Mapinduzi Yaliyoshindwa ya DARUSO 2002/3

Status
Not open for further replies.
Thanks brothers,I have enjoyed a wonderful conversation of traitors from UDSM to date.
guys,may I know a little bit about Introduction of HELSB during your university era!? And the trip to SA!?
 
Wanajf samahan ndg zangu najua ridhiwani nimesoma naye mkwawa-aliishi makongoro west-je huyu omary lyasa naye katoka kwenye ile shule kongwe iliyo na msomi karibia kila taasisi!?i mean mkwawa high school 1998-2000
 
Wewe mchokozi sana, mapinduzi yaliongozwa na akina Zitto, Ridhwan Kikwete, A.Msando na Omary Lyas

walikuwa wanasema tulishinda kijanja kijanja na hawakuwa na imani na ushindi wetu.

Kumbuka kabla ya Kayombo alikuwepo Rugemarila na kabla ya Ruge alikuwapo injinia mmoja, the war was engineers will never take over the DARUSO again!

Vita baridi au upinzani wa wahandisi na wasio wahandisi ( ambao tulikuwa tunawaita Mangwin) umekuwapo pale miaka mingi sana. cha ajabu hii vita iko mpaka level ya admistartion ya chuo.Utakumbuka walimu wa sociology, lawasa, FASS, Political science huwa hawapendi kabisa kuongozwa na wahandisi, na hii Luhanga alipata shida sana, mpaka kuliwa kichwa wakati anafanya degree ya sheria!

Leo hii Mkandala anafanya madudu hutawasikia wahadhiri wasio wahandisi wakipiga kelele sana!!...ni 'wao'

Back to the maada:

Nilikuwapo wakati kura zinahesabiwa za urais wa Kayombo, sikuona mchezo mchafu. Ila Ruge alimpa shavu Kayombo na hii ikawahudhi baadhi ya watu. na Ruge ndiye aliyesaini mikataba ya bodi ya mikopo hii watu wanayolia leo, sasa hii ikafanya hata Kayombo aliyekuwa supported na Ruge kuonekana kuwa atafuata nyayo zake tu! sasa hii sababu changanya na ule upinzani wa jadi wa maininjia na mangwin basi hapakukalika. Zitto akaenda kutokea bungeni na kuwa kuliongoza bunge la wanafunzi ambapo kupitishwa kwa mawaziri kulikuwa kasheshe pia.

Kayombo ni mhandisi yuko kiwanda cha chai Iringa nadhani ina future ana mpango agombee ubunge kule sijajua kwa chama gani

It was good days, memorable and from that generation today we have good politicians, I mean watu wanaojua siasa sio biashara, ukijua siasa tamu sana unaweza ukawapelekesha watu unavyotaka , na siasa ni hatari sana kama unapata viognozi wenye kujali maslahi yao, basi unaweza ukawapumbaza watu. Personally nimefanya kazi na Zito na Omar Lyas, Kizuri cha zito ambacho huwa nampa shavu, huwa anaquality ya kuangalia mbaaali sana, hili sina wasiwasi naye. Ridhwan nilijua tu alikuwa maneno mengi na misimamo, kama ya akina Zitto na nikajua labda atakuwa kiongozi mzuri, sijaona bado!! A. Msando is another 'animal' in politics sijui yuko wapi.

Our tactic of ushindi ilikuwa kila second year engineering anaenda na watu wawili kupiga kura, tukaenda kuwabembeleza sociology (you know) na haikuwa shida kwa B.com kuwa upande wetu... ule uchaguzi ushindi haukuwa rahisi, lakini kura hazikuchakachuliwa, ILIKUWA TU NI MBINU YA waliotaka kupindua kujitetea katika hilo. HALI ILIKUWA TETE

Marehemu Chachage ndio alituita kundi la serikali na wale waliotaka kutupindua kutusuluhisha na kuweka mambo asawa atleast. Ukweli Kayombo alikuwa na support ya administration si kwa ubaya.

Siyo siri, DARUSO inasaidia sana ku-shape viongozi, kinachotia uchungu viongozi wengi waliopitia DARUSO wako CCM na unajua what is happening there...ufisadi tu


kwani umekumbuka nini mkuu?[/

Unbelivable!

