Mapinduzi ya Zanzibar: Mchango wa John Okello (Che Guevara wa Afrika Mashariki) umefutwaje?

In the middle

Okello-and-supporters-.jpg
 
Nilipata kuijua historia ya Zanzibar mwaka 2006,nilisikitika sana. Kuna matukio makubwa yanayoweza kukutoa chozi ukifuatilia upande wa pili wa Tanzania! Pia sihafiki historia ya kweli ya Tanzania kufundisha shuleni,vingnevo baada ya darasa watoto wanaweza kuingia mtaani kwa mapinduzi ya pili.

Ukiangalia watu aliowafukuza mwl.Nyerere baada ya uhuru kwamba walikuwa wanaandaa mapinduzi pale mkwajuni kindoni,ukisoma jinsi dr.Ahammed Salimu anavohusishwa na zanzibar, worse uyu John Okello, ni majonzi matupu! Mwaka 2006 walitoa habari ya Maisha magumu ya Field Marshall John Okello alivokuwa anaishi Kenya surbubs, hamna Mtanzani hata mmoja alijitokeza kujua mambo yake.

Mwaka 2007 nilienda pale Vijana Hostel karibu na Mango Garden, ndo tulipokuwa tunalaza gari wakati ule, nilikuta ukuta wa hostel umejazwa picha za John Okello akila shida uko Kenya, yani niliona ajabu kubwa! Jamani uyu mtu hajafa,nahisi bado yu hai kenya,unless mtu alete taarifa ya Kifo chake, ikiwezekana wapenda historia tumtafute! Ni hayo wanaJF!
 
alsaidy,
Samahani sana lakini Ghassany kachakachua historia. Huwezi kuandika historia based on heresay.

Mkuu Jasusi,

Sijui umepata muda wa kukipitia kitabu chote au labda una mashaka na maandishi yake?

Mimi binafsi nina amini kabisa ni ukweli kilichoandikwa beside reference zake baadhi ya watu wanasema ni hadithi za kusimuliwa.

If that is the case naomba mwenye Historia ya kweli ambayo inapingana na ya Harith Ghassany atuwekee hapa watu wapate kuchambua na mtu mwenyewe apate kuamua which History to follow based on source.
 
Jasusi, at this stage nani atakuwa na historia ya kweli? Kitabu cha Ghassany sijakisoma chote lakini wengi wa aliowafanyia interview walikuwa wameshuhudia hayo mapinduzi na baadhi walishiriki.Nadhani katika wanamapinduzi original basi ni Ramadhani Haji tu ndiye aliye hai na hivi sasa ni mzee sana na akili zimeshakimbia.

Okello alikuwa kibarua mchonga mawe tu na ushahidi upo mpaka leo nenda pale soko la Chake Chake yale mawe ya kuchongwa yaliyowekwa ni kazi ya Okello. Yeye hakuwa Mzanzibari by any standard (hata hiyo ya kikoloni) na alikuja kama kibarua. Kuna Mzee mmoja sasa hivi marehemu aliwahi kunieleza vipi Okello alipata ile tetesi ya matayarisho ya Mapinduzi.

Inasemekana alisikia watu wanasema siri zao na yeye akasema yuko tayari kujiunga ili kumpinga Mwarabu. Alilazimisha kujiunga na kwa kuogopa siri isije kutoka basi ikabidi wamuingize kwenye mpango huo. Bahati yake ni kwamba yeye aliwahi kuwa askari huko anakotoka ijapokuwa hajawahi kukubali hata siku moja (soma kitabu chake).

Alizidisha vitisho kila mtu alitaka kumchapa viboko elfu tisa, mia tisa na tisini na tisa (soma kitabu chake) mpaka ikawa hamkani Zanzibar hakukaliki ni viboko tu. Sasa kama mtu mwenyewe siyo raia si afukuzwe tu.

Ukisoma kitabu cha Clayton utaona kwamba mpango wa kumuondoa ulipangwa na Karume na Nyerere kwa pamoja, kwani aliambiwa anaitwa Tanganyika na alipoondoka tu basi huku nyuma aliambiwa asikanyage Zanzibar kwa vile si raia. Alipofika Dar akaambiwa yeye si raia na hatakiwi hapo, akaishia Kenya ambako aliwekwa Shimo la Udongo wakati mipango ya kumrejesha kwao Uganda inaendelea.

Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.
 
Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.


Okello then stayed in Kenya, in Congo-Kinshasa and in Uganda. He was incarcerated multiple times and was last seen with the Ugandan president Idi Amin in 1971 and vanished afterwards. In the book "Revolution on Zanzibar", written by Don Petterson, it is more or less assumed that Idi Amin saw him as a threat (after Amin promoted himself, Okello reportedly joked that "now Uganda has two field marshals") and had arranged his assassination. This remains speculative, however.
 
maprofessa mahiri wetu mko wapi kwa historia ya kweli,upo wapi haroub othman,proffesa mazrui, baregu na wengine tele wasomi..wanazuoni.

Historia ya mataifa yetu hapa afrika mashariki imepindishwa ,andileni upya.....
kwa nini tunawafundisha watoto ...uwongo..
Hilo nalo neno! Kwanini historia ya Tanzania inapindishwa karibu kila eneo?
 
Jasusi, at this stage nani atakuwa na historia ya kweli? Kitabu cha Ghassany sijakisoma chote lakini wengi wa aliowafanyia interview walikuwa wameshuhudia hayo mapinduzi na baadhi walishiriki.Nadhani katika wanamapinduzi original basi ni Ramadhani Haji tu ndiye aliye hai na hivi sasa ni mzee sana na akili zimeshakimbia.

Okello alikuwa kibarua mchonga mawe tu na ushahidi upo mpaka leo nenda pale soko la Chake Chake yale mawe ya kuchongwa yaliyowekwa ni kazi ya Okello. Yeye hakuwa Mzanzibari by any standard (hata hiyo ya kikoloni) na alikuja kama kibarua. Kuna Mzee mmoja sasa hivi marehemu aliwahi kunieleza vipi Okello alipata ile tetesi ya matayarisho ya Mapinduzi. Inasemekana alisikia watu wanasema siri zao na yeye akasema yuko tayari kujiunga ili kumpinga Mwarabu. Alilazimisha kujiunga na kwa kuogopa siri isije kutoka basi ikabidi wamuingize kwenye mpango huo. Bahati yake ni kwamba yeye aliwahi kuwa askari huko anakotoka ijapokuwa hajawahi kukubali hata siku moja (soma kitabu chake).

Alizidisha vitisho kila mtu alitaka kumchapa viboko elfu tisa, mia tisa na tisini na tisa (soma kitabu chake) mpaka ikawa hamkani Zanzibar hakukaliki ni viboko tu. Sasa kama mtu mwenyewe siyo raia si afukuzwe tu.

Ukisoma kitabu cha Clayton utaona kwamba mpango wa kumuondoa ulipangwa na Karume na Nyerere kwa pamoja, kwani aliambiwa anaitwa Tanganyika na alipoondoka tu basi huku nyuma aliambiwa asikanyage Zanzibar kwa vile si raia. Alipofika Dar akaambiwa yeye si raia na hatakiwi hapo, akaishia Kenya ambako aliwekwa Shimo la Udongo wakati mipango ya kumrejesha kwao Uganda inaendelea.

Baadae walimrejesha kwao Uganda na kwa vile alikuwa na reputation ya kufanya Mapinduzi (theory mpya kwa wakati ule) basi alipokewa kwa suspicion kubwa sana hata huko kwao Uganda. Maisha hayakuwa mazuri kwake na baadae inasemekana alifariki.

Asante ila umeandika kishabiki zaidi na sijui lengo ni nini hapa!

Umemdharau Okello, na kusema vitu vingi ambavyo unajicontradict mwenyewe! tafuta na andika historia sahihi, na ushabiki usiwepo hapa, unacholinda ni nini?

Okello ndiye aliyeongoza mapinduzi, kwa taarifa yako video za kipindi hicho zipo!

