Mapigano ya kugombea ardhi yaua Tegeta

Huwezi amini hadi karne hii kuna polisi wanapata sana shida kuandika sentensi moja nzuri. Form 4 failures. Ndio maana kila kitu ni nguvu na hila bila akili.
 
Ndugu zangu. Naomba Mungu atuepushe na kikombe hiki cha kuuana sisi kwa sisi kwa ajli yoyote ile iwe kudai haki, kujilinda ama kujitetea. Serikali itambue kuwa damu ya Mtanzania yeyote inathamani na haitakiwi kumwagika kwa sababu yoyote ile. Ni wajibu wa serikali kuwalinda wa Tanzania bila kujali matabaka ya utajiri, elimu, dini, kabila, umri, jinsia, madaraka ama itikadi. Serikali ichukue hatua kwa askari waliogoma kwenda kudhibiti ghasia hadi wa Tz wenzetu wakatoana roho.

SASA SERIKALI IONE HAYA KWA MFUMO WAKE WA KUHAHA KUTAFUTA SOLUTIONS BAADA YA MATATIZO KUTOKEA HUKU IKITOA CHEAP EXCUSES ZA KUWAHADAA WANANCHI. SERA MBOVU, UTAWALA MBAYA, KUKOSA UWAJIBIKAJI, RUSHWA, UBADHILIFU, UTEKELEZAJI MBAYA WA MIPANGO MIBOVU NA UKIUKWAJI WA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU SASA ZINATUPELEKA TUNAKOTOKOMEA.

Watanzania wote tukatae kuuana kwa sababu yoyote ile. Badala yake, tuiwajibishe Serikali isiyothamini damu zetu na inayojenga mazingira yetu kupoteza uhai kwa sababu zinazozuilika.

Mwisho naomba kwa mwenye taarifa kamili atubainishie nini mgogoro uliopelekea ugomvi huo. Maana ni dhahiri kuna pande zimekinzana upande mmoja ukatuma ma baunsa na madalali na upande mwingine ukaona hatua hii ya madalali si sahihi.

Naomba ufafanuzi ili tuweze kuchambua na kujadili.
 
ARNACHISTs wanakuambia wazi kabisa kuwa "HAKI HAIOMBWI ILA INAPIGANIWA............"

Haki kwa Tanzania kwa sasa INANUNULIWA. Wenye PESA wameiteka.

Kama Tanzania inataka HAKI (Dalili zimeanza kuonyesha kuwa INAANZA KUDAI HAKI), basi huu ni mwanzo.

Kama mambo hayatabadilika na hasa KATIBA MPYA, basi kuna MAUWAJI mengi sana yanakuja.

Damu itamwagika na tutamwaga woote yaani Wageni wawekezaji/Wezi, Mafisadi, Viongozi na Watanzania wa kawaida.

Mambo mengine lazima yatokee ili miungu watu wageuke na kuwa binadamu.

Tangu enzi za Adamu, DAMU imetumika kusafisha dhambi. Msitegemee Tanzania itakuwa tofauti.
 
kwa wale wakristo wanafahamu kuwa laana ya kiongozi inaweza kukupata mwananchi wa kawaida....hii ni laana,mbona mambo haya hayajawahi tokea huko nyuma? Katika tukio hili watu wafuatao hawawezi kukwepa lawama

  1. Watu wa ardhi
  2. Viongozi wa halmashauri
  3. Viongozi wa Kijiji,mtaa,kata nk
Utashangaa baada ya tukio hilo,hakuna ata kiongozi atakayeonyesha kuumia wala kusikitika..na kama wakisikitika watakuwa ni wanafiki wasio na aya...
kama mimi ndiye ningekuwa JK (Rais)kwanza ningemtia adabu huyo bosi aliyewapa kazi hao jamaa wa kampuni ya mnada kwa kumfunga jela miaka 100 na kumnyang'anya viwanja vyote alivyonavyo. Pili ningewatia adabu hao jamaa wa kampuni ya mwangata...sijui mwangaza kwa kosa la kuwaajiri mabaunsa ili kwenda kuwaonea wananchi kwa maslahi ya fisadi mmoja tu....hiyo kampuni ningeifunga milele na wahusika wote wangeenda kunyea debe miaka 100 bila msamaha. Lakini ninavyomjua kikwete....hapo atabaki kuchekacheka tu na akuna action yoyote
 
ARNACHISTs wanakuambia wazi kabisa kuwa "HAKI HAIOMBWI ILA INAPIGANIWA............"

