Mapigano yaendelea DRC CONGO; Wakongo wanakimbilia Rwanda na Uganda

mwitaz

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
315
93
Taarifa kutoka Jamhuri ya
Demokrasi ya Congo
zinaeleza kuwa mapigano
yanaendelea mashariki
mwa nchi baina ya
wanajeshi wa serikali na wanajeshi walioasi. Msemaji wa waasi, Vianney
Kazarama, aliliambia
shirika la habari la
Ufaransa, kwamba jeshi la
serikali linashambulia
kituo chao kimoja kwa silaha nzito, huko Kivu-
Kaskazini. Mapigano hayo yalianza
kama siku 10 zilizopita. Umoja wa Mataifa unasema
maelfu ya watu
wamekimbia ghasia hizo,
wengi wao wameelekea
Uganda na Rwanda. Waasi hao wanasema wao
wamo kwenye vuguvugu
la March 23, ambalo asili
yake ni kundi la
wapiganaji wa Kitutsi, la
CNDP. Walikubali kujumuika na
jeshi la Congo, lakini sasa
wanadai kuwa wanataka
makubaliano ya amani ya
mwaka wa 2009
yatekelezwe kikamilifu.

Source: Wankuru Stephen Mwita
 
  • Thanks
Reactions: FJM
hawa waacheni tu wapigane ..vita i[o damuni sasa wanapigana pigana nini? bangi hizi
 
..Rwanda ndiyo inachochea mapigano ndani ya DRC.

..mpaka sasa hivi wamempa hifadhi Laurent Nkunda badala ya kumkabidhi kwa ICC.

..pia sielewi kwanini hao Watutsi walioko DRC hawarudi kwao Rwanda badala yake wanafanya vurugu DRC.
 
hawa waacheni tu wapigane ..vita i[o damuni sasa wanapigana pigana nini? bangi hizi

Kiongozi, mgogoro wa DRC is very complicated. Ukipata details zote has kuhusu Kivu utasikitika sana. It is very unlikely Kivu will see peace in our lifetime. Very unlikely! Kuna mkorogo wa mataifa mengi sana na tofauti na ilivyozoeleka kuona nchi za magharibi kama tatizo, DRC ina both nchi za magharibi na Africa.
 
Kagame is the one who spurs war in DRC. Under the pretext of Genocide, he has been sending his men in DRC to seek for indarahamwe. As the result, his soldiers are digging gold and diamond. If you remember well his soldiers fought in Kisangani DRC in 2000 against Uganda soldiers over a rich land dispute.
Now they want to occupy South kivu as their territory.

I think the incumbent president of DRC knows all these tricks as he is said to be originated from Rwanda.
 
Back
Top Bottom