Okello unayemdharau ndiye aliyemkabidhi Karume na Babu nchi! tena kupitia redioni, I mean kama angekuwa na tamaa ya madaraka alikuwa ameisha kiteka kisiwa!!

Jina la Okello litabaki kuwa ni symbo na ni watu ambao baada ya kutumika na Nyerere na Karume walikuwa dumped!!

Ukweli unabaki kuwa
Shamte ndiye baba wa taifa la Zanzibar
Ukweli unabaki Nyerere amefuta historia za heroes wengi wa Tanzania kumzidi yeye

Karume+Nyerere =unapata wahuni fulani tu waliotutawala na leo tuna suffer matendo yao!

.........Okello then stayed in Kenya, in Congo-Kinshasa and in Uganda. He was incarcerated multiple times and was last seen with the Ugandan president Idi Amin in 1971 and vanished afterwards. In the book "Revolution on Zanzibar", written by Don Petterson, it is more or less assumed that Idi Amin saw him as a threat (after Amin promoted himself, Okello reportedly joked that "now Uganda has two field marshals") and had arranged his assassination. This remains speculative, however.

unajifagilia na hiyo avatar!! umesema speculations sina comment na kama ni kweli ilikuwa hofu yako tu (avatar) kwani Okello alikuwa siyo mroho wa madaraka!
 
Bwana Phillemon, tafadhali tafiti kwanza kuliko kuegemea historia ya mapinduzi ambayo imejaa utata mtupu. Mimi sikubaliani na mtazamo wako kumfananisha Okello na Che Guevara ni upofu! Tafuta ukweli. Nchi hii ina mashujaa wa kweli ambao wamezimwa makusudi na hawajulikani kwa kizazi cha sasa.
 
Wakati huo huo tusisahau kuwa wengine ambao tunalazimishwa kuwasahau ni
Abdulwahid na Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Tewa Said Tewa,Ali Migeyo , Suedi Kagasheki,Dossa Azizi,Abdulkarim Karimjee,Chifu Abdieli Shangali wa Machame, Kleist Sykes,Ally Sykes na Abdulwahid Sykes

kwa uchache sasa huyo Okello alikwa ni just one in a million na at least eyey leo anazungumzwa,




umenikumbusha mbali sana haya majina...kn wanaosema waislam ndiyo walianza harakati za kudai uhuru? nisaidieni maana kuna jamaa yangu mmoja ana udini sana hasa katika suala la historia ya uhuru..
Kuna wengine wawili waliosahauliwa, hawa ni Robert Makange na jamaa mwingine akiitwa Baghdelah walifungwa jela na mkoloni katika harakati za uhuru.
 
Field Marshal John Gideon Okello (1937, Wilayani Lango Uganda – 1971?) Alikuwa ni mwana mapinduzi wa Afrika ya Mashariki na Kiongozi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyo mng'oa Sultan Jamshid Bin Abdulah.

Maisha yake

Alianza kuishi maisha ya uyatima akiwa na miaka 11. Alipofikisha umri wa miaka 15 aliondoka nyumbani kwao na kwenda kutafuta ajira katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki.

Kuanzia mwaka 1944 alikuwa amefanya kazi nyingi ikiwa ni pamoja na ukarani, mtunza bustani na mfanyakazi katika idara na shughuli mbalimbali.

Hata hivyo, alijifunza kufanya biashara ya kuuza matofali na baadaye alimudu kufanya kazi ya uashi, lakini alikamatwa mjini Nairobi, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa; hata hivyo yeye mwenyewe aliwahi kuelezwa kuwa alikamatwa kutokana na makosa yaliyohusiana na hali ya jinsia. Alifungwa miaka miwili gerezani. Kifungoni ndiko kulikomfanya awe na fikra za kimapindizi.
Mara nyingi umekuwapo uvumi kuwa huenda Okello alikuwa amepata mafunzo yake nchini Cuba, lakini jambo hili halikuwahi kuthibitishwa na Okello mwenyewe.

Mapinduzi

Mwaka 1959 aliingia kisiwani Pemba katika harakati zake za kutafuta ajira kwenye mashamba ya karafuu, lakini badala yake alijiunga na jeshi la polisi.
Hata hivyo, baadaye alijiunga na Chama cha Afro-Shirazi kilichokuwa kinapinga jamii ya watu wachache kuhodhi uchumi wa Zanzibar na Pemba.