Haki kwa Tanzania kwa sasa INANUNULIWA. Wenye PESA wameiteka.

Kama Tanzania inataka HAKI (Dalili zimeanza kuonyesha kuwa INAANZA KUDAI HAKI), basi huu ni mwanzo.

Kama mambo hayatabadilika na hasa KATIBA MPYA, basi kuna MAUWAJI mengi sana yanakuja.

Damu itamwagika na tutamwaga woote yaani Wageni wawekezaji/Wezi, Mafisadi, Viongozi na Watanzania wa kawaida.

Mambo mengine lazima yatokee ili miungu watu wageuke na kuwa binadamu.

Tangu enzi za Adamu, DAMU imetumika kusafisha dhambi. Msitegemee Tanzania itakuwa tofauti.

No more bloodshed for Tanzanians. I declare peace, justice and good life for all Tanzanians. I am reversing your confession in the Mighty Name of Jesus Christ. Amen
 
kama mimi ndiye ningekuwa JK (Rais)kwanza ningemtia adabu huyo bosi aliyewapa kazi hao jamaa wa kampuni ya mnada kwa kumfunga jela miaka 100 na kumnyang'anya viwanja vyote alivyonavyo. Pili ningewatia adabu hao jamaa wa kampuni ya mwangata...sijui mwangaza kwa kosa la kuwaajiri mabaunsa ili kwenda kuwaonea wananchi kwa maslahi ya fisadi mmoja tu....hiyo kampuni ningeifunga milele na wahusika wote wangeenda kunyea debe miaka 100 bila msamaha. Lakini ninavyomjua kikwete....hapo atabaki kuchekacheka tu na akuna action yoyote

Ninalaani vikali mauaji hayo, na ninawapa pole wafiwa na wale wote walioumia tokana na vurugu hizo. Ila hakuna sababu ya msingi ya kumtupia lawama Jakaya Kikwete. Ugomvi wa ardhi umekuwepo toka enzi na enzi ndani ya Tanzania. Kumbukeni kule Mara - Musoma, wakurya wamekuwa wakichinjana kwa ajili ya ardhi toka enzi za Nyerere. Kule Kilombero nako watu walipigana vikali na wengi kupoteza maisha enzi za Nyerere. Mbona Nyerere hakulaumiwa kwa mapigano yale?.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya sa mbili itv hali inatisha wananchi wamewashambulia mabaunsa utafikiri hawana akili nzuri halafu polisi wanapewa taarifa wanasema acha wauane huyo atakayebaki wa mwisho atawapelekea taarifa. This is outrageous!! Huyo tajiri aliyewatuma watu hao anapaswa kufikishwa mbele ya vyombo vya dola mara moja, fisadi mkubwa..
 
No more bloodshed for Tanzanians. I declare peace, justice and good life for all Tanzanians. I am reversing your confession in the Mighty Name of Jesus Christ. Amen
Imani bila matendo imekufa.

Yakobo 1: 14 - 17

14 Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa? *
15 Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. *
16 Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
17 Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

Wape watu haki yao, hii mijadala na habari kama hizi hutasikia...
 
Mpiga picha na mtangazaji wana roho za ngumu ... yaani wanapiga picha wanahoji badala ya kutoa huduma ya kwanza! Ndivyo mnavyofundishwa huko vyuoni kwenu?
 
Ninalaani vikali mauaji hayo, na ninawapa pole wafiwa na wale wote walioumia tokana na vurugu hizo. Ila hakuna sababu ya msingi ya kumtupia lawama Jakaya Kikwete. Ugomvi wa ardhi umekuwepo toka enzi na enzi ndani ya Tanzania. Kumbukeni kule Mara - Musoma, wakurya wamekuwa wakichinjana kwa ajili ya ardhi toka enzi za Nyerere. Kule Kilombero nako watu walipigana vikali na wengi kupoteza maisha enzi za Nyerere. Mbona Nyerere hakulaumiwa kwa mapigano yale?.
Kidatu,
Sahihisho kidogo. Nyerere alikomesha mauaji ya Tarime wakati wa utawala wake. Mauaji na mapigano yameanza tena miaka kumi na sita baada ya Nyerere kutoka mamlakani. Tujiulize Nyerere alitumia miujiza gani kusimamisha mauaji ya kikabila Tarime? Na mauaji ya Kilombero yametokea wakati wa Mkapa. Nyerere hakuwahi kustahmili mauaji ya kijamii hata kidogo!
 
Imani bila matendo imekufa.

Yakobo 1: 14 - 17

14 Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa? *
15 Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. *
16 Yafaa kitu gani ninyi kuwaambia hao: "Nendeni salama mkaote moto na kushiba," bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha?
17 Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

Wape watu haki yao, hii mijadala na habari kama hizi hutasikia...

Sote tunapigania haki iliyohodhiwa na watu wachache lakini haina maana lazima tumwage damu. Bloodshed ni roho nyingine na si lazima ilete haki. Si lazima haki ipatikane kwa kumwaga damu. Kuchukua hatua katika kudai haki haina maana sawa na kumwaga damu.

Tafadhali sana naomba tuzidi upeana mbinu nyingi nyingi tu za kudai haki zetu lakini hii ya kumwaga damu. hapana mtu wangu.
 
Nimesikitishwa sana na vifo vya hao waliouwawa kikatili,,,,,,,, i think its about time serikali ione hii nguvu ya uma uliochoka na kuanza kuwapa uma haki yao,
......wananchi tumechoka tena tumechoka sana,,,,,,

Nilisikia watu wakizungumza kariakoo hivi....... ipo siku tutakuja kuwauwa kwa mikono yetu hao wanaongoza nchi wanavyotaka kina rostam azizi, manji na lowasa ili tupate haki zetu..........

Serikali ni heri ikaliona hili la Tegeta katika macho tofauti!
Watu waliochoka(na chochote kile) wanahitaji only a slight spark ya kuwa fanya kuwa uncontrollable.
Amani, umoja na mshikamano tunaouongelea bila haki za kimsingi kwa mwananchi wa kawaida ni kujidanganya.
Kama yametokea Tegeta tukae chonjo!!!
Its a sign of things to come.
 
Ukweli ni kwamba hatuna serikali. Tuna genge la mafisadi tu wanao masquarade kama watawala.
 
duh iyo ni kali,bt yasemekana police waliitwa ,hawakufika ktk mda ule ,na majibu waliokua wanatoa hayaridhishi so w2 wakajichukulia hatua mkonon,

Mtawalaumu polisi wa watu bure, kama ilivyo kwa walalahoi wa TZ polisi nao wanamahangailko mengi kwenye maisha yao huku wakishuhudia mafisadi na viongozi vibaraka wa mafisadi wakifaidi nchi. Tusisahau ya Misri ambapo wanajeshi waliamua kuwaacha wamisri wafanye Vifaru vya jeshi kuwa viti vya kupumzikia wakidai mabadiliko, Na TZ tunaelekea huko huko tartibu ila kwa uhakika
 
Hivi hamna habari kwamba serikali ya JK iko likizo tangu zamani tu.
 
Hebu usimhusishe Yesu katika hili.

Huhitaji kujiita MNAJIRI kujua hili litakuja Tabby. It was just a matter of time.

Kitendo cha Tanzania kukosa UONGOZI, kumetengeneza VACUUM na kwa sababu Vacuum huwa haitaki kubaki wazi, lazima kitu kingine kije kuziba. Matokeo yake ni watu kujichukulia madaraka mikononi.

Sasa kwa nini UKEMEE hali hii na usikemee CCM na uozo wake kwa kutufikisha hapa?

Waliomba KUSHIKA HATAMU, wameshinda ila sasa tunaona kuwa kumbe na wao WAMESHIKWA hatamu na Mafisadi.

Usiwe na wasiwasi, siku watatengeneza Kimzoga KIFISADI, mambo yatabadilika.
No more bloodshed for Tanzanians. I declare peace, justice and good life for all Tanzanians. I am reversing your confession in the Mighty Name of Jesus Christ. Amen
 
Back
Top Bottom