Mapinduzi ya Zanzibar na Nyerere

Hizo ndio sababu za Nyerere kutaka kupewa utakatifu! kazi kubwa aliyoifanya ni kutaka kuuobdoa uIslam Tangamyika na Zanzibar, lakini kwa hilo hakufaulu. uIslam upo, utakuwepo na ndio dini ya mwanzo na ya mwisho katika dunia hii.
 
Wewe ndiye usiyejua kwamba Marekani wana interest na mafuta tu na ndio maana wanatoa misaada sana kwa baadhi ya nchi za kiarabu ili kuleta influence. Hayo ya udini huwa yanatumiwa ili kupata support ndio maana hata wewe unataja kuwa "damu za waislamu" bila kujali kama kuna watu wengine wasio waislamu wanaouawa!

sasa ndugu yangu afghanistan kuna mafuta gani? tatizo umeshakuwa brain washed ili uamini wanavyo taka wao lakini kwa akili iliyo salimika haiwezi kuamini propaganda kama hizi. Ndio maana hata Rais wa venezuela hugo chavez alisema sept 11 iliratibiwa na wamerekani wenyewe ili waweze kunyonya haki za wanyonge. angalia hii link Dailymotion - Hugo Chavez Says 9/11 was an Inside Job - a News & Politics video
 
Kimemuongelea Okello kuwa aliongoza mapinduzi kwa kutumiliwa.

Kimemchora kama mtu aliyepachikwa kupindua lakini hakuhusika na mipango yoyote. Kimesema kuwa Karume na Babu pia hawakujua mipango.

Mipango ilikuwa ni ya Hanga na Kambona.

Karume alikuwa Dar pamoja na Babu



Kitabu hicho kimemuongela mpiganaji John Okelo? Cjui kwa nn jamaa hakumbukwi, ni hila au nn jaman? Kwa sabab nackia wakati Okelo anawaondoa warabu Abed karume alikuwa Dar
 
Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 21
Peke yao Wazanzibari hawatojaribu kufanya kitu dhidi ya Tanganyika lakini wanaweza wakawaleta marafiki ambao wataweza kuwafanya wawe wakorofi. Zanzibar ilikuwa ni kituo cha kwanza cha ubeberu Afrika Mashariki. Uingereza ilichukuwa jukumu la kuulinda utawala huu [wa Zanzibar] na mantiki inasema kuwa baada ya Uingereza kuondolewa Tanganyika, Waafrika wa Zanzibar huenda wakauondowa utawala wa Kisultani.18
Mazungumzo hayo yalifanyika tarehe 27 Februari 1963 chini ya mwaka mmoja kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar. Nia ya Mwalimu Nyerere ya kuipinduwa Zanzibar ilikuwa imeshadhihirika kabla ya hapo lakini hilo lilikuwa kama tamko rasmi kwa Waingereza ambao hawakuonyesha kushituka au kukerwa na kauli hiyo. Jambo ambalo tutakuja kulieleza baadae kuwa ingawa Muingereza alichukuwa jukumu la kuilinda Zanzibar kabla ya uhuru alikataa kuilinda Zanzibar iliyopata uhuru na alipendekeza imezwe na Tanganyika ili awakomowe Wazanzibari walioupiganiya uhuru wao kwa kuungana na harakati za kikombozi dhidi ya Waingereza katika bara la Afrika.19
Upotoshaji mwengine mkubwa wa kihistoria ni kuwafanya watu waamini kuwa Waingereza, chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP), na Sultan Jamshid
walikuwa kitu kimoja na walipinduliwa pamoja tarehe 12 Januari 1964.
Msomaji anafaa pia akagutuka tena juu ya utumiaji wa neno “Muafrika” au
“raia” na kadhalika, na ujasiri wa kujipa haki wageni katika nchi ya Zanzibar isiyokuwa yao na utumiaji wa neno “Muafrika” kuhalalisha haki za wageni Zanzibar na kuwaharimisha wenyeji. Utumiaji wa neno “Mwafrika” ni kiini hai ndani ya simulizi nyingi za wazee ambazo utakuja kuzisoma huko mbele kuwa Mapinduzi ya Zanzibar hayakuwashirikisha wenyeji wa Zanzibar ambao si “Waafrika wa Zanzibar” kwa matumizi ya Mwalimu Nyerere ingawa katika hotuba ya Mwalimu ya 1995 aliweka wazi kuwa “hatuwezi kuwahishimu makaburu hapa [Tanzania] kwa sababu ni weusi tu.”
Zaidi ya nusu ya jamii ya Zanzibar iliyokuja kuvipigiya kura vyama va Zanzibar Nationalist Party na Zanzibar and Pemba People’s Party (ZNP na ZPPP) na kushinda kwa asilimia 46 ya kura na wingi wa viti 18 kati ya 31 katika uchaguzi wa Zanzibar wa Julai 1963 hawakuwa “Waafrika wa Zanzibar” kwa maana walikuwa ni Wazanzibari wa mchanganyiko wa damu na thakafa za Kiafrika na za Kiarabu na kwa mantiki hiyo haikutosha tu “Waafrika wa Zanzibar huenda wakauondowa utawala wa Kisultani” bali kuwauwa wale waliyoonekana kuwa si “Waafrika wa Zanzibar” yaani, Waarabu, Washirazi, nk. Mazungumzo ya Mwalimu Nyerere na Sir Pritchard yalikuwa tarehe 27 Februari 1963 na Mapinduzi yalifanyika tarehe 12 Januari 1964, yaani miezi sita kabla ya uchaguzi wa Zanzibar wa Julai 1963 na takriban mwaka mmoja kabla ya mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad anaelezeya kunako kitabu cha kumbukumbu ya maisha yake:
22 Mlango wa Pili
Julius Nyerere, Rais wa Tanganyika, ana sehemu ya lawama kwa mapinduzi ya Zanzibar. Aliamini kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanganyika na alianza kuyaingilia mambo ya Zanzibar mapema kuanzia katika miaka ya 1950…Mpaka sasa hivi, hadithi iliopo ni kuwa watu wa Zanzibar ndio walioyapanga mapinduzi, lakini kuna ushahidi kuwa Tanganyika ilihusika tena sana. Wengine wanaamini kuwa askari kutoka Tanganyika ndio waliyoyaongoza mapinduzi. Kwa kutumia ujanja, Watanganyika waliyagubika mavamizi kwa kuyafanya yaonekane ni mapinduzi, na ndio mwanzo wa matatizo ya Zanzibar kama ni dola.
Hisia yangu ni Nyerere alikuwa ndio kichwa nyuma ya mapinduzi. Ni vigumu kuziamini hadithi zenye kusema kuwa mwanzoni wanamapinduzi waliipinduwa serikali kwa mapanga tu; silaha walizozitumia zilitoka bara. Nyerere anabeba lawama pamoja na wanasiasa wa Kizanzibari kutoka pande zote mbili…Wanasiasa wetu wenyewe walimpa Nyerere fursa kuyaingilia mambo ya Zanzibar.20
Hisia za Maalim Seif zinalingana na matokeo ya utafiti na ushahidi kutoka kwa wazee wa ASP, TANU na CCM, kutoka Zanzibar na Tanganyika, waliohojiwa na mwandishi huyu na wenye kuufahamu uhakika wa mapinduzi ya Zanzibar. Hii ni dalili tosha kuwa uongozi na viongozi wa Kizanzibari na wa Kitanganyika ni kitu kimoja katika muelekeo na ufahamu wao wa kitendawili cha jinamizi lenye kuurusha usingizi Zanzibar kwa miaka arubaini na sita. Tafauti kubwa iko baina ya hisiya za Maalim Seif na “ushahidi” kutoka wazee wa ASP, TANU na CCM.
Kuanziya kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar; kudanganywa kwa marehemu Mzee Abeid Amani Karume na kutopewa fursa ya kushauriana na Wazanzibari wenzake kuhusu Hati za muungano; kujiuzulu kwa Mzee Aboud Jumbe; kuundwa kwa katiba ya CCM na kutiwa mnofu wa kisheria na Ilangwa Shahidi bila ya kuwashirikisha Wazanzibari; kufitinishwa marehemu Mzee Idris Abdulwakil na Maalim Seif Sharif Hamad; uingiaji madarakani wa Mzee Ali Hassan Mwinyi na kuondolewa kwa Idara ya Usalama ya Zanzibar wakati wa Urais wake; kuakhirishwa kwa Zanzibar kujiunga na OIC wakati wa uraisi wa Mwinyi na Dk Salmin Amour Juma; kugonganishwa Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kupitiya vyama vya siasa ambavyo vimewekewa sheria za kutoweza kuihoji mihimili ya Dola—Mapinduzi na Muungano; kuzama kwa mkono wa Bara ndani ya mambo ya Zanzibar halafu waowao kuombwa na baadhi ya viongozi wa Zanzibar wawe wasuluhishaji; mpaka kufikia Uraisi wa Dkt. Amani Abeid Karume na utetezi wa kuirudishiya Zanzibar haki zake za kinchi; ni mtiririko wa matokeo ya uvamizi wa Zanzibar ambao kwa mujibu wa maadili ya Nuremberg “ni kikomo cha jinai ya kimataifa kwa sababu unakusanya maovu yote yanayofuatiya.”
Zanzibar ya leo imeshaelekeya kuwa kitu kimoja na ni hikma na uwezo wa Mwenye Enzi Mungu ndio uliowafanya wazee wa Mapinduzi wazungumze na kuielekeza Zanzibar izungumze kwa sauti moja ndipo mtikisiko aliokuwa akiukhofiya Mwalimu Nyerere utakaposita na umoja wa Waafrika wenye asili na dini mbali mbali ndipo utakapoimarika na neema ya utajiri wa bara la Afrika
Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 23
kuwafikiya watu wake. Kila wakati wa binaadamu unakwenda kwa dhamira yake na wakati tulionao ni wa kujikombowa kutokana na upotoshaji wa ukweli wa historia ya Zanzibar baada ya kuvifahamu vyanzo nyake.
Mapinduzi Ndani na Nje ya Afro-Shirazi Party
Sheria mbili kati ya saba za chama cha Afro-Shirazi zinasema:
1. Kutafuta uhuru na utawala kamili utaokuwa miongoni mwa Dola zilizomo katika Shirikisho la Udugu na Dola ya Kiingereza…
2. Kuifanya na kuiamirisha Serikali ya Kidimokrasi katika visiwa vya Unguja na Pemba chini ya utawala na utii kwa Bwana Seyyid Mtukufu.21
Maneno yenye kuongoza kunako sheria mbili za chama cha Afro-Shirazi ni maneno “Shirikisho” na “utii kwa Bwana Seyyid Mtukufu.” Hizo zilikuwa ni sheria rasmi za chama cha ASP ambazo zilikubaliwa na viongozi wake na kukubalika kwa mujibu wa sheria za wakati ule.
Msomaji anatakiwa awe makini kabisa na hata kabla hajaendeleya kusoma inampasa afahamu kuwa viongozi wakubwa wa chama cha Afro-Shirazi, kama marehemu Mzee Abeid Amani Karume, na marehemu Mzee Thabit Kombo Jecha, au Sheikh Aboud Jumbe, hawakushiriki katika mipango halisi ya mapinduzi ya Zanzibar. Amekiri Mzee Jumbe katika kitabu chake The Partner-ship: Tanganyika Zanzibar Union: 30 Turbulent Years pale alipoandika kwenye kurasa 9–10 kuwa “ijapokuwa nilikuwa Katibu wa Mipango wa chama cha Afro-Shirazi, sikujuwa vizuri [kuhusu Mapinduzi] asubuhi ya tarehe 12 Januari 1964. Ilikuwa ni siri iliyohifadhiwa vizuri ambayo ilifahamika na uongozi wake [Karume] tu. Mpaka hii leo hadithi kamili imefungwa ndani ya nyoyo na kumbukumbu zao.”22 Mzee Jumbe amemuingiza marehemu Mzee Karume katika uongozi wa mapinduzi bila ya kutowa dalili au ufafanuzi wa aina yoyote.
Marehemu Mzee Thabit Kombo ambaye alikuwa chini ya marehemu Mzee Abeid Amani Karume pia ndani ya kitabu Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha kilichoandikwa na Minael-Hosanna O. Mdundo na chenye Utangulizi aliouandika Mwalimu J.K. Nyerere, amekiri kwa maneno yafuatayo:
Usiniulize vijana wetu walioendesha mapinduzi walipata wapi mafunzo, au nani hasa alivamia mahali gani; mimi sijui. Nasikia hadithi tu kila mmoja akijinasibu baada ya kushinda, mengi ya kweli na mengine ya uwongo mtupu.23
Mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wowote, mbali ya ule wa kinaga ubaga ambao unaweza kuthibitisha kuwa marehemu Mzee Abeid Amani Karume alikuwa jemedari wa Mapinduzi ya Zanzibar kama ilivyofanywa iaminike na kusadikiwa na wengi. Mara utasikia jemedari alikuwa Mzee Karume, na mara nyingine utasikia jemedari mkuu alikuwa ni “Field Marshall” John Okello. Mara
24 Mlango wa Pili
nyingine utasikia mpishi mkuu alikuwa marehemu Abdulrahman Mohammed Babu na nadhariya iliozamishwa ndani ya bongo za kila Mzanzibari na asiyekuwa Mzanzibari ni Mapinduzi yaliongozwa na Kamati ya Watu 14 au 13 + 1.
Hili ni jambo muhimu kuweza kuufahamu undani wake kwa sababu hapa ndipo kwenye kizungumkuti cha Mapinduzi ya Zanzibar. Hapa ndipo penye guo zito ambalo linatakiwa angalau ligeuzwe liwe chandarua. Kuanguka kwa Kamati ya Watu 14 kwenye chati ya Mapinduzi ya Zanzibar ni njia pekee ya kulivuwa guo la khadaa na kuirudishiya jamii nzima ya Kizanzibari na ya Kitanganyika nuru ya kufahamu inakotoka na kujipangiya inakotaka kwenda na kufika. Suala ni jee, Kamati ya Watu 14 walikuwa ndio viongozi wa mapinduzi ya Zanzibar au walikuwa ni walinzi wa kulilinda paziya la uongozi khasa wa mapinduzi?
Kati ya memba wa Kamati ya Watu 14 waliokuwa hai na wenye siha ya kuzungumza ni wazee Hamid Ameir na Abdalla Saidi Natepe. Katika mahojiano ambayo alifanyiwa Mzee Hamid Ameir katika gazeti la Mwananchi la tarehe 11 Januari 2008, mwandishi Salma Said alimuuliza “ni kwa nini wewe uko kimya kiasi hicho na hadi vizazi vya sasa haviutambui mchango wako?” Alijibu Mzee Hamid Ameir, memba wa Kamati ya Watu 14 kwa kusema:
Mimi sipendi kujitokeza kwa sababu kuna vitabu vingi sana tayari vimeshaandikwa kuhusu historia ya Sultani na kufanyika kwa Mapinduzi lakini cha muhimu zaidi ni kuwa unapojitokeza na kuzungumza wanatokea watu wanajibu hoja ulizozungumza na kuweka listi kubwa ya watu waliofanya Mapinduzi, nami kwa kuwa sipendi mabishano na kwa kuwa nafahamu kwamba kuna mtu siku moja ataandika historia ya kweli, hivyo mimi nimeamua kukaa kimyaa.24
Tarehe 8 Septemba 2002, alizungumza marehemu Mzee Khamis Daruweshi, memba mwengine wa Kamati ya Watu 14, na gazeti la Johari ya Mwananchi katika habari yenye kichwa cha maneno “Hamis Daruweshi afichua siri ya Mapinduzi Zanzibar”. Katika sababu alizozitowa Mzee Daruweshi za kufanyika mapinduzi Zanzibar ni kuwa watu wa Zanzibar “walikuwa hawataki kujinasibu kama Waafrika. Hawapendi kuunga mkono Waafrika na walikuwa wakiwaita wakata maji.” Daruweshi pia alielezea kuwa:
Huyu Okello alikuwa miongoni mwa Afro Shirazi [Youth] League. Tulimchukua Pemba alikokuwa akichonga mawe ili kutoa matufali. Tulimchukua kwa kazi maalum kwa sababu baada ya mapinduzi, tulijua tulihitaji mtu ambaye atatangaza mapinduzi hayo kwa lafudhi ambayo ni tofauti kabisa na ya wenyeji wa Zanzibar.25
Mzee Daruweshi alijifahamisha kuwa:
Mimi ni Myao, mtu wa Ruvuma, Tunduru, kijiji cha Masuguru, kata ya Malumba. Lakini hapa Zanzibar nimekuja zamani kidogo tangu mwaka 1941, niko hapa
Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 25
‘nimenationalize’ uraia wa Zanzibar. Nilipiga kura katika uchaguzi wa mwaka 1957. Lakini uchaguzi wa pili ikaja pingamizi kwamba wote waliozaliwa Bara hawatapiga kura. Ukijipanga kwenye mstari, wanakuja wakikuuliza, katika mstari walikuwapo mawakala wa Hizbu na wa ASP. Unaulizwa utamke ‘halua’, wengine hawawezi wanasema ‘haarua’ kwa hiyo wanakutimua kwenye mstari kwa kuwa wanajua kwamba wewe siyo Mzanzibari na kwa hiyo tuliotoka Bara wengi tukashindwa kupiga kura. Kwa hiyo nikaomba uraia wa Zanzibar Aprili 19 mwaka 1960 na kupewa kadi nambari 2020.26
La msingi katika mazungumzo ya Daruweshi ni kule kuelezea kwake bila ya kuweka ushahidi au vielelezo vyovyote vile kuwa: “Labda ni vyema ikajulikana tangu mwanzo kwamba kamati iliyoundwa na Karume ya kuongoza mapinduzi hayo, ilikuwa na jumla ya watu 14.”27
Walipotembeleya Cuba katika mwezi wa Mei 1964, Shirika la Habari la Cuba liliwafanyiya mahojiano memba wawili wa Kamati ya watu 14, Ramadhani Haji na Saidi Idi Bavuai yenye kutowa mwangaza mzuri juu ya maandalizi ya Mapinduzi ya Zanzibar. Baada ya kutowa historia fupi ya Afro-Shirazi kutokeya mwaka 1957 walielezeya matukio yaliofikiya kupinduliwa kwa Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah:
Uchaguzi ulipofanyika mwaka 1963 chini ya utawala wa kikoloni wa Kiingereza, chama cha Afro-Shirazi kilishindwa na kiliunda kamati ya kufanya mapinduzi. Baada ya uchaguzi kikundi kidogo cha chama cha Afro-Shirazi kiliungana na Chama cha Kizalendo (Nationalist Party).
Haya mapinduzi ya watu 14 hayakuungana wakati wowote ule na chama chochote chengine kikiwemo chama cha Afro-Shirazi…hata chama cha Afro-Shirazi chenyewe kilikuwa hakielewi kinachoendelea.28
Inaendelea ripoti ya Kiingereza juu ya ziara ya Bavuai na Haji:
Mchango wa kimapinduzi wa John Okello ulidharauliwa na Iddi na Haji na walisema kuwa mashirika ya habari yalikosea kumhusisha yeye kama ni kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar…Waliwaeleza Rais Karume na Waziri wa Mambo ya Nje Babu kuwa ni watu ambao hawakushiriki moja kwa moja katika harakati za mapinduzi, lakini hata hivyo, wanastahiki vyeo walivyokuwa navyo.
Inavyoonyesha, memba hao wawili wa Baraza la Mawaziri walishtukiwa na muungano wa Zanzibar na Tanganyika, na waliona haya kutamka chochote kuhusu maendeleo hayo huku wakieleza kuwa [muungano] umefanyika wakati wao wako nje ya Zanzibar.29
Mara nyingi imekuwa ikisikika kuwa Mzee Abdalla Saidi Natepe ameandika kitabu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar lakini hakitotolewa mpaka kufariki kwake. Hapa panaonekana kuna dalili kuwa mwanamapinduzi Mzee Natepe amekosa ushujaa wa kuandika kuhusu mapinduzi ya Zanzibar katika uhai wake na kuweza kuingiya katika midani ya mazungumzo wakati yungali hai.
26 Mlango wa Pili
Fikra iliyozoweleka na kushindiliwa ndani ya bongo za Wazanzibari na wasiokuwa Wazanzibari ni kuwa Kamati ya watu 14 ndiyo kamati iliyokabidhiwa kazi ya kuyapanga mipango ya mapinduzi na Mzee Karume. Hapana shaka memba wa kamati hiyo walihusika na mapinduzi na kama alivyosema marehemu Mzee Thabit Kombo “Usiniulize vijana wetu walioendesha mapinduzi walipata wapi mafunzo, au nani hasa alivamia mahali gani; mimi sijui. Nasikia hadithi tu kila mmoja akijinasibu baada ya kushinda, mengi ya kweli na mengine ya uwongo mtupu.”30
Sasa inawezekana kuwa Mzee Karume alikuwa jemedari wa Mapinduzi na msaidizi wake Mzee Thabit Kombo asiwajuwe vijana wa mapinduzi na awe amesikia hadithi tu. Lakini hili la “uwongo mtupu” ndilo linalofaa kutushughulisha. Ni uwongo gani huo wenye kuupotosha ukweli wa Mapinduzi ya Zanzibar? Uwezekano unaoingiya akilini na msomaji akawa ana uhuru wa kupima baada ya kumaliza kukisoma kitabu ni mambo mawili. La kwanza ni kuna utata wa idadi na majina ya memba wa hiyo Kamati ya Watu 14. Pili, na muhimu zaidi, inamkinika sana kuwa Kamati ya watu 14 iliundwa na kukwezwa baada ya Mapinduzi kwa lengo la kuufunika ukweli wa chimbuko la Mapinduzi yenyewe.
Tukirudi kunako kitabu maarufu na muhimu cha Mzee Aboud Jumbe The Partner-ship utakuta anwani yenye kusema “siasa za Zanzibar kabla ya muungano.” Mzee Jumbe anaelezeya kuwa:
Hata kabla ya Mapinduzi, Uongozi wa Siasa [wa ASP] ulikuwa haujaungana sawasawa. Kulikuwa na mvutano wenye kukuwa, kati ya wale, nikiwemo mimi mwenyewe, tuliomuunga mkono Karume, na baadae tukapewa jina la “Karume-Yeka”; na wale waliokuwa wakimpinga; na waliobakia waliojaribu kuyakubali makundi yote mawili. Mpasuko huu nusura ukivunje chama mwaka 1961 kwenye mkutano mkuu wa chama uliofanyika Municipal Hall, Mji Mkongwe.31
Kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu The Zanzibar Revolution and Its Aftermath, Anthony Clayton, “tarehe 2 Januari [1964] mivutano ndani ya A.S.P. ilikamilika pale walipojiuzulu Othman Sharif, Hasnu Makame, Idris Wakyl na Saleh Saadalla.”32
Bwana George Mooring, katika barua yake ya tarehe 29 Agosti, 1963, kwa
W. B. L. Monson wa Ofisi ya Makoloni, London, ameandika kuwa:
Imeripotiwa kuwa Moshe Feinsilber, Yahudi mwenye kuendesha biashara ya samaki hapa [Zanzibar], amejishughulisha na siasa kwa kuiunga mkono A.S.P. na yumo kujaribu kuwavutia viongozi wakubwa wa chama waachane na Abeid Karume na waungane na Othman Shariff katika jitihada zake za kuungana na Z.P.P.P. Ijapokuwa kikawaida maoni yake huwa yana uzito ndani ya chama, yeye [Finsilber] pia ameshindwa kukipeleka chama kwa Othman Shariff.
Wakati huu viongozi wa A.S.P. wamekuwa wakitembelea Dar es Salaam mara kwa mara kwa kupata ushauri, ambapo imeripotiwa kuwa washauri wao wakubwa ni Kawawa na Kambona. Inasemekana kuwa Watanganyika wameshinikiza kuwa
 