QUOTE]
 
Naukumbuka sana huu mgogoro wa daruso kipindi hicho japo sikua UDSM, Kayombo alikuwa makamu wangu kwenye uongozi wa TAHLISO kipindi hicho Mimi nikiwa rais DIT ... changamoto zinazojitokeza wakati wa uongozi vyuoni huwa ni mtihani sana na ndio maana wale wanaomaliza migogoro hiyo vizuri huwapa ujasiri zaidi na hatimaye wengi wao huweza kuwa viongozi wazuri...lakini wale wanaoumizwa na changamoto hizo wengi hukosa ujasiri wa kuongoza tena na hivyo kupotea kabisa kwenye siasa...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hivi yule Yank alietimuliwa na Government eti ni Mganda hafai kuwa kiongozi pale UD anaitwa nani
 
Kayombo alishinda kwa ujanja ujanja
Aliyeshika nafasi ya pili nakumbuka alikuwa anaitwa DEOGRATIUS MTUI inasemekana kuwa hiki kijamaa ndicho kilikuwa kishindi halisi lakini aliibiwa kura na Zitto kwa nia ya kumsaidia Mugurusi na Kayombo akapeta...

Alberto aliongoza mapinduzi ya kipuuzi akishirikiana na haka kajamaa basi nakumbuka tuliandamana.... Msando are you there? can you tell us what happened?
Huyo Jamaa alitumia pesa nyingi sana kufanya kampeni, lakini alishindwa na kampeni ya chumba kwa chumba ya Kayombo, tena alishindwa kabisa, hakuna kura iloibiwa!!
 
Dah mungu akubariki mleta uzi haitatokea tena UDSm kukawa na watu wa kuthubutu kama bench la 2001/2003 vugu vugu la mapunduzi ndilo lilonipa mke ambae nipo nae mpaka sasa thnk god for dat

Omar ilys alikua na rafiki yake wa kipemba alikua mpambe wake anaitwa nani vle
 
Wewe mchokozi sana, mapinduzi yaliongozwa na akina Zitto, Ridhwan Kikwete, A.Msando na Omary Lyas

walikuwa wanasema tulishinda kijanja kijanja na hawakuwa na imani na ushindi wetu.

kwani umekumbuka nini mkuu?

Waberoya Brother hivi unaweza kweli kuthibitisha kuwa kinachoendelea CHADEMA leo kina uhusiano na hili lilotokea wakati huo?
 
Last edited by a moderator:
Sidhani kama kayombo ana element yoyote ya kuwa kiongozi maana hao ni wale ambao CCM ilikuwa inapandikiza kuvuruga mandeleo ya wanafunzi na serikali zao basi kwisha habari hata Deo ni type hiyo hiyo, tunawaita mapandikizi; Ruge alipandikizwa na Malecela John Samwel kumbukeni ndio wakati huo anajiandaa kugombea Urais, Zitto na Omar walikuwa wing ya kikwete then wakati Ruge anaondoka wakakubaliana na Malecela nani apewe kupitia kwa Mzee Mungai wakasema wana-trust kwa kayombo ndio chanzo cha yeye kuachiwa maana mwanzoni Albeto alikuwa kambi ya Malecela ila baada Zito akamchukua then akawa kambi yao. kwa ufupi siasa za DARUSO halisi ziilishia mwaka 2000; baada ya hapo ni chezo wa kuigiza na akili za tuition hata Engineering hiyo mnayo semakwa maana ya FoE miaka ya 2002 haikuwepo tena; naweza kusema serikali halisi ya siasa ya watu wenye kujua nini ya mwisho ni Kitila sijui kwa sasa nini kinaendelea maana hata zito wewe umwkuwa ukitumiwa sana na TIIS kumbuka ata mgomo uliperekea kuondoka kwa wakina Magabe na Marehem Mkiri wewe ulikuwa imformer wa serikali good day.

Duh!
Kweli NGwini ngwini tu!
 
Hivi yule Yank alietimuliwa na Government eti ni Mganda hafai kuwa kiongozi pale UD anaitwa nani

Odong Odwar kama sijakosea...it was a very hot battle between Odong na uongozi wa chuo but finally jamaa alirudishwa Uganda baada ya maCcm kuplant kadi ya chama kwenye personal stuffs zake...
 
Hivi Tweve yupo wapi?nakumbuka mgomo wa kugomea kusainiwa mswaada wa mkopo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom