Mapigano yazuka kati ya wapiganaji Libya

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,107
Watu wanne wameuawa na
wengine watano kujeruhiwa
katika majibizano ya risasi
yaliyozuka mapema katikati
ya mji mkuu wa Libya,
Tripoli. Yalitokea katika jengo moja
la kijasusi lililopigwa na NATO
mwaka jana yalipozuka
mapinduzi ya kiraia dhdi ya
kiongozi Muammar Gaddafi. Brigedi moja kutoka mji wa
Misrata ilijaribu kuwaachilia
huru wafungwa, na
kuanzisha mzozo na kundi
lingine lililokuwa na silaha
kutoka Tripoli. Majeruhi walitoka pande zote
mbili. Milio ya risasi ilisikika karibu
na jengo hilo kati ya mitaa ya
Zawiya na Said. Barabara zilifunguliwa haraka
mara baada ya hali hiyo
kutulizwa. "Nasikitika kwa tukio hilo.
Sitaki kuingia kwa undani
zaidi, lakini ilikuwa ni
matokeo ya matatizo kati ya
wanamapinduzi wa Misrata
na wanachama wa baraza la kijeshi la mtaa wa Zawiya ,"
Abdul Hakim Belhaj, mkuu
wa baraza la kijeshi la Tripoli
aliuambia mkutano wa
waandishi wa habari. "Kilichotokea ni kitendo cha
kizembe na hali sasa
imedhibitiwa. Tangu mchana
hatujasikia tena milio yoyote
ya risasi," alisema. Ilikuwa ni dalili nyingine ya
tishio kwa usalama
linalosababishwa na
wapiganaji waliokata tamaa
wanaojaribu kuachana na
hadhi ya uasi, anasema mwandishi wa BBC Mark
Lowen akiwa Tripoli. Bado wana nguvu kutokana
na kutokuwepo kwa jeshi la
kitaifa au polisi. Lakini serikali mpya ya Libya
chini ya shinikizo, sasa
imeanza mchakato wa
kuyashunghulikia makundi
na kuyaunganisha na wizara
za ulinzi na mambo ya ndani, mwandishi wa BBC anasema. Makumi ya maelfu ya
wapiganaji bado yako
kwenye brigedi mbalimbali,
na kumezuka mfululizo wa
mapaigano kati yao katika
wiki za hivi karibuni. Mabadiliko kutoka vita vya
wenyewe kwa wenyewe
kuingia kwenye usalama na
Libya iliyotulia bado ni hatua
ya taratibu na ngumu na
tatizo la kushughulikia wapiganaji ni mojawapo ya
changamoto zilizo mbele.
 
Alisema mtoto wa gadaffi wakasema muongo.

Aisay watamjutia gadaffi.
 
Hali ya Libya ni tete sana..hili ni tukio moja tu lakini ukweli ni kwamba vita inapiganwa sehemu mbalimbali kule Libya..ila hawa manyangau hayawezi kusema maana ndio yalihusika na mambo haya..huyu Belhadji ni gaidi wa siku nyingi na US walishasema anataftwa ila sasa wamemtumia kumuua Ghadaff siku si nyingi watamgeuka tu...kwa ufupi nchi ile imeisha sasa..
 
heri shetani umjuaye kuliko malaika usiyemjua! walibya wanavuna walichopanda; hii nchi itaendelea kuwa chaotic kwa kipindi kirefu sana kijacho
 
Kila siku wana andamana Libya. Wa Tripoli hawawataki Wa Bengazi na Wa Bengazi hawawataki Wa Tripoli. Wana andamana Al Jazeera Square na sehemu nyingine nyingi tu. Kuna hatari wakagawana nchi. Na usijulikane kuwa wewe ni Gadhafi sympethiser, wataku uwa mpaka marafiki zako. Tukae tukijifunza kutoka matukio kama haya. Tusikubali kuchaguliwa mwelekeo wa nchi yetu na wazungu. Wao hawatujali. Wanajali rasilimali zetu tu.
 
Wazungu (us,uk &their alias) wanajua wanchotaka na wapo tayari kukichukua bila kujali nani anacho na kwa gharama yeyote. Wapo makini kutumia kinachoshika hisia za eneo husika ili kusababisha conflict na kuchukua wanachotaka.
 
Back
Top Bottom