Kwa waliokisoma kitabu, kinazungumzia mauaji ya Karume?? Niliwahi kusoma mahali fulani kuwa hata karume hakuhusiaka kwenye mapinduzi na usiku wa mapinduzi yeye alikuwa dar na mapinduzi yaliongozwa na John Okello na inasemekana kuwa wapo wengi waliokufa baada ya mapinduzi sasa hapo tena nyerere atalaumiwa?? habari iko hapa Mapinduzi ya Zanzibar na historia inayotatanisha
 
..mara nyingi kiongozi wa mapinduzi ni tofauti na yule anayetangaza mapinduzi.

..hata katika vita kamanda mkuu hawezi kupelekwa mstari wa mbele.
 
Sijamaliza kukisoma lakini mpaka nilipofika naweza sema kuwa mwandishi wa hichi kitabu amefanya research nzuri sana. Kitabu kama hiki wakati wa Nyerere isingekua rahisi kuandika/kukipata. Huu ni wakati wa utanda wazi and therefore I think the history will be rewritten.

Wakati tunajadili hiki kitabu ni bora kuja na facts na sio hisia, kwa sababu mwandishi amekuja na mambo mengi with facts...

Ahsante mwandishi kwa kuweka hiki kitabu bure kwa mtu yoyote anayetaka kukisoma
 
Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 27
endapo Z.P.P.P. itakataa kujiengua kutoka Z.N.P. na kujiunga na A.S.P. basi A.S.P. iwe chama cha upinzani na isikubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na vyama vingine viwili [Z.P.P.P. au Z.N.P.]. Bahati mbaya ushauri huu umekubaliwa na A.S.P.; kwa vyovyote vile uwezekano wa kuundwa Serikali ya vyama vyote ya Umoja wa Kitaifa, umepotea.
Hapana shaka A.S.P. wameridhika kuwa mwisho wake, uzito wa kuungwa mkono na bara ndio utakaowaweka madarakani Zanzibar, na inawezekana ni imani hiyo kuliko kitu chengine chochote inayotuweka kwenye hali tuliyo nayo.33
Ripoti ya siri na kielelezo cha mukhtasari cha kitengo cha usalama cha Zanzibar cha tarehe 31 Julai–28 Agosti, 1963 kinamuelezeya:
MOSHE FINSILBER, mtu wa Israel Zanzibar, ambaye ni memba kamili wa A.S.P. Katika mikakati ilioelezewa katika kifungu kilichopita, [Finsilber] dhahiri amekuwa akimuunga mkono OTHMAN SHARIFF MUSA katika mkakati wake wa kuungana na Z.P.P.P. na amejaribu kwa uwezo wake wote kumvuta SALEH SAADALLA AKIDA na ABOUD JUMBE MWINYI kuachana na ABEID AMANI KARUME na kujiunga na OTHMAN SHARIFF MUSA. Lengo la FINSILBER, ni bila shaka, ni kukingowa chama cha Z.N.P. chenye kuongozwa na Waarabu ili kisiungwe mkono na walio wengi. Anatumia ushawishi wake mkubwa ndani ya chama [A.S.P.] kuondowa ushirikiano wowote ule wa serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itaihusisha Z.N.P.34
Ni dhahiri baada ya kukamata khatamu za serikali marehemu Mzee Karume aliwabadilishia kibao Maisraeli kwa kule kuwaunga mkono makhasimu wake ndani ya A.S.P. Anaandika William Edgett Smith kwenye kitabu chake Nyerere of Tanzania:
Israel, kwa mfano, ilikuwa iwe rafiki wa kwanza na wa karibu wa serikali mpya, kwa sababu Maisraeli walikuwa wachangiaji wakubwa wa chama cha Afro-Shirazi katika miaka kabla ya uhuru. Lakini, baada ya mapinduzi, Maisraeli walipojaribu kuanzisha mahusiano na serikali ya Karume, walikutana na upinzani mkubwa usiofahamika.35
Kwa upande wake, Mzee Jumbe ameonyesha kuwa mvutano ulikuwa baina ya ujumbe kutoka Pemba ambao ulishikiliya kuwa Othman Shariff awe Waziri Mkuu baada ya uchaguzi mkuu wa kabla ya uhuru wa Zanzibar. Mvutano huo, anaendeleya kuelezeya Mzee Jumbe, uliendeleya kufukuta na ulijitokeza kwa nguvu katika mkutano wa pili wa kikatiba uliofanyika jijini London. Anaandika Mzee Jumbe:
Karume alikuja kujuwa kuwa baadhi ya wajumbe wa ujumbe wake walikuwa wanataka kufanya urafiki na ujumbe wa serikali kwa lengo la kutaka kujuwa wangeliweza kupewa nafasi gani za uongozi wakiamuwa kutoka kwenye chama cha upinzani [ASP]…Karume alifupisha mazungumzo ya London na akaweza kuuondowa uwezekano wa mpasuko ndani ya safu ya chama.36
28 Mlango wa Pili
Mpasuko ndani ya ASP ambao Mzee Jumbe amejaribu kuuonesha ni mpasuko baina ya ujumbe wa ASP kutoka Pemba na ule uliokuwa chini ya uongozi wa Mzee Karume. Hakuna mahala ambapo Mzee Jumbe ameutaja upinzani wa marehemu Abdalla Kassim Hanga, Abdulaziz Twala au Saleh Saadalla Akida dhidi ya uongozi wa Mzee Karume. Wala hakutowa maelezo yoyote kuhusu TANU kama ilikuwa ikimuunga mkono Mzee Karume au kundi lipi lililokuwa dhidi ya uongozi wake ndani ya ASP. Kwa mujibu wa Mzee Abbasi, "TANU ilikuwa imeshachoka na hayati Mzee Karume na khasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Julai 1963."37
Katika kuthibitisha kutoelewana Mzee Karume na Mwalimu Nyerere, anaelezeya Profesa Issa G. Shivji, kuwa Mzee Aboud Jumbe anaelezeya kuwa baada ya daktari wa Kichina kumuambiya kuwa Mzee Karume alikufa palepale alipopigwa makao makuu ya A.S.P. Kisiwandui, Mzee Jumbe moja kwa moja alimpigiya simu Mwalimu Nyerere na kumwambiya:
Huku jambo kubwa limetokea. Yeye [Nyerere] akaniambia "Karume?" Nikasema "ndio." Akasema "basi nitaitisha Baraza la Mawaziri." …Sauti ya maelezo ya Mzee Jumbe ilitowa ujumbe kuwa Mwalimu Nyerere alikwishajuwa kuwa Karume ameshauawa Zanzibar kabla ya kuarifiwa na Mzee Jumbe.38
Kipindi cha kabla ya kuuliwa kwa Mzee Karume hali ya uhusiano baina yake na Mwalimu Nyerere ilikuwa mbaya kuliko wakati mwengine wowote ule.
Anaelezeya Shivji:
Kwa mujibu wa Jumbe [Karume na Nyerere] walikuwa hawazungumzi kwa mwaka mzima au kama hivyo kabla ya kuuliwa. Bhoke Munanka kwa upande wa Nyerere, na Jumbe kwa upande wa Karume, walikuwa wajumbe wa kupeleka na kurudisha habari. Salim Rashid amemuambia mwandishi [Shivji] kuwa alipokwenda kumuaga Karume baada ya kuwacha kazi serikalini siku moja kabla ya kuuliwa, Karume alimshauri kuwa asiwache kazi kwa sababu alikuwa anataka kuuvunja Muungano.39
Undani wa kuuwawa kwa marehemu Mzee Karume umeficha Mapinduzi kama kuundwa kwa Kamati ya Watu 14 kulivyolifunika kombe mwanaharamu apite. Nadhariya iliyopo ni kuwa waliyopanga kumuuwa marehemu Mzee Karume walikuwa wanafanya kazi ndani ya mpango ambao hawakuutambuwa undani wake. Maalim Seid Sharif Hamad ameandika kuwa "Baadhi ya watu wanafikiria kuwa Nyerere alimtumilia Babu na chama cha Umma kumuuwa Karume kwa sababu ikijulikana vizuri kuwa yeye [Nyerere] na Karume walikuwa hawana masikilizano mazuri."40
Alipohojiwa Babu na mwandishi wa televisheni wa Kiingereza alikiri kuwa Balozi wa Cuba aliyekuwepo Dar es Salaam alikuwa hajui chochote kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar kama alivyokuwa hakuyajuwa yeye. Babu aliyarudiya
Mirengo ya Kizalendo na Mapinduzi 29
maneno ya John Okello kwa kusema kuwa hakusaidiwa na nchi za kikoministi katika kuyapanga mapinduzi ya Zanzibar bali alisaidiwa na "Mungu wa Waafrika."
Jee, Waingereza hawakumuona "Mungu wa Waafrika" alipokuwa akiandaa kupinduliwa kwa Dola ya Zanzibar na badala yake waliamua kuwanyosheya kidole wana-Umma Party kutokana na imani yao kuwa ASP haikuwa na uwezo wa kufanya Mapinduzi bila ya Tanganyika? Na si hivyo tu, Mzee Karume, Babu na viongozi wengi wengine wakaipokeya sifa ya kuyaongoza mapinduzi na kumfunikia kombe "Mungu wa Waafrika?" Kama John Okello alikuwa ni mtu aliyekuwa na nyota mbaya iliyochomoza na kuanguka papohapo, na marehemu Babu na Karume walikuwa hawayajuwi mapinduzi lakini walijaaliwa kupata vyeo, watakuwa wamebakiya nani na kwa ushahidi gani ambao walikuwa viongozi wa mapinduzi ya Zanzibar? Ni Waafrika waliowapinduwa Waarabu Zanzibar au ni Waafrika waliowapinduwa Wazanzibari?
Takwimu za Kikabila Zanzibar
Ukiiweka kando propaganda inayolinganisha Ubantu peke yake na Uafrika utakuta Marais wakubwa wa Kiarabu wa Kaskazini ya Afrika, marehemu Gamal Abdel Nasser, na Ahmed Ben Bella ambaye yuhai, walikuwa upande wa ASP na TANU katika kuyafanikisha mapinduzi ambayo kijuujuu yamekuwa yamefahamishwa na kufahamika kuwa yalikuwa mapinduzi ya "Waafrika" wanyonge dhidi ya "Waarabu" mabepari wa Zanzibar. Kana kwamba hao Waarabu wote wa Zanzibar walikuwa matajiri na mabepari.
Akitumiya takwimu za Michael Lofchie, Profesa Issa G. Shivji ameeleza yakuwa asilimia moja (1) tu ya jamii ya Kiarabu ilokuwa ikiishi Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa katika tabaka la juu la kijamii, na asilimia 76 ya Waarabu walikuwa katika tabaka la chini. Kwa mujibu wa takwimu za kikabila za 1948 Waafrika Asilia (Washirazi) walikuwa asilimia 56.2, Waafrika kutoka bara walikuwa na asilimia 19.4, Waarabu asilimia 16.9, Wahindi asilimia 5.8, na Wangazija asilimia 1.2.41
La msingi si kutafautisha baina ya tabaka za Waarabu baina ya asilimia 1 na 76, bali kufahamu kuwa hawa Waarabu masikini za Mungu wa asilimia 76 waliokuwa wakiishi mashamba ndio walioubeba mzigo wa kifo na maangamizi katika mapinduzi ya 1964.42 Na hao hao Waarabu wa kawaida wa Kizanzibari waliokuwa wakulima, wavunjaji mbata na wazegazega hubebeshwa tuhuma za utumwa. Na katika hiyo asilimia 1 ya tabaka la juu na la kati la Kiarabu ipo haja pia ya kujiuliza Waarabu wa Zanzibar wakijiona kama raia au watawala? Kama watawala mbona hawajazijaza skuli za Kiarabu nchini? Mbona wengi wao walikuwa hawaijuwi lugha ya Kiarabu? Na nini mchango wa Waarabu katika kuijenga Zanzibar?
30 Mlango wa Pili
Leo Mji Mkongwe wa Zanzibar una heshima ya Kimataifa (World Heritage Site) uliopewa na shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa (UN). Wakfu wa mwanzo wa maji ya mji wa Zanzibar ulianzishwa na Sayyid Barghash bin Said bin Sultan. Mchango wa Wahindi hauelezwi vya kutosha na khasa katika kuigharimiya misafara ya utumwa, au kuipa misaada ya kifedha chama cha Afro-Shirazi, au hata mchango katika kazi za udobi, ukataji nywele, au kuuza vifuu. Na huenda sababu ikawa kutaka kuonyesha pengo la kibaguzi baina ya Waafrika kutoka bara (asilimia 19.4) na Waarabu (asilimia 16.9). Takwimu hazisemi asilimia ngapi kati ya Waafrika kutoka Bara na Waarabu walikuwa Wazanzibari kisheria au kinyume na sheria


