Mapigano makali Libya-Mji wa Sabha

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
[h=1]Mapigano makali Sabha, Libya[/h]
27 Machi, 2012 - Saa 16:29 GMT



Mapigano kati ya makundi hasimu ya wapiganaji nchini Libya yamesababisha vifo vya watu 30. Mapigano hayo yalifanyika eneo la Sabha kati ya wapiganaji wa kabila la Toubou baada ya mpiganaji mmoja kuawa katika mzozo wa umiliki wa magari.

Majeshi ya serikali yamefika eneo hilo kutuliza hali. Utawa wa mpito wa Libya unakumbwa na wakati mgumu kudhibiti nchi hiyo baada ya kumuondoa Kanali Muammar Gaddafi mwaka jana.
Ahmed al Hamrouni ambaye zamani alikuwa kamanda wa waasi amesema milio ya roketi imesikika katika barabara kuu huku moshi ukionekana kupaa juu ya uwanja wa ndege wa Sabha.
Serikali ya mpito imewashawishi wapiganaji waliosaidia kumng'oa madarakani kanali Gaddafi kusalimisha silaha na kujiunga na jeshi la taifa.
Mwakilishi wa utawala wa mpito amesema makabiliano yalianza pale wapiganaji wa kabila la Toubou walipojaribu kuiba magari ya wapiganaji wa kundi la Sabha.

110922234111_sabha_fighting_304x171_afp.jpg


Msemaji huyo amesema kamati ya maridhiano imeundwa ili kumaliza mapigano.






Source:bbc
 
Marekani wameshafanikiwa kuwachonganisha Walibya wapigane, huku wao wakichota mafuta. Adui wao aliyesema mafuta ya Libya ni kwa ajili ya walibya keshauawa kinyama, Libya imetumbukia pabaya.
 
Wapi mmmeona kusimamisha na kutekeleza demokrasia kwa njia ya mtutu?
Serikalii ya mpito ya Libya ilishinda vita lakini itachukua miaka mingi kushinda mapambano.
 
Ni kweli kabisa kwa sababu wao walitoa silaha na wakamdhibiti Gaddafi asiweze kujitetea mwishowe mambo ni kama yalivyo na kuna waafrika wenzetu pamoja na viongozi wetu walisherehekea hadi kutaifisha mali za serikali ya libya.
Hivi sasa for strategic reasons wanafanya hivyo hivyo nchini siria na hakuna apigae japo kelele.
Hivi katika yale machafuko ya london miezi michache iliyopita kama wale vijana wangepewa silaha na wapinzani wa dola ya kiingereza . Jee serikali ingetumia njia gani kutuliza maasi hayo??? hivi ushauri wanaoutoa kwa siria wao wangekubali????
 
Sabha ilikuwa ni eneo pekee ambalo haliku dhurika na mabom ya NATO. Pia ni eneo ambalo lipo kusini mwa Libya na karibu na mpaka na Niger. Wengi hapo ni wasomi na wengi wamejifunza kiswahili kwa kujitayarisha kwa matumizi ya lugha hiyo na AU. Kama Libya itagawanyika basi jimbo hilo litajitenga. Hawapendi msimamo wa NPC na pia sio watu wa Gadhafi. Kwani huwa wanajiita waafrica wa kweli.

Nawombea kila la kheri huko Sebha. Amani itapatikana. Bakini na msimamo wenu na sisi waafrica wenzenu tunakuja kuwa unga mkono.
 
Back
Top Bottom