Serikali ya Kikwete. Nyumba 26 za waathirika wa mabomu zinajengwa kwa gharama ya sh.96, 000, 000 zote pamoja.
Mkuu binafsi sijakuelewa, hiyo miloni 96 kwa nyumba 26 umeiona ni kubwa au ni ndogo? naomba uniweke wazi ili tuelimishane kitu
Tanzania hakuna amani, wanaodai kuna amani ni waongo wakubwa, hakuna amani bila haki, na tz hakuna haki, ni swala la muda tuu machafuko yatarindima kila kona. Watawala wetu wakiendelea na ubabe wao pamoja na kuziba masikio yao kuusu katiba huru mpya hapatatawalika.Nimekuwa nikipinga huu msemo kuwa Tanzania kuna amani. Nimerudia tena na tena kuwa amani sio kutokuwa na vita, bali ili pawe na amani utawala wa haki kwa kila binadamu utumike. Amani iko wapi kama mahakama, polisi, na huduma zingine hazifanyi kazi vizuri? Watu wanakufa kila siku kwa majanga mbalimbali, kukitokea watu ambao wanataka kuleta mabadiliko mazuri wanaambiwa wanavunja 'amani'.