Inaelezwa kuwa Okello alikuwa muumini mzuri wa dini. Aliamini kuwa alipewa amri hizo na Mungu akiwa kwenye ndoto kuuondoa utawala wa mabavu wa Waarabu na kuanzisha serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Pemba.
Usiku mmoja kabla ya mapinduzi hayo, Okello aliwaamuru watu wake kuua vijana wote wa Kiarabu waliokuwa na umri kati ya miaka 18 na 25, lakini wasiwadhuru kina mama wajawazito na wazee na pia wasifanye ubakaji.

Januari 12, 1964 akiwa anaungwa mkono na asilimia kubwa ya watu waliokuwa wanakandamizwa – wengi wao wakiwa Waafrika – Okello na kikosi chake waliweza kuingia katika mji wa Stone Town, Zanzibar, kulikokuwa maskani ya Sultan.

Inaelezwa kuwa takriban watu 10,000 waliuawa, licha ya kwamba kikosi cha Okello kilikuwa na silaha duni. Okello na kikosi chake walilishangaza Jeshi la Polisi Zanzibar na kuchukua ofisi zao.
Kwenye hotuba yake iliyotangazwa kwa njia ya redio, Okello alitangaza kuwa yeye ni ‘Field Marshal wa Zanzibar na Pemba' na alimwamuru Sultan aue familia yake na kisha ajiue mwenyewe, la sivyo Okello ataifanya kazi hiyo mwenyewe.
Hata hivyo, Sultani mwenyewe alikuwa tayari ameshajipatia maficho ya usalama nchini Uingereza, na waziri mkuu pamoja na mawaziri wengine pia waliwahi kutoroka.

Kuwekwa pembezoni
Kutokana na kufanikiwa kwa mapinduzi hayo, Okello alitangaza Baraza la Mapinduzi na Sheikh Abeid Amani Karume kuwa Rais. Kiongozi wa Chama cha Umma, Abdulrahman Mohamed Babu, akawa waziri mkuu. Baadaye alikuja kuwa Makamu wa Rais.
Sheikh Karume na Babu hawakuwa wamejulishwa kuhusu mapinduzi hayo ya kijeshi kwani wote walikuwa Tanganyika, lakini walirudi Zanzibar walikokaribishwa na Okello.

Lakini pamoja na shughuli yote aliyoifanya si Karume wala Babu waliomhitaji tena. Okello aliondoka kuelekea Tanganyika na kuanzia wakati huo alizuiwa kurudi Zanzibar na alipigwa marufuku pia asionekane Tanganyika na Kenya.

Kutengwa

Kuna wengi walifanya mambo yanayofanana na Okello. Miongoni mwao ni Ernesto Guevara de la Serna maarufu kama Che Guevara, aliyeshiriki kikamilifu kwenye mapinduzi ya Cuba licha ya kwamba alikuwa ni mzaliwa wa Argentina.
Leo hii Che Guevara ni jina linalosifika na kuheshimika nchini Cuba kutokana na mchango wake. Haiyumkiniki jina la Okello nalo lingekuwa ni jina la kuheshimika kwenye na kukumbukwa kwenye Mapinduzi ya Zanzibar lakini ndivyo imekuwa sivyo.

My Concern:
Kwanini Tunapoadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar John Okello haenziwi?
 
WanaJf salaam! Nakumbuka siku chache palikuwepo na mjadala mzito kuhusu nani aliyeleta mapinduzi Zanzibar na leo kiu yangu ya kujua mambo imetimia. Leo sa1 asubuhi TBC1 wameonesha vizuri kuwa mwanamapinduzi alikuwa mtu mwenye utata wa uraia John Okello akisaidiwa na Engen aliyekuwa Mkenya.