hapa ndio mwisho wa sura ya pili
 
Waislamu huwa hawana jema toka kwa Mkristo hata siku moja, hata kama ukiwalamba nyuma watakudharau tu! Huwezi ukawasikia wanamlalamikia Dikteta Iddi Amin Dada wa Uganda pamoja na maovu yake yote simply kwa sababu alikuwa mwislamu! Similrly kwa magaidi kama akina Osama bin Laden, pamoja na unyama wote wanaofanya, kwao ni mashujaa! Hata hivyo si ajabu kwa sababu asili ya chuki waliyo nayo iko moja kwa moja ndani ya Quran (death manual)!

You are blinded by hate filled religion views. If you want the truth then you've to use your brains....
 
sasa ndugu yangu afghanistan kuna mafuta gani? tatizo umeshakuwa brain washed ili uamini wanavyo taka wao lakini kwa akili iliyo salimika haiwezi kuamini propaganda kama hizi. Ndio maana hata Rais wa venezuela hugo chavez alisema sept 11 iliratibiwa na wamerekani wenyewe ili waweze kunyonya haki za wanyonge. angalia hii link Dailymotion - Hugo Chavez Says 9/11 was an Inside Job - a News & Politics video

Mkuu,

Hivi karibuni kuna ripoti ya Pentagon ambayo inasema Afghanistan kuna minerals worth of trillions of dollars! Google unataona hiyo, inawezekana ni sababu ya wao kuingia huko. Natumai umesikia pia kuwa wanataka kuisaidia Uganda kumkamata Joseph konye. Why now? Mafuta ya Uganda na south Sudan!

Wamarekani wanaunga mkono ujenzi wa bandari mpya Tanga, hii nimeona thread humu JF. Si ajabu hata ile milipuko ya Kenya na Tanzania na upitishaji wa sheria za ugaidi na money loundering hapa Tanzania ni kazi ya Amerika kuweka maandalizi kwa shughuli zao siku za mbele.
 
Kwa waliokisoma kitabu, kinazungumzia mauaji ya Karume?? Niliwahi kusoma mahali fulani kuwa hata karume hakuhusiaka kwenye mapinduzi na usiku wa mapinduzi yeye alikuwa dar na mapinduzi yaliongozwa na John Okello na inasemekana kuwa wapo wengi waliokufa baada ya mapinduzi sasa hapo tena nyerere atalaumiwa?? habari iko hapa Mapinduzi ya Zanzibar na historia inayotatanisha

Kwa vyovyote vile Karume anastahiki kuitwa mmoja ya mashujaa wa mapinduzi.Hata kama siku hiyo alikuwa Dar pengine aliitwa kwa hila na Nyerere lakini yeye ni moja ya nguvu zilizoipinduwa serikali changa,ya kizembe na legelege ya Zanzibar.Harakati za Karume za kutaka kupindua yawezekana zilikuwa tofauti kidogo na zile za Nyerere na Kambona.
Karume mzanzibari mwenye asili ya Malawi alifanikiwa kuwakusanya na hatimae kuwatumia vijana wa kihuni waliokuwa katika vikundi vya ngoma vya ndala ndala na Tupendane pale Miembeni. Uvivu wa kufanya kazi na kupenda kula ilikuwa ni chambo alichotumia Karume kuwanasa vijana hao.Muda mrefu kabla serikali halali ya Zanzibar haijaundwa,Karume alifanikiwa kuwajaza fitna vijana hao kwa kutumia mianya ya ujinga wa serikali ya kisultani.
 
