whats the fuss jamani?yaani zito kutishiwa na kubenea amekimbia mazima
mkuu, ulikuwa ushasepa eeh?damn i feel ancient...
kwani umekumbuka nini mkuu?
In our days wazee wa. FOE lazima upige kura ! Na unasaini kabisaa..hiyo ni 2000 wakati wa Kitila Mkumbo..not sure kama ndio alikuwa presdaa ama vipi?..however personnaly sioni kama a good freedom fighter can be the best kupewa wizara au urais..have watched my share of trade union leaders getting posns and fail..so do the freedom fighters they are needed to get the revolution on bt then step out watching trouble makers..not running the show!Alberto sasa ni Diwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na leo anachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Atafutwe mtu anaitwa Siriwa ndiye anajua mkakati ulianzia wapi na akina nai walihusika. Hao hapo wanaotajwa wala hawakuwepo na waliokuwepo walidandia basi ndio maana lilizama. Niko Tite kusaka LEAKS ZA TANZANIA niacheni kwanza na hivi vijimambo vidogo vidogo. Wewe uliyechukua fedha za China kupitia benki fulani hivi inaanza na jina la N ama M nisubiri nabandika cable zako humu siku sii nyingi
Sidhani kama kayombo ana element yoyote ya kuwa kiongozi maana hao ni wale ambao CCM ilikuwa inapandikiza kuvuruga mandeleo ya wanafunzi na serikali zao basi kwisha habari hata Deo ni type hiyo hiyo, tunawaita mapandikizi; Ruge alipandikizwa na Malecela John Samwel kumbukeni ndio wakati huo anajiandaa kugombea Urais, Zitto na Omar walikuwa wing ya kikwete then wakati Ruge anaondoka wakakubaliana na Malecela nani apewe kupitia kwa Mzee Mungai wakasema wana-trust kwa kayombo ndio chanzo cha yeye kuachiwa maana mwanzoni Albeto alikuwa kambi ya Malecela ila baada Zito akamchukua then akawa kambi yao. kwa ufupi siasa za DARUSO halisi ziilishia mwaka 2000; baada ya hapo ni chezo wa kuigiza na akili za tuition hata Engineering hiyo mnayo semakwa maana ya FoE miaka ya 2002 haikuwepo tena; naweza kusema serikali halisi ya siasa ya watu wenye kujua nini ya mwisho ni Kitila sijui kwa sasa nini kinaendelea maana hata zito wewe umwkuwa ukitumiwa sana na TIIS kumbuka ata mgomo uliperekea kuondoka kwa wakina Magabe na Marehem Mkiri wewe ulikuwa imformer wa serikali good day.
salaam,
Ukweli kuhusu mapinduzi ya 2003.
Alberto aliongoza mapinduzi ya kipuuzi akishirikiana na haka kajamaa basi nakumbuka tuliandamana.... Msando are you there? can you tell us what happened?
maneno hayo hapo juu yana mapungufu mawili. kwanza mapinduzi yale hayakuwa ya kipuuzi. Pili sikushirikiana na Deo Mtui katika mapinduzi yale.
Kwangu binafsi na wote walioshiriki mapinduzi yale inabaki kuwa historia ya pekee katika masha yetu ya Mlimani.
Kilichotokea siku ya tukio ni mkutano ulioitishwa kwa ajili ya kujadili hoja ya mikopo na malipo ya field. Kipindi hicho mimi sikuwa kiongozi kwenye serikali ya Daruso. Wakati mkutano huo unaendelea nilipita eneo la Rev Square nikakuta wanafunzi wamekusanyika na ndipo nikaombwa kupanda jukwaani kutoa muongozo!
Baada ya kupanda jukwaani nilwataka wanafunzi tuwatafute viongozi wa Daruso, Bwana Kayombo na serikali yake ili watoe majibu kwa wanafunzi lakini hawakuwepo popote! Tukawatafuta 'wabunge' (class representatives') na wao wakawa wameingia mtini!!
Baada ya hapo nikatoa wazo kwamba hatuwezi kuendelea na mkutano ule Rev Square hivyo tuhamie Nkurumah Hall!! Hoja hiyo ilikubaliwa tukaelekea Nkurumah!
