Mapenzi yawaweka pabaya wanafunzi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WANAFUNZI watano wa shule ya Sekondari Mbagala ya jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwafanyia fujo wanafunzi wenzao wa shule ya Sekondari Nzasa kwa sababu za kimapenzi.
Mwishoni mwa juma lililopita wanafunzi hao waliwavamia wanafunzi wenzao wakiwa na silaha za ugomvi yakiwemo mawe, misumari kwa madai na kuchukuliwa mpenzi wao kwa madai kuna mwanafunzi wa kiume wa shule hiyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wa kike ambae alikuwa na mpenzi wake katika shule hiyo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema kuwa chanzo cha vurugu hizo zilisababishwa na mwanafunzi mmoja wa shule ya Mbagala alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mmoja wa shule hiyo na baadae mwanafunzi huyo alibaini kuwa mpenzi wake huyo ana mahusiano na mwanafunzi mwingine anayesoma Nzasa.

Kamanda Misime amesema kuwa, kutokana na ugunduzi huo mwanafunzi huyo aliamua kwenda na kundi lake shuleni hapo kwenda kumfanyia vurugu mwanafunzi huyo.

Waliokamatwa kwa kusababisha vurugu hizo ni Said Muhibu wa kidato cha tatu, Reuben Hosea wa kidato cha tatu, Shana Reagan wa kidato cha nne wa shule ya Mbagala na Twahir Sultan wa shule ya Nzasa

Hivyo kamanda huyo alivifafanulia vyombo vya habari kuwa upelelezi utakapokamilika wanafunzi hao watafikishwa Mahakamani.
 
Na hao nao wakifeli mwaka huu wazazi kama kawaida wataelekeza lawama kwa walimu na serikali.Psychologically mawazo yao yote yapo kwenye mapenzi
 
Hao wote wanastahili adhabu kali, ambayo itawafanya wawe mfano kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Wazazi wanaangaika kusomesha watoto wao kwa tabu alafu wanaenda kuendekeza ngono!!!!

Ni hatari kwa maendeleo ya Elimu Tanzania.
 
Hakuna cha shule ya kata wala nini! We unapelekwa shule af unaenda kufiligiswa nyang'au "kabaisa" unategemea kuwalaumu waalimu na serekali alaaaa
 
Kamanda anataka kupeleka kesi mahakamani ili iwe nini, hapo wazazi wakae wawaozeshe tu vijana wao kazi iishe, shule imewashinda, mahakamani ni kuongezea mahakimu mzigo tu
 
WANAFUNZI watano wa shule ya Sekondari Mbagala ya jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kuwafanyia fujo wanafunzi wenzao wa shule ya Sekondari Nzasa kwa sababu za kimapenzi.
Mwishoni mwa juma lililopita wanafunzi hao waliwavamia wanafunzi wenzao wakiwa na silaha za ugomvi yakiwemo mawe, misumari kwa madai na kuchukuliwa mpenzi wao kwa madai kuna mwanafunzi wa kiume wa shule hiyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi wa kike ambae alikuwa na mpenzi wake katika shule hiyo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema kuwa chanzo cha vurugu hizo zilisababishwa na mwanafunzi mmoja wa shule ya Mbagala alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mmoja wa shule hiyo na baadae mwanafunzi huyo alibaini kuwa mpenzi wake huyo ana mahusiano na mwanafunzi mwingine anayesoma Nzasa.

Kamanda Misime amesema kuwa, kutokana na ugunduzi huo mwanafunzi huyo aliamua kwenda na kundi lake shuleni hapo kwenda kumfanyia vurugu mwanafunzi huyo.

Waliokamatwa kwa kusababisha vurugu hizo ni Said Muhibu wa kidato cha tatu, Reuben Hosea wa kidato cha tatu, Shana Reagan wa kidato cha nne wa shule ya Mbagala na Twahir Sultan wa shule ya Nzasa

Hivyo kamanda huyo alivifafanulia vyombo vya habari kuwa upelelezi utakapokamilika wanafunzi hao watafikishwa Mahakamani.

hivi enzi hizo nineteen kweusi, wanafunzi walipokuwa na uhusiiano.. marafikai walikuwa wanjua kweli... sidhani, ingawa mambo hayo yalikuwa si mengi... laki kwa vija wa siku hizi... du...kaaaaazi kwel kwel
 
Kuna kitu kilikuwa kinaitwa "Suspension" na siku ukirudi unakuja na mzazi wako, hapo utakula viboko mbele ya mzazi na wanafunzi wote kama fundisho kwa wanafunzi wengine. Hivi bado kipo?
 
Cha ajabu hata waalimu wengine nao wamewageuza wanafunzi kuwa wake zao. Jamani wanafunzi wameshindikana!
 
mi sijui nini kinaendelea nchi hii, juzo kati hapo kule tegta the same issue ilizuka, kuna wanafunzi wa shule moja kule inaitwa kondo na nyengine inaitwa pwani, zote ni shule za msingi. walikua wanagombana kisa kuibiana wapenzi. ulikua ni ugomvi mkubwa mpaka polisi wakaja kupunguza makali.
 
dah!:doh: kitabu na mapenzi mbona haviendani...wasome kwanza mapenzi baadae. ngoja wajutie kuchanganya mapenzi na masomo, kwan alikuwa ni mke huyo aseme alimtolea mahari. utoto unawasumbua wakikuwa wataacha
 
Kwa mtaji huu wa mapenzi na shule. Wazazi wanao kataa kusomesha watoto zao,wako sawa kabisaa
 
Tusubiri matokeo yao ya mwisho yakitoka WALIMU watabebeshwa lawama zifuatazo
1. Walimu hawajui Hisabati na Kiingereza
2. WALIMU hawajui kufundisha wanahitaji semina elekezi
3.WALIMU wamepitwa na wakati na wanatafuna tu pesa za michango
nb:
nyie watoto mapenzi yapo hayaishi so someni shairi la MSIHARAKIE MAMBO
 
ndo wanafunzi wa bongo fleva hao , wanashindwa kufikiri kwenye
jambo dogo hivyo je masomo wataweza kweli?
 
Back
Top Bottom