..mbona wanaotajwa asili yao ni wale waliotoka Bara tu?

..utasikia Mzanzibari mwenye asili ya Tanganyika,Msumbiji,Malawi...kule kwenye ngozi nyeusi tu.

..hata siku moja hutasikia Mzanzibari mwenye asili ya Oman, Yemen, etc etc.

..nadhani wa-Zenj waache kuuliza huyu katoka wapi na mambo mengine kama hayo.

..pia waachane kwa muda na kilichokea kabla[utumwa,umwinyi,..], wakati[mauaji..], na baada ya mapinduzi.

..kuna mambo ya msingi ya kushughulikia hapo Zenj na siyo haya mambo ya ku-dig about the past and pointing fingers.

..challenge moja inayowakabili wa-Zenj ni hii hapa: kati ya mwaka 1970 mpaka 1980 uzalishaji wa karafuu ulianguka toka tani 14000 mpaka 3000. nini kifanyike kuinua zao hilo ambalo ndilo uti wa mgongo wa uchumi wa Zenj?

..Zanzibar inatakiwa itafute sekta mbadala zaidi ya zao la karafuu itakayokuwa engine ya uchumi wa Zenj.

..badala ya kuhangaika na historia ambayo imejaa mambo mengi ya kusikitisha, wa-Zenj waungane kushughulikia future yao. tena sasa hivi kuna hii ahueni iliyotokana na serikali ya mseto wa CCM na CUF.
 
Wakati tunajadili hiki kitabu ni bora kuja na facts na sio hisia, kwa sababu mwandishi amekuja na mambo mengi with facts...
Naungana na wewe, mwandishi did something which is better than nothing, critique yangu kwa mwandishi, ameegemea mno fasihi simulizi, kwa wana fasihi, wanayajua mapungufu ya fasihi simulizi, mapinduzi yametokea 1964, huu mkusanyika wa simulizi miaka 40 baadaye unageuka ni hadithi tuu. Hizo facts unazosema ni facts mimi sizioni, ninachoona, ni mwandishi alishakuwa na premises zake akazitafutia proof kuzihalalisha.

Kitendo cha kutotumia andiko la John Okello ni udhaifu mkubwa wa kuukwepa ukweli, ili kuhalalisha kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ni mpango wa Nyerere.

Mengi sana yasasemwa kuhusu mapinduzi hayo, kwangu kubwa ni kuwa Karume na wanaye Ali na Amani, hawakuwepo Zanzibar, walikuja bara, akiwapeleka wanaye hao shuleni, wakisomea kwa babu yao Malawi!.
 
Hicho kitabu watunzi walimuuliza Nyerere, Okello, Karume na wengine juu ya Mapindizi ya Zanzibar au ni one sided story? Je, kuna document zozote mithili ya zile za WikiLeaks juu ya tukio zima au ni masimilizi ya wazee wanaokunywa kahawa kule Mji Mkongwe?
Kuna simulizi za wazee wanaokunywa mbege kule Tarime. Soma kitabu uelimike.!
 
Waislamu huwa hawana jema toka kwa Mkristo hata siku moja, hata kama ukiwalamba nyuma watakudharau tu! Huwezi ukawasikia wanamlalamikia Dikteta Iddi Amin Dada wa Uganda pamoja na maovu yake yote simply kwa sababu alikuwa mwislamu! Similrly kwa magaidi kama akina Osama bin Laden, pamoja na unyama wote wanaofanya, kwao ni mashujaa! Hata hivyo si ajabu kwa sababu asili ya chuki waliyo nayo iko moja kwa moja ndani ya Quran (death manual)!
iddi amini kwani dikteta? mbona hakuwahi kushtakiwa Mahakama ya kimataifa? hii ni propaganda ya nyerere kuwapiga waganda
 
Kwa vyovyote vile Karume anastahiki kuitwa mmoja ya mashujaa wa mapinduzi.Hata kama siku hiyo alikuwa Dar pengine aliitwa kwa hila na Nyerere lakini yeye ni moja ya nguvu zilizoipinduwa serikali changa,ya kizembe na legelege ya Zanzibar.Harakati za Karume za kutaka kupindua yawezekana zilikuwa tofauti kidogo na zile za Nyerere na Kambona.
Karume mzanzibari mwenye asili ya Malawi alifanikiwa kuwakusanya na hatimae kuwatumia vijana wa kihuni waliokuwa katika vikundi vya ngoma vya ndala ndala na Tupendane pale Miembeni. Uvivu wa kufanya kazi na kupenda kula ilikuwa ni chambo alichotumia Karume kuwanasa vijana hao.Muda mrefu kabla serikali halali ya Zanzibar haijaundwa,Karume alifanikiwa kuwajaza fitna vijana hao kwa kutumia mianya ya ujinga wa serikali ya kisultani.

Mkuu na hili la Karume kuwa dikteta na ya kwamba viongozi wengi hasa wale waliokuwa threat kwake walipotea katika mazingira ya kutatanisha baada ya uhuru unazungumziaje hilo??.......au hicho kitabu hakijagusia hilo??
 
Kitu kimoja ambacho ni kizuri kwa kitabu hicho ni kuwa kina maneno yake mwenyewe muandishi machache mno. ( chapters za introduction na conclusion tu).
Ningependa kujua kama hizo nukuu ni accessible. Yaani kama zinapatikana hata leo hii mtu akitaka kufanya uchunguzi
 
Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya Mapinduzi
Na Joseph Mihangwa - Raia Mwema toleo Na. 11
VISIWA vya Zanzibar vilipata uhuru wa bendera Desemba 10, 1963 kutokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Julai 8-15, 1963 pale muungano wa vyama vya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na Zanzibar and Pemba People`s Party (ZNPP)-ZNP/ZNPP ulipoibuka mshindi kwa viti 18 katika Bunge dhidi ya viti 13 vya chama cha Afro-Shirazi Party (ASP).
Kwa ushindi huo, Mohamed Shamte wa ZPPP aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar na Sultan wa Zanzibar Jamshid bin Abdallah Khalfa Harubu alibakia kama Mkuu wa nchi, mwenye mamlaka ya kuteua mrithi (Gazeti la serikali 1963).
Kilichoshangaza ulimwengu ni jinsi Serikali ya Shamte ilivyopinduliwa hima, siku 34 tu toka uhuru wa bendera, yaani Januari 12, 1964 katika mabadiliko sawia ambayo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanayaeleza kuwa ni ya aina yake katika nchi za Kiafrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, ukiondoa Guinea ya enzi za Rais Sekou Toure. Nini na kina nani ‘waliochochea’ mapinduzi hayo?
Wakati kuna majibu ya kutosha juu ya sababu ya Mapinduzi hayo, bado ni kitendawili ni nani aliyaanzisha na kuyaongoza kiasi kwamba suala hili limepata simulizi na tafsiri mbalimbali zinazokinzana na kuacha umma gizani.
Katika makala haya kwa kutumia vyanzo mbalimbali tutaelezea matukio yaa kabla, wakati na baada ya Mapinduzi, kuwawezesha wasomaji kupata angalau picha ya nini kilichotokea ili kuweza kujibu swali “nini na nani alichochea au kuongoza Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ambayo sherehe za miaka 44 ya kumbukumbu yake zinafanyika Jumamosi hii.
Harakati za uhuru Zanzibar kwa sehemu kubwa ziliendeshwa na vyama vikuu viwili –ZNP kilichoundwa Desemba 1955 na ASP kilichoanzishwa Februari 5, 1957.
Kati ya mwaka 1959 na 1963 kuelekea uchaguzi wa Julai 1963, mitafaruku ilizuka miongoni mwa wanaharakati wa vyama hivyo, Mohamed Shante akijiengua kutoka ASP na kuunda chama cha ZPPP ambapo Abdulrahman Mohamed Babu alijitoa ZNP na kuunda Umma Party (UP) chama cha mrengo wa kushoto.
Katika uchaguzi wa Julai 1961, ASP kilipata asilimia 49.9 ya kura zote, ZNP kilipata asilimia 35 na ZPPP asilimia 13.7. Hata hivyo, pamoja na ushindi wa kura ASP, kilishindwa kutamba katika viti vya bunge (LEGCO) kilipopata viti 10, ZNP 10 na ZPPP vitatu.
Uchaguzi huo ambao haukupata mshindi na ulifuatiwa na ghasia, zilizoacha watu 68 wakiuawa na wengine 400 wakiwa majeruhi. Watu 100 walikamatwa hivyo ilibidi urudiwe Julai, 1963, chini ya ulinzi mkali wa askari zaidi ya 100 waliwamo askari wa Kiingereza.