Kufika uwanja wa vita tukamkuta Prof. Issa Shivji akiwa anatoa lecture kwa wanafunzi wa mwaka wa pili Sheria. Nikamfuata mbele nikamwambia Prof tuna kazi ya kufanya tunaomba microphone. Alichosema Prof 'kama ni suala la kudai haki Albert the floor is all yours'. akafunga vitabu vyake akatuachia Nkurumah wanafunzi wakashika nafasi zao.
Kipindi chote hicho Zitto alikuwa mjini pamoja na Omar Ilyas nadhani. Nikawapigia simu kuwaambia kwamba Nkurumah moto umewaka tukubaliane way forward. Zitto alikuwa wa kwanza kusema hakuna kurudi nyuma tuendeleze shughuli ile. Hivyo hivyo Omar Ilyas.
Wakati wote huo hakukuwa na kiongozi wa Daruso anayeonekana!! Mtu ambaye nilikuwa nashirikiana nae ni Emanuel Mvula na ndiye aliyepokea mikoba yangu ya lecture ambayo sikuweza kuhudhuria tena!!
jambo la kwanza tulilokubaliana ni kuchagua Raisi wa muda ili aweze kuendesha shughuli zile. Lilipendekezwa jina la Bwana mmoja anayeitwa Siriwa lakini wanafunzi walipiga kelele kupinga ndipo jina langu likapendekezwa. Wanafunzi wote wakaridhia nikabeba jukumu la kuongoza wanafunzi kuelekea ofisi ya Dean. Kipindi hicho alikuwa Mama Kitula ndiye Dean. Tulipofika ofisini mwake ikawa mchakamchaka akinilaumu kwamba mimii ndiye chanzo cha mgomo huku akijua kabisa mimi sikuzuia mikopo wala posho za field kwa wanafunzi!! Akizidi kunilaumu kwamba nimevunja katiba ya Daruso ambayo mimi ndie nilikuwa Spika (Zitto waziri Mkuu, Ruge Raisi, Omar Ilyas waziri wa Haki za binadamu na engineo wengi) wakti inapitishwa na nilichangia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa kwa kupitisha katiba hiyo.
Hayo yote hayakusaidia kwani baada ya malumbano ya muda mrefu wanafunzi walielekea ofisi za Daruso ambapo nilikabidhiwa rasmi desk la Kayombo. Kwa makusudi kabisa nikijua siasa za chuo niliwaashauri wanafunzi wote walioshiriki waweke saini zao na walifanya hivyo kuonyesha mshikamano!!
Muda ulikuwa umeenda sana tukakubaliana tulianzishe kesho yake. Kwa bahati mbaya siku iliyofuata hali ilikuwa tofauti! Usiku mapema polisi walizingira chuo ikiwa ni pamoja na vyumba vyetu vya kulala. Niliamka nikamfuata Zitto ambapo ikatulazimu kukimbilia Hall One kujificha. Kila aliyefungua chumba tulipogonga alipotuona alifunga mlango. Ikabidi tukimbilie Hall Three tukapata hifadhi kwa rafiki yetu mmoja (jina linahifadhiwa ni mke wa mtu sasa). Asubuhi Mary Mugurusi akaja kutuchukua kwenye gari yake akatupeleka Mabibo Hostel. Wakati tunapita maeneo ya Hall one polisi walikuwa bado wanarandaranda kututafuta! Tukaenda mpaka Mabibo Hostel tukapolewa na John Mnyika na rafiki yake Reginald. Hawa ndio watu waliotuhifadhi kwa muda na kutusaidia sana kwani tulikuwa choka mbaya!
Baada ya kujadiliana tuliamua kurudi chuo kudai barua zetu a kufukuzwa chuo. Tulipofika ofisi ya Dean akatuambia twende tukachukue Auxiliary polisi. Hapo shida ilianza ubishi kati ya Zitto na Dean kwamba kwa nini tukachukue barua polisi!! Ikabidi polisi waitwe watuletee barua zetu za kufukuzwa chuo!!