Kuna Mzanzibar aliyekuwa na umri wa miaka 14 Salim S.Salim ameleta waraka pale Tbc akieleza nani alileta uhuru wa zbar,kasema John Okello. Pia Fatma,mama Karume ameeleza kuwa wakati wamelala na Mzee karume alikuwa akisikia risasi nje na wao hawakuwa na taarifa yoyote ya mapinduzi na wala Karume hakujua mapinduzi yatakuwa lini,lakini mpango wa kupindua ulikuwepo pia naye Karume alikuwa anajua kuwa siku moja yatakuwepo.

Mama Karume kaeleza mengi sana yanayoonesha kuwa Karume hakuhusika,ila baada ya mapinduzi kuna watu walifika kwa karume wakiwa na gari ya kijani na nyingine ya manjano walikuwa wamefunga shoka juu ndo walipofika kwa karume na kupitia mlango wa nyuma waligonga mlango na mama karume alipofungua mlango aliona sura ambazo hakuzikariri wala hakuziona tena, walifika wakasema wanamtaka mzee na kisha waliondoka nae baada ya kukamilisha mapinduzi! Nadhani mama amemaliza utata uliokuwepo hapa Jamvini.

WanaJF sasa kwa nini hii historia ya kweli isifundishwe mashuleni na watu wanadanganywa? Kwa faida ya nani?

Mwisho: WanaJF kuna kitu kimenstua kwenye mapinduzi, kumbe ASP walikuwa na ishara kama ya Chadema, yani vidole viwili kama ishara ya chadema ya sasa. Hapa akili inasumbuka,ina maana chadema imechagua ishara ya mapinduzi kama ya Z'bar au? Ningetaka muelewa anieleshe,ni ombi langu tu! Nawatakia siku njema!
 
Nakuunga sana mkono na thread yako ya mchana niliisoma kiundani sana tu. kweli wana jf great thinkers sio siri na hapo jamvi letu limeleta hali ya leo hii taifa kuelezwa ukweli uliokwepwa kwa miaka mingi mno.
 
Mmimi nimesoma kile kitabu Cha JOHN OKELLO, hawa akina Karume hawana cha kujivunia pale inasikitisha sana tena sana jamaa walichomfanyia
 
HII NCHI KILA KILICHO CHA UKWELI INAJARIBU KUKIPINDISHA NA KUDANGANYA UMMA,SIJUI LINI SERIKAL ITAACHA KUWADANGANYA WANANCHI WAKE-CHEK LINK HII PIA-
John_Okello
 
John Okello anapaswa kuendelea kuitwa field marshal na mwanamapinduzi wa zanzibar waganda wanapaswa kudai fidia ya kuchangia umapinduzi ya zanzibar
 
Toka lini ukweli ukafunikwa chini ya kapeti ikawezekana? Tunaambiwa miaka mingi iliyopita, kuna msomi mmoja wa kigiriki aliwaambia watu dunia ni duara, kanisa likamlaani. Ila baadae ikaonekana kuwa walimuonea maana kweli dunia ni duara.
Na kuna mifano mingi ambayo inaonyesha jinsi ilivyo ngumu kuuchezea ukweli. Well, historia ya Tanganyika na Zanzibar imepindishwa kwa makusudi kabisa ili kunufaisha watu fulani.
 
Ni siri iliyowazi, John Okelo did everything na kumkabidhi AAK ila jamaa alionekana atakuwa maarufu kisha wakam marginalize Bara na Baadaye akaenda Kenya na kuishia home of origin Uganda.

Nako Uganda, inasemekana Idd Amina alimuona ni threat zaidi na inasemekana alipotea ktk mazingira ya ajabu na kuhofia kuuwawa na Idd Amin DADA. Kwani yeye alikuwa ni Field Marshal wa kweli wakati Idd Amin alikuwa ni wa kujipachika. Bado histaria ya Mapinduzi Zanzibar haiwezi kamilika bila yeye na ninadhani kama wote wangekuwa hai basi wangeheshimiana sana.

Lakini kitendo chake cha kumkabidhi AAK nadhani ni cha kawaida kwani asingeweza kuwa yeye kwa kuwa alikuwa ni raia wa Uganda na alichofanya ni kumkabidhi mzawa anayekubalika.
 
Back
Top Bottom