Mapenzi ni kitu gani?

Mudathir Ali

Member
Jul 4, 2016
28
30
Nakuleteeni swali, wajuzi wa maarifa,
Mlojaliwa akili, na bongo zisizokufa,
Muwezao ona mbali, naombeni maarifa,
Mapenzi ni kitu gani?

Mapenzi ni kitu gani, swali langu nauliza,
Kwani yalianza lini, hadi leo yatatiza,
Watu kuzama dimbwini, mbona yanawaumiza,
Mapenzi ni kitu gani?

Ama kuna tofauti, na yale ya vitabuni,
Yetu kizungumkuti, wengi wayalaani,
Kwamba raha hawapati, tena humo mapenzini,
Mapenzi ni kitu gani?

Niliyaanza zamani, nami pia nikapenda,
Tena niliyaamini, nazo siku zikaenda,
Pamoja nayo imani, mpenzi akanitenda,
Mapenzi ni kitu gani?

Walisema kupotea, ndiko kuijua njia,
Kidogo nikatulia, maumivu kupungua,
Ni kweli niliumia, nikawaza mara mia,
Mapenzi ni kitu gani?

Ikajatokea tena, mapenzini nikazama,
Wengine sikuwaona, kwake moyo kutuwama,
Nilimpenda kwa sana, sikujali wakisema,
Mapenzi ni kitu gani?

Ikajatokea naye, kanifanya kuumia,
Yule nimwaminiaye, ubaya kunifanyia,
Nani sasa awezaye, swali akanijibia,
Mapenzi ni kitu gani?

Huyu mwingine wa tatu, alinikata maini,
Pengine hanao utu, kashindwa kunithamini,
Kaona si malikitu, sipati jibu moyoni,
Mapenzi ni kitu gani?

Kapasi kwenda chuoni, nikabaki mtaani,
Hesabu zake kichwani, zikagoma abadani,
Akaniona wa nini, basi kanipiga chini,
Mapenzi ni kitu gani?
Huyu kaenda Ulaya, akasema sasa basi,
Kaniumiza vibaya, sitolipiza kisasi,
Sikumfanyia baya, akaninyima nafasi,
Mapenzi ni kitu gani?

Na huyu ile zawadi, kampa mtu mwingine,
Akaivunja ahadi, kwa kuzaa na mwingine,
Nadhani ni makusudi, sijiulizi jingine,
Mapenzi ni kitu gani?

Nikaipata adhabu, mapenzi yakanitesa,
Zingenipanda ghadhabu, dali wangu kumkosa,
Sijapata bado jibu, ndani kuna nini hasa,
Mapenzi ni kitu gani?

Wanasema yana raha, mi’ raha sijaipata,
Wanasema ni furaha, machozi yangenifuta,
Na kama siyo karaha, mbona mie nimesota,
Mapenzi ni kitu gani?

Ya kutoka kwa mzazi, hakika nayaamini,
Lakini ya kwa mpenzi, nimeona walakini,
Nishafanyiwa ushenzi, nikazama majonzini,
Mapenzi ni kitu gani?

Mapenzi ni raha gani, mbona wayasifia,
Ama yamo nchi gani, watu wasikoumia,
Hebu jifikirisheni, majibu kunipatia,
Mapenzi ni kitu gani?

Nawauliza malenga, nami nitoke kizani,
Haya watu wanalonga, kweli yapo duniani?
Ama kunayo machanga, yaso na ladha kwa ndani?
Mapenzi ni kitu gani?

Kwani huwa vipivipi, hayo mapenzi ya kweli?
Washayaonja wangapi, leo waseme ukweli,
Tena siyo ya makapi, yaso na ubaradhuli,
Mapenzi ni kitu gani?

Semeni semeni jama, nahitaji kuelewa,
Naogopa kuja zama, vile nilivyotokewa,
Nifahamu kuyapima, nisipate kuchachawa,
Mapenzi ni kitu gani?
Swali nimewauliza.
 
Mapenzi ni ngonjera isyoeleweka

Mapenzi ni fumbo lisilo na ufumbuzi

Mapenzi ni shairi bila vina

Mapenzi ni kitendawili bila jibu

Mapenzi ni mapenzi tu.
 
Mimi pia nashangaa watu chunvini kuzama,
kutwa pilikapilika na wengine kufumana,
wapo walioenda mbali kufikia kusagana,
Vidume bila aibu kushinda kugeuzana,
Nafunga pia na swali mapenzi ni kitu gani?
 
Mimi pia nashangaa watu chunvini kuzama,
kutwa pilikapilika na wengine kufumana,
wapo walioenda mbali kufikia kusagana,
Vidume bila aibu kushinda kugeuzana,
Nafunga pia na swali mapenzi ni kitu gani?

umetisha kumbe na ww huvumi lakin umo
 
Mapenzi ni hali inayojitokeza baina ya wa tu wawili (most often than not, me na ke) pale ujinga wao unapofanana
 
NIMEPATA JIBU:

KWA MWANAMKE:

Mapenzi ni, mawasiliano, romance, matunzo, monogamy,full attention,romantic dinners and walks,surprised gifts,cuddling,ndoa,pesa,kutimiza ahadi kwa wakati...hii list haina mwisho.

KWA MWANAUME
Mapenzi ni KUPIGA KUNI, full stop.
 
Ni mahusiano baina ya watu wa2 wenye jinsia mbil tofaut nayo mahusiano hubebe vtu vingi ikiwemo uvumilivu na mambo meng yanayohusu mahusiano kwa ujumla,,,na micng muhim ya mapenz ni LAZIMA uwe mkwel,muwaz kwa mwenzako,kuheshimiana,kuvumiliana n.k ni ivo yaan navooelew
 
MAPENZI NI MAISHA.
hakuna maisha bila mapenzi na hakuna mapenzi bila maisha.
Mapenzi hayakwepeki ikiwa upo hai au ukiishi.
Mapenzi ni bahari na Hili neno maana yake ni kwamba mapenzi yanafananishwa na neno bahari aina mwisho.
Na mapenzi yanaumiza ikiwa unapata marejeo hasi kutoka kwa kile ulicho kitarajia baada ya kujitoa kimwili, kiakili, kiroho
 
Back
Top Bottom