mapenzi na ndumba

hakuna uchawi acheni kuishi kwa uoga,anayejua kuroga natangaza hapa aniroge mie nisipewe ban na PAW lol
 
Yaani ukisikia stori za kinamama wanavyokwenda kwa Kalumanzila utachoka kabisa.Kusema kweli kinababa sijui huwa tunalishwa uchafu kiasi gani.Wengine nasikia wanawapikia waume zao kwa maji yanayoosha maiti mochware,wengine nasikia wanachukua vipande vya nyama wanavisokomeza kusikotamkika kisha wanawakaangizia waume zao,ili mradi ni waganga kutaka kuzidiana ufundi. Jamani jamani uuuuuuwwwwiiiii,huko kwa mahawara ndo usiseme,ndo hakufai kabisa maana hawara ndo anakuwa anahangaika umsahau mkeo.Inachosha kabisa!
sasa jamani kama utapewa na mke wako wa nadi inamaana hakuna mausiano mema nyumbani ukitoka nje anatafuta security ya ugali unaouleta kwake USHAURI WANGU kaa na mkeo nyumbani usiende nje na hakikisha anakuaamini na imani hiyo uionyeshe kwake hakika kwa kailimanzira kwishiney
 
ni tatizo la mob mentality,akianza mmoja baadae genge zima linahamia kwa babu.

Ukweli kabisa na hawajui inawezekana mganga akakupa wazi kapike chakula kizuri kwa mumeo na muwekee dawa hii kumbe umepewa unga wa mahindi
Ukarudi nyumbani ukajipinda ukapika chakula chako kizuri anachopenda mumeo na ukaweka ule unga ukadhani ni daw akumbe hakuna kitu
Unaona taratibu mume anarudisha upendo nyumbani kumbe mapenzi yamerudi kutokana na maandalizi yako ya chakula na the way umemkaribisha pale nyumbani wewe mawazo yako yakakimbilia dawa
 
Hii kitu ipo jamani cz kwenye nyumba tuliyopanga kuna wapangaji wenzetu mamlaka ya baba anayo mama,mwanaume anafanya kila kitu hadi zamu za kudeki chooni tunaye..mkewe ni mzima haumwi hafanyi kazi ye ni full pombe akilala nje tatu sawa tu,akienda club kujirusha mwanaume ye ndani tu hatoki na mkewe akirudi anagonga mlango anafunguliwa kama kawaida na kuulizwa mbona chakula cha leo kibaya baba nanii.Smtms huwa anatoa kauli mbaya nimekwambia nguo hujafua unanitania au niende safari zangu za Tanga kukurekebisha,so ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii na tunaviona.
WANAUME MSIACHE KUOMBA MNAPOTAFUTA MKE AU MCHUMBA ANAE KUPENDA HAWEZI KUKUFANYA HIVYO.
 
Tatizo ni makundi na sinema za ki-nigeria. Hata wanawake wasio na wasiwasi na waume zao wanashauriwa waende kwa mganga "kuimarisha" ndoa. Ndio mazungumzo ya salon nyingi.
 
Jamani haya mastory mmeamua kutuondolea appetite au??? Maana mambo ya kula vitu vilivyowekwa huko sijui wapi, khaaa, basi bana.
 
Post hii imenikumbusha niliyoyasikia leo..nilienda kumtembelea rafiki yangu kwao,kwa bahati nikamkuta na bibi yake.basi katika mazungumzo yetu lilikuja suala la mwanamke(anayefaa) wa kuoa.yule bibi alimwambia mjukuu wke(rafiki yangu) akioa m2 kutoka kabila jingine yeye(bibi) atamwendea kwa mganga amloge(mke) ili afe kabla ya huyo mke hajamwahi na kumloga mjukuu wake ili apate mali
 
sasa jamani kama utapewa na mke wako wa nadi inamaana hakuna mausiano mema nyumbani ukitoka nje anatafuta security ya ugali unaouleta kwake USHAURI WANGU kaa na mkeo nyumbani usiende nje na hakikisha anakuaamini na imani hiyo uionyeshe kwake hakika kwa kailimanzira kwishiney

sawa Mkuu,tumekusikia.
 
Ukweli kabisa na hawajui inawezekana mganga akakupa wazi kapike chakula kizuri kwa mumeo na muwekee dawa hii kumbe umepewa unga wa mahindi
Ukarudi nyumbani ukajipinda ukapika chakula chako kizuri anachopenda mumeo na ukaweka ule unga ukadhani ni daw akumbe hakuna kitu
Unaona taratibu mume anarudisha upendo nyumbani kumbe mapenzi yamerudi kutokana na maandalizi yako ya chakula na the way umemkaribisha pale nyumbani wewe mawazo yako yakakimbilia dawa

masuala ya saikolojia sio?
 
Yaani ukisikia stori za kinamama wanavyokwenda kwa Kalumanzila utachoka kabisa.Kusema kweli kinababa sijui huwa tunalishwa uchafu kiasi gani.Wengine nasikia wanawapikia waume zao kwa maji yanayoosha maiti mochware,wengine nasikia wanachukua vipande vya nyama wanavisokomeza kusikotamkika kisha wanawakaangizia waume zao,ili mradi ni waganga kutaka kuzidiana ufundi. Jamani jamani uuuuuuwwwwiiiii,huko kwa mahawara ndo usiseme,ndo hakufai kabisa maana hawara ndo anakuwa anahangaika umsahau mkeo.Inachosha kabisa!

Mimi huwa naokotaga kipande cha jiwe barabarani naiweka mfuko wa nyuma wakati naenda kwa hawara ndiyo kiboko ya wachawi. Au saa zingine nageuza chupi nyuma mbele!
 
Back
Top Bottom