangu, then feed me back.

  NAMNA YA KUTENGENEZA MAANDAZI
  [/h]
  Chukua Amira ya chenga gram 11, Chumvi nusu kijiko kidogo cha chai,Sukari gram 250, Unga wa ngano kilo moja, Maji ya uvugu vugu nusu lita, Mafuta ya kupikia lita 2 na nusu. Weka pakiti ndogo ya amira yenye ujazo wa gramu 11 yoote kwenye unga wako wa kilo moja. Kisha weka chumvi nusu kijiko kidogo cha chai chumvi hii husaidia kupunguza mafuta ndani ya andazi baada ya kuiva andazi lako litakua halina mafuta safi na salama kwa mlaji. Weka sukari gram 250 katika unga wako. Baada ya hapo weka mafuta ya moto ujazo wa kikombe kidogo cha chai au gr 250 changanya vizuri mafuta bado yakiwa ya moto. Kisha weka maji ya uvuguvugu ili kuuwa ngano na kufanya amira kuweza kuumuka haraka. Kanda mchanganyiko wako safi kwa kutumia nguvu na umakini mpaka mchanganyiko wako uwe laini. Mchangyanyiko wako kama uko bado ni teketeke na ulizidisha maji kidogo weka unga kiasi kisha endelea kukanda mpaka uwe mkavu na laini. Hapa safi sasa. Shepu vizuri tayari kwa maandalizi ya kusukuma na kukata Sukuma unga wako mpaka saizi ya unene halisi wa andazi lako utakavyopenda liwe. Kisha tumia kitu chechote kile kukatia kwa umbo lolote lile utakalo lipenda. Yaache kwa muda wa dakika 10 baada ya kuyakata yaumuke kisha itakua tayari kwa kuyachoma. Baada ya kukata maumbo mazuri ya duara unga unaobakia unaweza viringisha maumbo tofauti kama uonavyo katika picha pia unaweza tengeneza hata herufi. Pasaha mafuta yako katika moto wa wastani yasiwe na moto mkali utapelekea maandazi yako kuungua kisha yaweke katika moto na geuza kila mara ili yasivimbe upande mmoja na ikawa vigumu kuyageuza. Hili ni andazi lako safi limeshaiva na halina mafuta ndani na safi kabisa.
   
 2. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asante
   
 3. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,150
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ahsante sana.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,234
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  Asanteni mliopika.
   
 6. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,718
  Likes Received: 394
  Trophy Points: 180
  nimepika natamani nikuonjeshe.
   
 7. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,267
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  nifundishe kababu, mke wangu hajui nikampe shule
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,234
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  safi sana, hongera.
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27,234
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  QUOTE=First Born;2219255]nifundishe kababu, mke wangu hajui nikampe shule[/QUOTE]

  1. Mapishi – Kababu (Meat Ball)
  Leo tuangalie mapishi ya meat ball (kababu) za nyama ya ng'ombe. Ni kitafunwa kizuri sana kwa asubuhi au hata jioni.
  Mahitaji
  · Nyama ya kusaga 1/2kg
  · Yai 1
  · Kitunguu maji 1
  · Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1
  · Pilipili manga kijiko cha chai
  · Chenga za mkata (bread crumbs) kikombe cha chai
  · Kotmir majani 3
  · Chumvi kiasi
  · Mafuta ya kupikia
  Matayarisho
  1. Katakata vitunguu maji vipande vidogo vidogo, kisha changanya nyama ya kusaga, vitunguu maji ,kotmiri iliyokatwakatwa, vitunguu saum (tangawizi ukipenda), na chenga za mkate.(Ukitumia chenga za mkate halisi ni nzuri zaidi kuliko zile spesho za madukani). Weka chumvi na pilipili manga. Waweza pia weka pilipili mbuzi kama utapendelea.
  2. Pigapiga yai na kisha uchanganye kwenye mchanganyiko wako, hakikisha vimechanganyika kabisa. Kisha tengeneza madoge madogo ya mviringo na weka pembeni. Hakikisha madonge sio makubwa sana ili nyama iweze iva vizuri.
  3. Weka kikaango jikoni na mafuta na kiasi ili madonge yako yasizame, weka kababu zako kwenye mafuta na ziache ziive upande mmoja kisha geuza na upande mwingine. Zingatia moto uwe wa kiasi ili zisibabuke bali ziive hadi ndani kabisa.
  4. Epua na weka kwenye sinia yenye karatasi za jikoni ili zichuje mafuta yote kisha weka mezani tayari kwa kula.
  Waweza kula na chai, juis, soda au hata mchuzi wa maharage, mboga za majani n.k jinsi upendavyo mwenyewe.
  2. Kababu Za Mayai

  VIPIMO
  Mayai yaliochemshwa 6
  Nyama ya kusaga 1 1/2 Ratili (LB)
  Tangawizi na thomu iliyosagwa 1 kijiko cha Supu
  Pilipili mbichi ya Kusaga 1
  Mafuta 2 Vijiko Vya Supu
  Unga wa mahindi (Constarch) 1 Kijiko cha Supu
  Chumvi Kiasi
  Bizari ya manjano 1/4 kijiko cha chai
  Dania ya unga 1/4 Kijiko cha chai
  Bizari ya Pilau 1/4 Kijiko cha chai  NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
  1.Changanya nyama na vitu vyake kisha gawanya madonge 6 yaliyosawa.
  2.Chukuwa donge moja tia ndani yake yai uliochemsha na lifunike vizuri .
  3.Ukisha maliza yote panga kwenye treya la kupikia katika jiko la oveni nyunyizia mafuta kidogo na choma moto wa 375F kwa muda wa dakika 25.
  4.Yakishaiva epua na kisha ukate kama ilivyo kwenye picha .Tayari kuliwa

  Viungo vinapatikana ktk maduka ya viungo au s/markets
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Jul 13, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,200
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Thanks dear... mapish yako yametulia...
   
Loading...