Mapenzi yalivonitia umasikini.

Nakulaumu sana kwa kutoa mimba, ume ua mzee, umeua binadamu mwenzio, tena mtoto wako, yaani umeua mwanao kabisaaa....pengine huyo angekuja kuwa ndo mtetezi wako...jua katika maisha yako kuwa, mtoto wa kwanza huwa na baraka za kipekee, nyota ya mtoto wa kwanza ni tofauti kabisa na zile za wengine...hivyo umepoteza kitu cha maana sana katika maisha yako....lakini basi utafanyaje sasa omba tu msamaha kwa Mungu, lakini ukae ukijue kuwa umemuua mtoto wako mwenyewe.
 
Ndio nilimwchia yeye kwa sababu maelekezo yote yalikua yanamhusu yeye 100%

Na yai lake linaji fertilize lenyewe kwa 100%? Nawe una share yako bwana. Na hiyo njia waliyowashauri waliwaambia ina uhakika kwa 100%?
 
mnhhh...hapo nilipo-bold naona kama umekosea vile...upepo upitao ni uleeee wa kisiasa hizi pepo zingine hazipiti hivihivi bila kufanyiwa kazi ya ziada.

Nakumbuka shule nilisoma newton laws of motion ipo moja inasema a body will remain at its state of rest until external force is applied...

Huyu bwana bila ku-apply external force sioni anavyobadilika toka hiyo state of rest and worse enough soon atakuwa mariooo baloteli na mama akishaanza kazi baada ya maternity leave ndo jamaa atakuja na thread ya kulalamikia "mfumo jike" hapa jf.

naomba tumsaidie "baba fulani" hapo alipo keshaingiza hadi gea ya foowili naona gari linazidi kuzama.

anatakiwa kutafuta kazi na kurekebisha mapungufu kama yalivyosemwa na wengine
 
Na sasa hivi bado una mtizamo kuwa ilikuwa inamhusu yeye 100%??Kama bado una mtizamo huo, kuna kitu bado hujajifunza.

No. Hapana sasa hivi nishajua why we used to call them babies.
 
maji yeshamwagika... Na kifupi jamaa anahitaji kazi ili aweze kujikimu kwa maisha yake mapya na magumu kwa sasa... Tafadhali tuhjuze yafuatayo:-

1- elimu na utaalamu wako ni katika fani gani plus experience uliyonayo

2- a minimum starting salary unayodhani kidoogo inaweza kukuweka mjini ni kiasi gani

wadau naomba huyu "baba asiyejiandaa" asaidiwe kupata ajira kwa haraka sana maana mtoto ndo huyo na kodi ya pango alopanga masaki inakaribia kwisha.

jf= home of greatest thinkers

Ahsante mkuu. mi ni Accountant na experience 3 yrs, need more details please tell niku pm.
 
Kweli unawakati mgumu mkuu....ila pole sana na inakupasa ujifunze kutokana na makosa na si yeye tu, iwe fundisho kwetu pia.
 
Weakness ni zako mwenyewe, huna maamuzi yako as an individual, unafuata upepo sana.


Jifunze kutokana na makosa, tafuta kazi, kuwa na mipangilio na mikakati kichwani mwako wewe ni mwanaume hutakiwi kuishi kama unamtegemea mtu
 
Mi naona tatizo sio mapenzi, ni uzembe wako na kukosa misimamo na akili ya maisha. Halafu nashangaa, kama mlishaenda wote clinic na mkaelekezwa kujizuia na mimba ilikuwaje wewe hukuplay part yako hapo. Ulikuwa unaomba game hata siku za hatari!!!! Pole sana, ila naamini bado u kijana na una muda wa kusimama imara tena. Mungu atakusaidia.
 
Pole sana ila jamani haya maisha ya mahusiano tuyachukue kwa tahadhari sana. Mahusiano yanaweza kukumaliza kimaisha kabisa. Pia ni wakati umefika usikubali kukaa tu na binti au kijana eti unampenda wakati unaona ni mtu ambaye anapenda starehe tu. Mwanzo wa maisha ni mgumu hasa kama umetoka familia isiyo na uwezo mkubwa so aina ya marafiki ni lazima uchague sana. Again pole, ila na dada ni wakati wake wa kujifunza kuwa familia si mchezo.
 
mi nadhani iwe fundisho kwa watu wote, tuukimbie uzinifu jamani, una madhara mengi.
Nadhani chanzo cha yote haya ni uzinifu.
 
Ndio mana akabase upande wa jinsia yake, Nshakusoma Matola. Eti tumeenda mpaka Ushauri wa uzaz wa mpango,akaelekezwa jinc ya kujikinga lakini mwenzangu akabeba mimba, sio kutegesheana huku?

kwa hiyo mlivyoenda uzazi wa mpango wewe ulitumbua mijicho tu badala ya kusikiliza somo? Utasemaje ulitegeshewa wakati mwenyewe ulifanya siku za hatari ? Na utasemaje hutaki kuzaa kama unaenda peku?
 
Back
Top Bottom