Mapenzi ni nini hasa?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Kila siku najiuliza hivi mapenzi ni nini hasa?
Najiuliza kwa nini watu wanapenda mapenzi?
Nashuhudia ili mapenzi yanoge je ni lazima kuwe na wivu ndani yake?
Nashuhudia watu wengi wanatoa roho zao kisa mapenzi?
Hivi mapenzi jamani nini kwa kweli?
Naomba msaada nifanye nini ili niweze kuyafaidi mapenzi.

Ni nini kiini cha wivu katika mapenzi?
Hivi mapenzi yana nini mpaka mtu unang'ang'ania?
Mapenzi kwa nini mtu akisaliti yupo radhi kujinyonga?
Naombeni msaada nilazima uliye mzimia na kufa na kuoza juu yake mkafanya mapenzi?
Mapenzi jamani yana nini utakuta ndugu wanahasamiana kwa ajili ya mapenzi.
Nitaendelea.....
 
mapenzi KIZUNGUMKUTI!

Hivi mapenzi yana formula ambayo unaweza ukaitumia?
Kwanini mapenzi yanakosanisha watu na kujenga uhasama?
Je kuna haja ya kuyaendeleza mapenzi jamani?
 
Hivi mapenzi yana formula ambayo unaweza ukaitumia?
Kwanini mapenzi yanakosanisha watu na kujenga uhasama?
Je kuna haja ya kuyaendeleza mapenzi jamani?
hahahahah!
We mkuu inaonekana YOU HAVE SOMETHING IN YOUR HEAD WHICH IS EATING YOU UP!we sema tu
 
hahahahah!
We mkuu inaonekana YOU HAVE SOMETHING IN YOUR HEAD WHICH IS EATING YOU UP!we sema tu

Mapenzi jamani wanasema ni matamu utamu wake ni upi?
Mapenzi ni shubili wengine wanadai,shubili yake ni ipi?
Mwanajamii,Masanilo,Yo Yo,Msanii,Kaizer,Mbu,WOS,Nyamayao,Penny mpo wapi jamani mnisaidie sielewi nini maana ya mapenzi.
 
Eh sasa Fidel ndugu yangu unatutega
Kusema kweli kwa experience yangu naweza sema mapenzi ni vyote utamu na shubiri.
Utamu- Pale mnapokuwa mnaelewana na mpensio, mnaongea lugha moja na kufurahiana uwepo wenu- mara nyingi hii huwa wakati ule wa mwanzoni wakati novel bado ipo.

Shubiri - pale mnapokuwa mmechokana na kuwa na tofauti zenu hasa mtaposhindwa kuzishughuliki8a/tatua

mie nimeonja sehemu zote mbili so am writing according to my experience
 
Mapenzi jamani wanasema ni matamu utamu wake ni upi?
Mapenzi ni shubili wengine wanadai,shubili yake ni ipi?
Mwanajamii,Masanilo,Yo Yo,Msanii,Kaizer,Mbu,WOS,Nyamayao,Penny mpo wapi jamani mnisaidie sielewi nini maana ya mapenzi.

Tafiri rasmi na sahihi kabisa ya mapenzi Mheshimiwa Fidel 180 ni vile unavyoishi na mrembo wako au mywife wako.
Ukingoja ya kusimuliwa na wengine, imekula kwako, maana watakusimulia jinsi wao wanavyo`do` na akina Chausiku wao! ha ha haaaaa!!!
Usihofu kwamba unavyoenda wewe ni wrong, no no nooo,... uko sawa kabisa, maana hii mambo ni personal bana!!
 
Mapenzi jamani wanasema ni matamu utamu wake ni upi?

...utamu wake upende nawe upendwe!

Mapenzi ni shubili wengine wanadai,shubili yake ni ipi?

...Fidel80, shubili ni pale yule umpendaye yeye wala hana habari nawe!