Tulipopokea tukaondoka na baada ya siku chache tulifanya mawasiliano na chuo tukaruhusiwa kufanya mitihani kwa masharti kwamba baada ya mitihani Disciplinary Hearing itafanyika kujua hatma yetu. Hayo yalifanyika. Kwenye Disciplinary Hearing tulikuwa tisa kama sikosei na baada yakutoa utetezi wetu mimi na Bwana Siriwa tulikuala 'rustication' ya miezi tisa!! wengine hawakukutwa na hatia.
Walichofanya uongozi wa chu ni kutugawa na walijua kabisa kwamba wanafunzi watakuwa busy na mitihani na baada ya hapo wataondoka kwenda makwao kwa hiyo uamuzi wowote usingekuwa na shida kutekeleza.
Wanafunzi waliporudi chuo hakuna aliyekumbuka kwamba Albert Msando na Siriwa wamesimamishwa kwa miezi tisa. Ikabidi kuanza kupambana kurudi chuo ili kumaliza Degree etu! Zitto na Omar wao walishamaliza hivyo chuo kikabaki na Bwana mmoja anaita Tweve kama mbishi aliyebaki na wengine wachache!
Baada ya kupambana tukarudishwa chuo kwa masharti makali kabisa. Kutokushiriki katika mkusanyiko wowote wa watu zaidi ya watano! Hata group discussion ikizidi watu watano inabidi tusishiriki!
Kwa kiasi kikubwa chuo kikawa kimepoteza hamasa ya migomo ya wanafunzi. Upole na sera za amani na utulivu zikatawala zaidi.
Wakati tunafika mwisho ukatokea Mgomo mwingine ambao na wenyewe haukufanikiwa. Nakumbuka Mabibo Hostel tulikusanyika baada ya mimi na John Mnyika kupanda gari usiku kutokea Morogoro kuwahi mgomo ambapo wanafunzi walijaa kwenye eneo la wazi la Mabibo lakini kuna gari iliingia getini wakadhani ni polisi hakuna alieybaki zaidi yangu na Mnyika! Kuanzia pale nikawaeleza wanafunzi hakuna wa kuendesha mgomo ukakamilika kutokana na woga ambao tayari umlishajengeka! Mnyika anawezakuuelezea zaidi mgomo huo!!
Mwisho, mgomo ambao ulikuwa na mafanikio ni ule ambao uliweza kushinikiza serikali kumuachia Marehe Gervas Mkil (RIP) na wanafunzi wengine wa Muhimbili kutoka rumande. Mgomo huo uliendeshwa na Zitto, Mimi, Rugemalira, Omary Ilyas na wengine siwakumbuki majina vizuri. Nakumbuka nilichaguliwa kwenda ITV kutoa Tamko kwamba wanafunzi warudi madarasani na Mkili atatoka. Nilienda na Raisi alieyekuwa anamaliza muda wake kwa jina la John wa Engineering (siyo John Kusaja). kitendo kile kidogo kiniletee shida kwa wanafunzi kwani wengi waliamini tumesaliti.
Nakumbuka nilikaa na Zitto nyuma ya Nkurumah hall tukiomba Mungu kwamba Prof Luhanga atimize ahadi yake ya Mkili kuachiwa!! Ahadi hiyo ilitimia na Mkili alisimama Nkurumah Hall akawasalimia wanafunzi! It was the happiest moment!
Tulitumia mafanikio hayo kumuuza Julius Rugemalira kama mgombea Urais dhidi ya Fundikira. Julius alishinda na Mkili na Fundikira wote walipewa wizara za kuongoza. Ila baada ya uchaguzi ule ambao uliwaingia madarakani baadhi yetu tuliokuwa tunaonekana ni wapiganaji matumaini ya wanafunzi yalipotea ghafla!!
Kutokuelewana kulianza mara moja, Raisi na Makamu, Zitto na Raisi, Albert na Zitto etc etc. Wan JF wengi wataelezea zaidi ile hali!!
Mpaka hapa niwachie wenzangu kusahihisha pale nilipokosea kutokana na kumbukumbu au vinginevyo!! Na pale ambapo nimesahau wengine waongezee kuweka historia sawa!!