Mapigano ya Wakristo na Waislam yazuka Arusha

mwankuga

JF-Expert Member
Aug 30, 2010
334
120
na Mwandishi wetu


amka2.gif

YAMEZUKA mapigano kati ya Waislam na Wakristo katika mji mdogo wa Mto wa Mbu wilayani Monduli, mkoani Arusha, na kusababisha wachungaji wawili kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Karatu kwa matibabu.
Hadi tunakwenda mitamboni gazeti hili lilikuwa na taarifa tofauti kuhusu chanzo cha vurugu hizo ambapo moja ilieleza kuwa chanzo cha vurugu hizo ni baadhi ya Waislamu kuwatuhumu wachungaji wawili waliotajwa kwa majina ya mchungaji Jakson na mwenzake Prospatus, kwamba wamekuwa wakiichambua vibaya Kurani tukufu hivyo kuidhalilisha dini ya Kiislam, hivyo wakaamua kuvamia mkutano wa Injili na kuwashambulia wachungaji hao pamoja na wasikilizaji wao.
Mbali na kuwajeruhi wachungaji hao, ilielezwa kuwa Waislam hao walivunja na kuliharibu kanisa la Anglikana la Mto wa Mbu.
Hata hivyo, taarifa nyingine kutoka Mto wa Mbu zilisema chanzo cha vurugu hizo ni mahubiri yaliyofanywa na mhubiri mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Utouh ambaye ilielezwa kuwa mahubiri yake aliyoyafanya kwa wiki nzima yalisababisha waumini wa Kiislam 20 wabadili dini na kuwa Wakiristo, hali ambayo ilidaiwa kuzusha chuki ya kidini katika eneo hilo.
“Walikwenda nyumbani kwa huyo mhubiri hawakumkuta, walivunja mlango wa nyumba yake na kutoa vitu vyote nje na kuvichoma moto.
“Walipotoka hapo walikwenda katika Mwalimu Anne Academy ambayo mwenye shule ni Mkiristo, hapo walivunja ofisi ya walimu ambao walikuwa madarasani na kuchukua simu za mikononi na kisha waliwapiga walimu na watoto,” zilieleza taarifa hizo kutoka kwa baadhi ya wananchi wa Mto wa Mbu waliodai kujua yaliyotokea.
Gazeti hili lilipowasiliana na kamanda wa polisi, OCD Maganga, alithibitisha kupata taarifa za tukio hilo na kwamba alikuwa njiani akielekea Mto wa Mbu kulifuatilia.

Source:Tanzania Daima 25/02/2011

Hii Wana JF imekaaje,mwenye habari kamili na hali ilivyo sasa atujuze.Lakini issue kama hizi sio nzuri kwani athari zake ni mbaya.Wakati huu tunatakiwa kuwa kitu kimoja ili tuweze kuung'oa utawala wa CCM uliodumu madarakani zaidi ya miaka 30,huku umasikini miongoni mwa Watanzania ukizidi kuongezeka


amka2.gif



amka2.gif
 
Hii habari tangu jana nilivoisoma kwa mara ya kwanza, haikuniingia akilini na mpaka sasa haitaki kuniingia. It is a cooked story yenye lengo fulani. Watu wamechoka na amani wanataka kujaribu vurugu na vita.
 
Back
Top Bottom