Matokeo ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifuatavyo muungano wa ZNP/ZPPP viti 18 na ASP viti 13 chama cha umma hakikugombea. Shamte alishauriwa aunde Serikali ya mseto kati ya ZNP/ZPPP na ASP ili kulinda umoja wa kimataifa, lakini alikataa kwa kiburi kwamba hawezi kukubali “kugawana mateka”
Sherehe za uhuru zilifanyika Desemba 9, 1961 zikihudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri kutoka nchi 70, akiwamo mwana wa Mfalme (Duke) wa Edinburgh pamoja na Aga Khan. Hakuna kiongozi yeyote wa Afrika aliyehudhuria.
Katika salamu zake za uhuru siku hiyo, Babu wa Umma Party aliwashangaza watu alipomaliza kwa kusema “umma wa Zanzibar na chama chao cha UMMA unasubiri kunyakua madaraka ya nchi saa itakapowadia”. Alikuwa na maana gani?
Serikali ya Shamte ilitoa haraka haraka madaraka makubwa kwa Wazanzibar katika Jeshi la Polisi, ambayo kabla ya hapo yalishikwa zaidi na Wamakonde kutoka Tanganyika na Msumbiji Kaskazini, ambao sasa waliachishwa kazi na kubakia Visiwani kwa uchungu bila kazi.
Mapema Januari 1964 (kabla ya Mapinduzi) Serikali ya Shamte ilikipiga marufuku chama cha UMMA na Babu akawa anasakwa kwa kosa la uhaini kwa kuhutubia mkutano wiki mbili kabla na kumshambulia Sultan na Serikali ya “kibaraka” Shamte. Kwa sababu hiyo alikimbilia Dar es Salaam kukwepa kukamatwa.
Tetesi za Mapinduzi zilianza asubuhi Jumamosi ya Januari 11,1964 ambapo Sultan Jamshid alidokezwa uvumi kwamba kungetokea machafuko siku hiyo usiku au kesho yake lakini kwa kuhakikishwa na waziri wa usalama kwamba huo ulikuwa ni uvumi usio namsingi aliamua kuupuuza.
Jioni ya siku hiyo askri wa kuzuia fujo Kambi ya Mtoni walipewa amri kwenda kuzuia fujo mjini Unguja umbali wa kilomita tatu wakabakia huko usiku huo. Ndipo vikundi vya wananchi viliposhambulia na kuteka Kituo cha Polisi cha Ziwani na kujipatia silaha na hatimaye kushambulia Kituo cha Mtoni kwa uraisi na kuteka silaha nyingi zaidi.
Hadi saa 11.00 alfajiri Vituo vya Ziwani na Mtoni vilikuwa vimesalimu amri, upinzani pekee ukibaki Kituo cha Malindi karibu na bandari ya Unguja.
Wakati huo huo Shamte aliendelea kutapatapa kuomba Uingereza ipeleke majeshi, lakini ombi hilo likakataliwa kwa sababu nchi hiyo haikuwa na mkataba wa ulinzi na Zanzibar. Alitumia ndege ndogo Pemba kuleta silaha lakini ilishindikana kurejea baada ya Uwanja wa Zanzibar kufungwa.
Saa 3.00 asubuhi Sultan Jamshind alitaarifiwa na watu wake kuwa majeshi ya Serikali yalikuwa yameshindwa na kwamba aondoke Zanzibar katika muda wa dakika 10.
Kwa kutumia ulinzi wa Kituo cha Malindi, Jamshid alitoroka jumba la kifalme akaingia kwenye boti iendayo kasi iliyoitwa Salama na kuingia kwenye meli “Seyyid Khalfa” kwenda Mombasa kutafuta hifadhi, lakini Serikali ya Kenya ikamkalia, akageuza njia kuelekea Dar es Salaam.
Siku hiyo ya Jumapili ambayo ndiyo ilikuwa siku kwanza ya Mapinduzi machafuko yaliendelea hadi mashambani kwa walalahoi kuwashambulia mamwinyi.

Asubuhi uvumi ulienea kwamba Mapinduzi yaliendeshwa na vyama vya UMMA na ASP, kwamba UMMA waliratibu oparesheni yote na ASP walitoa askari. Uvumi huo ulisema vijana wa Babu wanashirikiana na washauri kutoka Cuba.
Jioni ya siku hiyo, mtu mmoja mwenye sauti nzito, alitangaza kwa Kiswahili kupitia Radio Zanzibar na kujitambulisha (bila kutaja jina) kama “Field Marshal” alisema “sasa Zanzibar ni Jamhuri, vyama vya ASP na UMMA vitaunda Serikali mpya, Rais atakuwa Sheikh Abeid Amani Karume”. Katika hali ya kukanganya aliita kwa sauti ya kuamrisha “Karume (popote ulipo) rudi haraka kuchukua nafasi yako”
Inasemekana Karume aliondoka Dar es salaam siku ya Jumamosi kabla ya Mapinduzi kuanza au kushika kasi kwa madai ya kwenda kumweleza Mwalimu Julius Nyerer jinsi Mapinduzi yanavyofanyika na kufuatiwa na Kassim Hanga siku ya Jumapili asubuhi kwa madai ya kwenda kupata bunduki zaidi.
Itakumbukwa kuwa kwamba Babu wa UMMA alikuwa Dar es Salaam tangu alipotoroka huko kukwepa kukamatwa sasa kama wote hawa hawakuweao Zanzibar nani aliongoza Mapinduzi?
Kitu kingine kinachoshangazaa wengi ni kuwa katika orodha ya wajumbe 30 wa Baraza la Mapinduzi iliyotolewa baadaye jina la Okello ni la kwanza lakini Karume halikuwapo hata miongoni mwa majina ya wajumbe 14 wa Kamati ya Mapinduzi (Gazeti la Serikali , Januari 25, 1964).
Usiku siku hiyo Mwalimu Nyerere alionana na Karume Ikulu na kumshauri arudi Zanzibar mara moja baada ya kuona hapakuwa na sababu ya yeye kuwa Dar es Salaam.
Siku ya pili; Jumatatu Januari 13:
Asubuhi “Field Marshal”alijitambulisha kama kawaida kupitia redioni kwa jina la John Okello kisha kwa sauti yenye mamlaka akaendelea kusema: “Sultan amefukuzwa mguu wake hautakanyaga tena ardhi yetu, jumba lake na mali yake itataifishwa” kisha akaiomba Serikali ya Tanganyika ipeleke ndege nzima ya dawa na kuwataka wauguzi wote warudi kazini.
Aliendelea kutamba: “Nitachukua hatua kali, kali mara 88 zaidi, hakuna ruhusa mtu kuacha mke wake atakayefanya hivyo atapata viboko 65; Sultan alikuwa shetani na kibaraka wa mabepari. Mtu atakayejaribu kuwa mnafiki atafungwa miaka 50, atakayeiba hata mche wa sabuni atafungwa miaka minane. Mimi ni Field Marshal naweza kutengeneza mabomu 800 kwa saa moja”
Siku hiyo mchana, Oscar Kambona, Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa Tanganyika, alimpigia simu Rais Nyerere kutoka Nairobi kumjulisha kuwa Kenya na Uganda zimeitambua Serikali ya Mapinduzi na kumwomba aitambue pia bila kumeza maneno Nyerere alikataa kwa kuwa hakuwa na hakika kwamba Karume na ASP walikuwa wameshika hatamu na kwamba hakuyapendelea mauaji yaliyokuwa yakiendelea.
Kwa mujibu wa Okello baadaye alieleza kuwa watu 9,999 waliuwawa lakini kulikuwa na taarifa nyingine za kuwa walikuwa ni 200, japo taarifa za Mzungu mmoja Visiwani zilikadiria watu 6,000 kuwa waliuawa.
Vivyo hivyo katika simu hiyo Kambona alimjurisha Nyerere juu ya Sultan Jamshid kukataliwa kutia nanga Mombasa na kumshauri naye asimruhusu, hata hivyo, Nyerere alimjibu Kambona kuwa hakuwa na ugomvi na Sultan, kwa hiyo, hakuwa na sababu ya kutomruhusu nchini.

KARUME na John Okello

Karume na Hanga waliondoka Dar es salaam kutokea eneo la “Silver Sands” saa 8.00 alfajiri (saa 24 baada ya Mapinduzi kwanza) kuelekea Zanzibar kwa boti ya Fainzilber na kufika Zanzibar saa 6.30 baadaye eneo la Kizimkazi asubuhi ya Jumanne waliomba na kupata usafiri wa gari la mwalimu mmoja wa shule na kwenda moja kwa moja eneo la Raha Leo na kulakiwa na “Field Marshal” wakala chakula pamoja.
Siku ya tatu; Jumanne Januari 14:
“Field Marshal” John Okello alitangaza kupitia redio kwamba mawaziri wanne wa Serikali ya zamani watanyongwa, lakini Karume alipinga siku iliyofuata (Januari 15) kwamba hakutakuwepo kulipiza kisasi.
Siku hiyo Mwalimu Nyerere alikwenda Nairobi kuonana na Waziri Mkuu wa Kenya, Jomo Kenyatta, kuzungumzia uundwaji wa shirikisho la nchi za Afrika Mashariki. Ni katika ziara hiyo Mwalimu alipoanza kubaini kwamba Jomo Kenyatta hakuwa na shauku ya kuundwa kwa shirikisho hilo ambalo ndoto yake haijatokea kuwa ya kweli hadi leo.
Siku ya nne; Jumatano Januari 15:
Sultan Jamshid aliyekataliwa kutia nanga Mombasa na Serikali ya Kenya alitia nanga Dar es Salaam na kuruhusiwa na Mwalimu Nyerere kukaa nchini hadi alipokamilisha mipango yake ya kukimbilia uhamishoni Uingereza siku nne baadaye.
Siku ya tano Alhamisi Januari 16:
Huku “Field Mashal” Okello akiendelea kutoa matangazo mbalimbali kupitia radio, Karume, Babu na Hanga waliondoka kwa ndege kwenda kuonana na Nyerere kumwomba aitambue Serikali yao na kuomba askari wachache kuweza kurejesha amani na utulivu Visiwani. Siku mbili baadaye askari 300 waliwasili Zanzibar.
Okello pengine bila kufahamu juu ya safari ya Karume, Babu na Hanga, alitangaza redioni kulalamika kwamba alifanya makosa kumteua Karume kuwa Rais kwa sababu hakushiriki hata kidogo katika mapambano, hivyo siku hiyo, Okello alijipa mwenyewe cheo cha Rais na kumtangaza Karume kuwa makamu wake.
Mchana “Field Marshal” Okello alitembelea makao makuu yake yaliyokuwa kwenye Jumba la Manjano, Raha Leo ambako umati mkubwa wa watu ulikuwa ukimsubiri kumwona akiwa amevaa mavazi meusi ya kijeshi, mara alipojitokeza tu umati ulizizima kwa shangwe na kupiga kelele “Jamhuri! Jamhuri!.......”
Siku hiyo Okello alikaribisha wageni wa kimataifa na kwa msaada wa mkalimani alizungumza kwa kirefu habari za maisha yake na jinsi alivyopanga Mapinduzi ya Januari 12 bila kumwambia Karume wa sababu angeyazuia kutokana na ukweli kwamba bado alikuwa na matumaini ya kufika mwafaka na Shamte wa kuunda serikali ya mseto.
Huko nyuma Karume alimtumia Shamte ujumbe mara mbili kumbebeleza akubali lakini Shamte alikataa kata kata akitaka ASP kivunjwe.
Siku ya nane; Jumapili Januari 19:
Siku ya sita na ya saba, Okello aliendelea kutangazia umma juu ya Mapinduzi na matarajio yake kama kawaida lakini siku ya nane aliondoka kwenda Dar es Salaam kama mapumziko kidogo baada ya kazi kubwa. Usiku huo alionana na Mwalimu Nyerere Ikulu na alishauriwa kufanya kazi kwa imani na Rais Karume. Aliporejea Zanzibar siku moja baadaye aliambiwa anatakiwa Dar es Salaam. Nyerere alimkamata Uwanja wa Ndege wa Dar es salaam na kurejeshwa kwao Uganda.

Kwa hiyo wanaharakati hawakuyatambua matokeo ya uchaguzi wa 1961 na 1963 na kwamba ASP kilidai kupokonywa ushindi. Lakini swali juu ya nani aliongoza Mapinduzi ya Januari 12 halijapata jibu.
Tunaambiwa kuwa ni Mzee Karume aliyeongoza mapambano, lakini hoja hii imejaa ukingu baridi na maswali tele kwa nini alikimbilia Dar es Salaam kabla au mara Mapinduzi. Kama ilikuwa ni kumjulisha Mwalimu Nyerere juu ya Mapinduzi kama alivyodai kwa nini asingepiga simu?
Kwa nini Nyerere hakuyatambua Mapinduzi mapema na kwa haraka kama zilivyofanya Kenya na Uganda? Kwa nini alimhifadhi Sultan Jamshid kwa chukizo la Karume na wanamapinduzi? Kuundwa kwa serikali ya mseto kati ya ASP na Umma kunaonyesha nini juu ya Mapinduzi? Na kama tutakataa kwamba Okello ndiye aliyeongoza Mapinduzi kwa nini aliruhusiwa “kutamba” kwenye radio ya Serikali (mpya) kwa siku nane mfululizo?

Na kama tutakubali kuwa Okello ndiye aliyeongoza na hatimaye Karume (ASP) na Babu (Umma) wakaunda serikali ya mseto Karume akiwa rais na “Field Marshal “ John Okello akatupwa nje; je, tuseme hatua hiyo yalikuwa Mapinduzi ndani ya Mapinduzi?


Zifuatazo ni ushahidi katika picha - kuna anayebisha ?


Okello.jpg REVOLUTION+PIX.jpg
Ingawa mwanzoni Field Marshall John Okelo alitangaza kuwa amemteua Karume kuwa Raisi wa Zanzibar, baada ya kuuonja utamu wa madaraka, aliamua Karume awe Makamu Wake. Hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya Karume kuomba msaada kutoka nje ya Zanzibar aweze kumwondoa Okelo kwani hakuwa na ubavu wala ujasiri wa kufanya hivyo. Kwa mara ya pili na kwa msaada wa Mwalimu, mapinduzi mengine ndani ya mapinduzi yakawezekana baada ya Okelo kuhadaiwa kuja Dar es Salaam. Bila hivyo historia ya Zanzibar ingekuwa nyingine kabisa na wazushi kama huyu Harith Ghassany hawangepata nafasi ya kuandika na kueneza hizi hadithi zao.
 
Back
Top Bottom