Mwanajamii,Masanilo,Yo Yo,Msanii,Kaizer,Mbu,WOS,Nyamayao,Penny mpo wapi jamani mnisaidie sielewi nini maana ya mapenzi.

... mapenzi ni pamoja na 'uchoyo' wa roho kutaka "umtakaye" awe wako peke yako, kwa hali yeyote ile iwayo hata kama itabidi udhalilike mbele ya jamii inayokuzunguka.
 
... mapenzi ni pamoja na 'uchoyo' wa roho kutaka "umtakaye" awe wako peke yako, kwa hali yeyote ile iwayo hata kama itabidi udhalilike mbele ya jamii inayokuzunguka.

nimeipenda
 
Ni vigumu sana kupata majibu kuhusu mapenzi kwani kila mtu ana jibu lake kwa swali lile lile.Majibu kuhusiana na mapenzi utokana na experience,mbaya zaidi kila mtu ana uzoefu wake katika hili.
 
Mapenzi... mapenzi aisee ni vigumu sana kuyaelezea, wanaosema ni pamoja na uchoyo mi naona kama kuna kijiukweli ndani yake, labda niongeze na ubinafsi. Nafikiri kwa wengi jibu la mapenzi ni nini litaendana na yuko katika stage gani ya mapenzi. Kwa wenzangu na mimi 30+ nafikiri itakuwa ngumu kutoa jibu la haraka haraka kuwa mapenzi ni nini. Tunachokubaliana wote ni kwamba mapenzi yako so complicated, si kitu ya kurukia kichwa kichwa...
 
Love is love...Love is a understanding... it's unconditional
I will quote this poem by Elizabeth Barrett Browning...U will love it too. it sums it up for love...

""How do I love thee? Let me count the ways.
I love thee to the depth and breadth and height
My soul can reach, when feeling out of sight
For the ends of Being and ideal Grace.
I love thee to the level of every day's
Most quiet need, by sun and candlelight.
I love thee freely, as men strive for Right;
I love thee purely, as they turn from Praise.
I love with a passion put to use
In my old griefs, and with my childhood's faith.
I love thee with a love I seemed to lose
With my lost saints, I love thee with the breath,
Smiles, tears, of all my life! and, if God choose,
I shall but love thee better after death. "

Mapenzi ni subira, uelewano, So many small things.
 
Mapenzi ni kuwa tayari kujitoa Mhanga kwa uwapendao kuanzia katika familia yako
 
Eh sasa Fidel ndugu yangu unatutega
Kusema kweli kwa experience yangu naweza sema mapenzi ni vyote utamu na shubiri.

Mwana mimi sikutegi lakini nataka nipate ufafanuzi haya mapenzi kama ni matamu kwa nini watu wanauana kwa ajili ya wivu wa haya mapenzi.
Na hapo kama ni shubili mtu unateseka kwa ajili ya mapenzi kwa nini usiayaache jamani?
 
Hehehehe Mbu umeniacha hoi hapo kwenye uchoyo.
Duh mtu hata kama anamiliki nyumba kubwa,nyumba kati na nyumba ndogo anataka amege zote yeye mwenyewe amfumanie timbwili lake hapo hehehe sasa hao wote 3 wamzubili mzee mmoja inawezekana kweli?
 
...huyo tunamwita 'mlafi'! si unajua mwenye tabia za ulafi akivimbiwa anakuwaje? mwenyewe hujiona kafwaudu kumbe -anahitaji kusaidiwa, hajiwezi!
 
Mapenzi hayana formula,na wala hayana utamu maana yake ukitaka umpende mtu lazima umpende hata kama akutaki, mapenzi hayaeleweki, si umeona hiyo avatar ya mkuu kyakya, dogo ana show love kwa pig,
NOTE: Chochote ambacho akili yako na moyo wako utakua umeupeleka huko 97% fahamu utakuja siku kulia tuu, siyo mapenzi,hata pesa, watoto,n.k
 
Back
Top Bottom