Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,530
- 13,467
Wana MMU huenda tukajifunza kitu hata katika kipindi hiki cha mapenzi ya vitu au convinience!
Kuna couple moja ilikuwa haina uwezo wa kifedha iliyoishi huko Brazil. Kipindi cha Noel ambapo wenzetu wanatabia ya kupeana zawadi kilipofika, kila mtu aliumiza kichwa ampe mwenzake zawadi gani.
Mke ambaye alikuwa na nywele nzuri na ndefu (ingawa hazikutunzwa vizuri) aliamua kwenda kuziuza (ili kina King'asti wanunue) na kumnunulia mumewe mkanda wa saa yake ambao ulikuwa umekatika.
Huku nyuma mume naye aliamua kwenda kuuza ile saa isiyo na mkanda na kumnunulia mkewe brush ya nywele na mafuta ili nywele za mkewe zizidi kupendeza.
Walivyofika nyumbani Mke kafunga lemba kichwani na mume kaficha zawadi yake. Siku ya kufungua zawadi ilivyofika mama anaona brush na mafuta ya nywele ambazo hana, na mume anapata mkanda wa saa ambayo hana.
Mtaconclude wenyewe!
Robo weekend njema!