Mapenzi yanaumiza sana

shoshte

Senior Member
Apr 9, 2011
129
20
Nawasaimu wote wana Jf
Unakuta umekutana na msichana unampenda unamtokea anakukubali na mnakuwa marafiki ila mzazi wake (mama)
anafahamu baada ya muda yule binti from no where anakwambia hakufeel tena bila sababu yoyote wee unaumia
ila unapiga mwoyo konde unasonga mbele.Kipindi hicho ulikuwa unasoma chuo na binti pia. anamaiza chuo anakutana
na jamaa mmoja basi wanachukuana wanakaa kama mume na mke kwani wanaishi nyumba moja.Mungu naye anakubariki
unapata kazi nzuri maisha yanasonga.Baada ya muda wale watu wanapata matatizo,wewe katika fani yako unaweza kutoa
msaada unatoa msaada bila hata kujali ya zamani.Baada ya muda yule jamaa anamwacha yule binti.SASA HAPA NDO PATAMU
BINTI BAADA YA KUACHWA ANAKUJA KWAKO KUOMBA MSAMAHA NAKUTAKA MRUDIANE ANAMTUMIA MAMAKE SASA KUKUCONVINCE
MRUDIANE.WEWE HAPO UNAKUWA UMESHAMPATA MWINGINE NA UMENUIA KUISHI NAYE.Kwa busara nzuri unaweleza kwamba una mtu
mwingine tayari na maisha yanakwenda.ila wao wanaanza kumponda yule uliye naye kuwa hakufai ukiuliza sababu za kutokukufaa hawasemi
je ingekuwa niwewe ungejisikiaje na ungefanya nini???????
 
Hapo ni kuwaambia ukweli mwanzo hadi mwisho. Ikiwa ni pamoja na kuwaeleza wazi wazi, "Nikimuacha huyo niliye naye nitakuwa sijamtendea haki na nafsi yangu inasema sitakuwa na amani tena". Kwangu mimi sitotegemea kubadili msimamo, labda kama uhusiano ulio nao uko katika mashaka nikiwa na maana ya kuwa hauko level fulani ambayo unaweza kukosa amani lakini bado siyo sababu ya kurudiana na huyo Ex - G kwa jinsi alivyofanya.
 
Jibu mbona unalo?? kama hakukuona una thamani yoyote kipindi kile itakuwa sasa hivi?
 
Nime waeleza mkuu na sirudi nyuma niliye naye tunapendana na hamna shida kilicho niboa nikuwa yeye ameenda huko kutanga tanga leo hii anaona nafaa???
 
Jibu mbona unalo?? kama hakukuona una thamani yoyote kipindi kile itakuwa sasa hivi?
Ni kweli jibu lipo ila inaumiza sana kuwa wakati unampenda mtu anakuona mambo fulani ila akishatendwa huko ndo anakukumbuka
 
huyo ni materialist!!!
akiingia ndani ya nyumba atakuumiza.
kimbia fasta na usigeuke nyuma
 
Ni kweli jibu lipo ila inaumiza sana kuwa wakati unampenda mtu anakuona mambo fulani ila akishatendwa huko ndo anakukumbuka
Achana nae hakufai yeye na mama ake watakuja kukupa presha, wamama wanaoingilia mahusiano ya watoto wao huwa wanaendelea mpaka mkiwa ndoani, na mpaka umeleta humu inaonekana umeshalainika, shauri yako sie tunasubiria tu thread ingine ooooo sijui mama mkwe ananiingilia na mke wangu
 
Wazazi weng wanaharibu mausiano ya watoto yao kwasababu ya visingiziyo ving sana. Lakini nilazima ujuwe, mwanamke atakaye kupenda kutoka moyon mwake atakupenda hata kwa gharama yakifo out of that don't don't west ur tm. Yamenikuta hayo nasiwez kusahau,ila NILIJIPA MOYO NAKUAMINI HAKUNA GUMU MBELE ZA MUNGU,TENA MKE WANGU YUPO NA SIITAJI KUUMIA B'COZ OF LOVE
 
Hapana silainiki nimeshaamua kimoja sirudi nyuma kuhusu mama kuingilia mahusiano sikufichi ni kweli nikiwa chuoni nilikuwa choka mabya siunajua tena yule mama alitamka kuwa mwanaye haolewi na mtu ambaye hana hata suruali sasa leo sababu nina kazi na maisha yanaenda nafikiri ndo maana mama anashadadia
 
Wazazi weng wanaharibu mausiano ya watoto yao kwasababu ya visingiziyo ving sana. Lakini nilazima ujuwe, mwanamke atakaye kupenda kutoka moyon mwake atakupenda hata kwa gharama yakifo out of that don't don't west ur tm. Yamenikuta hayo nasiwez kusahau,ila NILIJIPA MOYO NAKUAMINI HAKUNA GUMU MBELE ZA MUNGU,TENA MKE WANGU YUPO NA SIITAJI KUUMIA B'COZ OF LOVE
pole sana kaka usijali hata mimi nimemwomba Mungu amenipa nguvu nasonga mbele sirudi nyuma
 
Hapo unahitaji jibu tena wakati ulishapigwa chini na demu hakuwa anakufeel!! Hata sasa wala hakufeel, anataka umpe maisha mazuri tu.
 
hana mapenzi endelea na msimamo wako............epuka simu zake za mara kwa mara........usikubali lunch/dinner ya pamoja labda kama unahitaji kuendeleza pale mlipoachia....usisahau kumweleza ukweli kwamba kwa sasa una mwingine asijekuharibia bure
 
Achana nae hakufai yeye na mama ake watakuja kukupa presha, wamama wanaoingilia mahusiano ya watoto wao huwa wanaendelea mpaka mkiwa ndoani, na mpaka umeleta humu inaonekana umeshalainika, shauri yako sie tunasubiria tu thread ingine ooooo sijui mama mkwe ananiingilia na mke wangu

Bila kusahau kibwagizo cha shetani alinipitia
 
nitakushangaa sana kama utamuacha huyo uliyenaye kwasasa kwasababu ya huyoaliyekuja baada ya kupata matatizo, tumia akili yako na ya kushauriwa ufanye uamuzi sahihi ndugu yangu
 
Sijui muda wa kuwasikiliza wakimponda mtu wako unaupata wapi, inaonekana unawaachia mwanya hadi wa kujadili maisha yako mtu wangu usipokua makini utaangukia pua.
 
Mapenzi sio mtihani useme ukifeli utarudia, achana nae songa mbele no 1 can love u like your mother dude!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom