TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,463
- 11,166
Wanajamii kwa mtazamo wangu nimeona kuwa mapenzi kwa sasa yanachanganya sana kiasi kwamba mtu ukifikiria sana unaweza kuibuka na uamuzi kuwa ni bora usijiingize kabisa kwenye huo ulimwengu wa kimapenzi. Utamkuta mwanadada ana mtu ambaye anampenda sana (siku hizi inasemwa anam-feel) huyo ndiye anakuwa dream husband wake wakati huo huo pembeni kuna kibosile anayemtatulia matatizo yake ya kiuchumi, pembeni tena kuna mwingine ambaye anamfikisha vyema kwenye tendo (kwa mujibu wao) wengine wanadiriki humu jamvini kusema kuwa wanapenda kujiexpress lakini si na waume zao (wapo wanaosaidia) n.k n.k n.k
Tukija kwa upande wa wanaume, utakuta kuna mwanadada ambaye anakuwa anam-feel kiasi cha kumchukulia kama wife wake (kama hawajaoana). Wakati huo huo kuna mwingine kwa ajili ya kumpatia huduma ya mtandao (Wasiliana na Chrispin au Fidel kama hujui hii ni nini) wakati huo huo naye anataka aukemee uzee (kwa mujibu wa Annina), miongoni mwa tetezi wanazotumia mabinti wanaoamua kujiingiza kwenye usagaji ni pamoja na wanaume kutokujali hisia zao, kutokuwa waaminifu, kutowaridhisha vyema kwenye tendo (kwa mujibu wa maelezo niliyopata kwa baadhi yao) n.k n.k n.k ..
Kwa hali hii, wanajamii wenzangu, tunaelekea wapi hasa? Na ni upi mtazamo wako kama mwanajamii mwenzangu, nini hasa kifanyike ili kunusuru kizazi kijacho?
Jiulize...............................................