Mapigo ya moyo kwenda haraka haraka, naomba ushauri

Dr tida

Member
Sep 9, 2011
6
0
Habari zenu wanaJF.

Mimi nina tatizo la mapigo ya moyo kwenda haraka haraka sana, kuchoka bila ya kufanya kazi na nikifanya mazoezi kidogo hali inakuwa mbaya, nahema sana.

Nimefanyiwa vipimo vya moyo ECG na ECO, Regency na KCMC nimeambiwa moyo hauna tatizo. Ugonjwa huu umeanza tangu 2003.

Naomba ushauri wenu.
 
Hata mimi leo na kama kichomi kifuani upande wa moyo, mfano nikicheka au kuvuta hewa kwa nguvu nackia panachoma, hili tatizo limenianza tangu asubuhi. Naomba msaada wenu pia wakuu.
 
jitahidi sana kunywa maji kwa wingi hasa yakuchemsha i mean natural water sio hayo tunayonunua pia jiepushe sana na vyakula vyenye mafuta hasa nyama nyekundu, na jitahidi kufanya mazoezi madogo madogo kuna rafiki yangu alikuwa na tatizo hilo siku hizi ananafuu kiaina
 
jitahidi sana kunywa maji kwa wingi hasa yakuchemsha i mean natural water sio hayo tunayonunua pia jiepushe sana na vyakula vyenye mafuta hasa nyama nyekundu, na jitahidi kufanya mazoezi madogo madogo kuna rafiki yangu alikuwa na tatizo hilo siku hizi ananafuu kiaina
<br />
<br />
Ahsante kwa ushaur wako nitaufanyia kazi.
 
Mkuu sikiliza natakiwa kutoa maelezo muafaka ili uwze kusaidiwa maana maelezo yako hayajitoshelezi kabisa
kwa ufupi kulingana na maelezo yako unaweza kupima ECG kama maumivu hayo yanachukua mda mrefu
Pili kama ni upande wa kushoto na inaambatana na bega la upande huo naweza sema ni tatizo la moyo
lakini kwa hapa siwezi kutoa maelezo sahihi kwa sababu taarifa yako sio timilifu ila angaia kipimo hicho kitakupa majibu yote.

pia Punguza vyakula vya mafuta kama chipsi n.k also kunywa maji ya kuchemshwa.
 
hizo ni dalili za matatizo ya moyo, mkewangu anatatizo linaitwa miltralvalve prolapse na anadalili hizo lakini sikuhizi hajambo kiasi flani.

nakushaur ukaonane na dk mlawa ni senior specialist wa magonjwa ya moyo anapatikana tumaini, muhimbili, aljumaa, nyengine nimesahau lakin ye alikua akionana nae pale aljumaa siku ya jumanne na ijumaa anakuwepo, clinic inaanza saa kumi na bei ni 35000 (imepanda sikuhizi zaman ilikua 20000).

atakushauri hadi sehem za kwenda kupima, baadhi ya hospital hawana wataalam wa kuchek vizur kipimo icho hasa ECHO. hutojuta yupo vizur ukifika muhimbili ukimuulizia pia utampata fasta wanamjua wengi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom