Mapigano Wakulima na Wafugaji yaibuka tena Mvomero-Morogororo

Huyo waziri hamna la maana atakaloenda kufanya zaidi ya kuuza sura tu.

Hiyo mifigo inatia huzuni sana!!
 
Ni ukatili na unyama wa hali ya huu kuua mifigo kwa namna Hiyo. Wanyama hao ni hayawani hawana akili yoyote ya kutafakari. Serikali inabidi ikomeshe maji ya kikatiri namna hii dhidi ya wanyama, Japo pia siungi mkono kitendo cha baadhi ya wafugaji kulisha kwa makusudi kwenye mashamba ya wakulima.
 
Kuna watu siku ya mwisho sijui mashitaka yao yatakuaje ,kuna wanao fanya mapenzi na mifugo kama nguruwe ,mbuzi na wenzake ,kuna wanao wakatakata kama hivi kwa hasira ......yaani kitengo cha kutoa hukumu Mungu angegawanya kwa viumbe halafu Punda ndio awe msimamizi wa hukumu kama hizi ,sijui naandika nini ila nahisi nime eleweka
 
waziri Mwigulu upoooooooooooooo mbona hatupatiwi majibu kamata wauwa mifugo tia ndani
 
Kita mtu arudi kwao kwa kweli,wasukuma kwenu, Wamasai kwenu

Fatilia vizuri kila linapotokea jambo hili wafugaji wakimasai ndo wenye shida hawa wasukuma wanalima pia so wanajua umuhimu wa kilimo tofauti na wamasai.
 
Lakini hawa mbuzi si huwa wanachinjwa pia shingoni kwa kisu? Au hapo si kuwaonea?
Wafugaji lazima wawe walinzi wa mifugo yao, wakila mazao ya watu na wao waisome namba.
kuchinjwa sawa lakini si kuwakata miguuu na maeneo mengine ya mwili huku wakiachiwa maumivu makali jamani nimeumia sana.. akichinjwa anakufa .. ndiyo maana ahata binadamu akifa tunasema kapumzika loh... si kuwaachia hawa viumbe hayo maumivu makaili hivyo
 
Huko Gairo si kuna mtu ana jeshi lake kabisa na polis wanamuogopa balaa..ngoja niulizie jina la kijiji
 
Kama kawaida ya maigizo yanayoendelea sasa hivi tz hii ni 'opportunity' kwa Mwigulu kuuza sura. Of course atafika na waandishi wa habari na atasemasema tu ili aonekana anachapa kazi, ...
 
Nimesoma na kutafakari. Nimebaini hakuna mapigano hapo. Bali wananchi walikuwa na hasira ya mifugo kula nusu ekari ya mazao. Hebu fikiria mifugo inakula mazao kiasi hicho na wafugaji wanaangalia tu. hao si wauaji? Ila nawapongeza wakulima kwani wangemuua binadamu ingekuwa habari nyingine
unawapongeza kwa lipi? yaani huna hata huruma kwa hao viumbe wasio na hatia?
 
Zaid ya mbuzi na kondoo 200 huko Dihinda mvomero mkoani Morogoro wamekatwa katwa na walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la MWANU.
Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walizinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai.
Lakini inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo mjane haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.
Waziri mwenye dhamana mupitia wizara ya mifugo na kilimo hivi sasa ameelekea eneo la tukio.
 

Attachments

  • 1455022217894.jpg
    1455022217894.jpg
    102 KB · Views: 38
  • 1455022273481.jpg
    1455022273481.jpg
    122.5 KB · Views: 40
Nimesoma na kutafakari. Nimebaini hakuna mapigano hapo. Bali wananchi walikuwa na hasira ya mifugo kula nusu ekari ya mazao. Hebu fikiria mifugo inakula mazao kiasi hicho na wafugaji wanaangalia tu. hao si wauaji? Ila nawapongeza wakulima kwani wangemuua binadamu ingekuwa habari nyingine

Mifugo wamekula nusu hekari tu, ambayo thamani yake sidhani kama inafika nusu million

Wao, wameua mbuzi na kondoo 200, ambao, kwa bei ya 50,000 mmoja, inafika takribani 10,000,000,

Na pili, mnyama hana akili, kwa nn ahukumiwe, tena kifo cha kikatili hivyo

Kwa nn wasikamate hiyo mifugo na kubinafsisha, kulingana thamani ya hasara waliyopata.

Hii ni chuki kubwa, tena ya kijinga kabisa, imeachwa imekuwa na kukomaa, imeota mizizi sasa
 
Mifugo wamekula nusu hekari tu, ambayo thamani yake sidhani kama inafika nusu million

Wao, wameuwa mbuzi na kondoo 200, ambayo, kwa bei ya 50,000 mmoja, inafika takribani 10,000,000,

Na pili, mnyama hana akili, kwa nn ahukumiwe, tena kifo cha kikatili hivyo

Kwa nn wasikamate hiyo mifugo na kubinafsisha, kulingana na thamani ya hasara waliyopata.

Hii ni chuki kubwa, tena ya kijinga kabisa, imeachwa imekuwa na kukomaa, imeota mizizi
 
nilikuwa na shama maeneo hayo Masai kaingiza ng"ombe wake shambàni kwetu namuuliza ananiambia ikale wapi lakini Wa fugaji ni wamasai peke yao mbona wama ng"ati hawana ugomvi wapo pia wasukuma kule Kilombero mbona hakuna mapigano hawa wamasai Wa Dogo ,kiteto, Mvomero, sunya leiseri mbona wagomvi sana
Unachosema si kweli!fuatilia Mara ya mwisho tukio la kukatwakatwa mifugo huko huko lilikuwa baina ya makabila yapi kama si ya wamang'ati
 
Hii sio sawa kabisa ni kukosa u binadam hivi mifugo inakosa gani
Ni kitendo cha kinyama sana, ila nao wafugaji kwa nini wanapeleka mifugo yao ktk mashamba ya wakulima?
Chanzo kikubwa ni wafugaji maana mashamba hayahami kufuata mifugo bali ni mifugo inafuata mashamba.
Wafugaji ndo chanzo cha huu unyama, na sasa naona wafigaji wakienda kuua wakulima, vita!
 
Nimesoma na kutafakari. Nimebaini hakuna mapigano hapo. Bali wananchi walikuwa na hasira ya mifugo kula nusu ekari ya mazao. Hebu fikiria mifugo inakula mazao kiasi hicho na wafugaji wanaangalia tu. hao si wauaji? Ila nawapongeza wakulima kwani wangemuua binadamu ingekuwa habari nyingine
Acha ujinga wewe,sasa hao wanyama waliokatwakatwa wana makosa gani?halafu umeambiwa wanyama waliokatwakatwa sio wale walioingia shambani,ni wa mjane mwingine kabisa.Kwenye makosa ni hiki kikundi cha kigaidi kinachoandaliwa na watawala.
Lakini pia wakulima wa maeneo hayo watakuwa na matatizo maana haiwezekani kila siku wao tu.Mbona tunaishi na wafugaji maeneo mengine ya nchi bila uhasama?
 
Back
Top Bottom