Mapenzi siyo mradi

jamadari

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
295
92
Najua umekaa mkao wa kula kutaka kujua leo nimekuja na mada gani kuhusiana na kona yetu ya mahaba. Leo nataka kuongelea tabia mbaya za baadhi ya wanawake wanaotanguliza maslahi mbele kuliko upendo katika mapenzi.

Hii imetokana na kupata maswali mawili yanayofanana kutoka kwa wasomaji wangu wa kona hii. Mmoja analalamika kuwa alikuwa na mpenzi wake, mambo yalipokwenda kombo akamkimbia, lakini baadae mambo yalipokuwa mazuri akaomba kurudi. Na wa pili, yeye analalamika kuwa mpenzi wake anapenda sana fedha, bila fedha maelewano yanakuwa madogo hata kunyimwa haki yake ya ndoa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mapenzi siyo mradi. Kama unampenda mpenzio kwa kile alichonacho na anapokosa mapenzi huyumba au kuvunjika kabisa, basitambua kuwa una kasoro. Hivi mwanamke wa aina hii ana tofauti gani na wale waliotoa miili yao kama mradi? Ni heri ujiingize huko ijulikane moja ili atakayekufuata akupe chako mapema na mkimalizana kila mtu ashike hamsini zake.

Mwenzio anapokuchagua ili uwe wake, amekuchagua ili kupunguza zile taabu ambazo alijua kuwa na wewe kuna unafuu mkubwa. Na kama angejua upo pale kimaslahi, wala asingelogwa kukuchukua na kukuweka ndani au kukufanya mpenzi wake.

Kwa sababu wenye kazi zao wapo na wanajulikana, hawali bila kuuza miili yao. Ni wazi wewe ni mmoja wapo aliyevaa ngozi ya ustaarabu kumbe ni wale wale, waliogeuza miili yao mradi. Unapoamua kuwa na mwenzako unatakiwa kuwa wewe ndiye wa kwanza kumpoza machungu ya kutwa nzima na siyo kumuongezea maumivu.

Kupata ni majaliwa na wala kukosa sio sababu ya kumkimbia mwenzako. Usione watu walikuwa maskini wa kutupwa, walipovumiliana Mungu aliwaangazia nuru na mwisho wakazila mbivu. Lazima uelewe kuna kupata na kukosa.

Mapenzi ya kweli hayaangalii kuna kitu au hakuna bali yamejaa huruma na upendo wa kweli. Hivi wewe ni mtu wa aina gani unayediriki kupigilia msumari wa moto juu ya kidonda cha mwenzio? Maisha yakiyumba unakimbia, yakiwa safi unarudi.

Hakuna raha za kila siku, lazima uelewe kuna kupata na kukosa. Kuvumilia ni sehemu ya maisha. Unapomnyima mwenzio haki yake ya ndoa au kila ukimuona ndiyo unataka shida zako zote ziishe, bila kuangalia uwezo wa mwenzako, unakuwa unakosea.

Namalizia kwa kusema waoneeni huruma wapenzi wenu, pia kuweni na mapenzi ya kweli yasiyojali mali. Kama unataka kufanya mapenzi kuwa mradi, basi jiunge na kina dada poa ili nafasi uliyoipata uwaachie wenzio wanayoitafuta kwa udi na uvumba. Kwa leo hayo machache yanatosha Asanteni.
 
SAWA kabisa, nakubaliana na wewe mia kwa mia, LAKINI? matatizo mengi ya ndoa tunaanza sisi wananume je ni wanaume wangapi tunakuwa wa wazi? wewe kesho ilikuwa uchukue mshahara leo umefukuzwa kazi,utamwambia mkeo harakaharaka umefukuzwa kazi? tena kwa kosa la kukutwa unazini ofisini na secretary? na kesho ulimuahidi mkeo kumpa sh 100,000, hazipo kazi haipo, anauliza unasema ngoja nitakupa,yeye atadhani umehonga, ugomvi unaanza,kwa hasira anaenda kwa buzi au kutafuta kidumu . Tuwe wawazi zaidi,matatizo mengi yataisha.
 
SAWA kabisa, nakubaliana na wewe mia kwa mia, LAKINI? matatizo mengi ya ndoa tunaanza sisi wananume je ni wanaume wangapi tunakuwa wa wazi? wewe kesho ilikuwa uchukue mshahara leo umefukuzwa kazi,utamwambia mkeo harakaharaka umefukuzwa kazi? tena kwa kosa la kukutwa unazini ofisini na secretary? na kesho ulimuahidi mkeo kumpa sh 100,000, hazipo kazi haipo, anauliza unasema ngoja nitakupa,yeye atadhani umehonga, ugomvi unaanza,kwa hasira anaenda kwa buzi au kutafuta kidumu . Tuwe wawazi zaidi,matatizo mengi yataisha.

Tall kuna maswali uliulizwa sehemu kuhusu umri wako ukapiga chenga! Soo nikimnyima shemejio hela ya saloon niandike maumivu! EEh hii nayo ni hatari sana!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom