everybody
JF-Expert Member
- Oct 30, 2010
- 337
- 103
Huwa nawashangaa sana watu wanaowabeza walalahoi kama wamachinga, wapiga debe and vijana wa mtaani kujihusisha na kushabikia matukio (kama vile maandamano na mikutano ya hadhara) yanayolenga kufikisha ujumbe kwa ajili ya kuboresha maisha ya mtanzania. Siku zote hawa ndio watu wanaoguswa na hali duni ya maisha na siku zote ndio watakua wa kwanza kwenye matukio kama haya. Tunahitaji viongozi wachache tu kama wanavyofanya viongozi wa CHADEMA kwa sasa kuwaongoza jinsi watakavyoweza kutimiza azma yao ya kupata maisha bora.
Hivyo nawashangaa sana watu wanaokaa kubeza mikutano na maandamano ya wanamapinduzi Tanzania eti imejaa wavuta bangi, wezi na vijana wasio na la kufanya. Kwa hali halisi hawa ndio wenye kujua uchungu wa maisha magumu ya Tanzania na siku zote ndio watakua mstari wa mbele na ni halali yao kufanya hivyo. Wewe unashinda ofisini ukienjoy kiyoyozi huwezi kujua hali ngumu wanayokutana watu wa mitaani. Sana sana wewe hali ngumu utakayoiongelea ni kwamba umekosa hela ya kukaa kwenye kiti kirefu kunywa bia kumi na badala yake unakunywa mbili ili upate hela ya kumpeleka mtoto wako Academia school. Mwenzako mlala hoi anayeingia kwenye maandamano hana hata uhakika wa hiyo hela ya kupata sembe la mchana. Walala hoi wanaoingia mtaana kudai haki ya maisha bora kwa sababu wamekosa ajira na hawana jinsi ya kujipatia kipato kutimiza mahitaji yao ya msingi inabidi wapewe support badala ya kuwabeza. Watu kama hawa ndio wanaowasaidie nyie mnaokuwa kwenye maofisi yenu kufikisha ujumbe.
Nawasilisha..