Mapenzi na kigezo cha elimu na kipato (chapaa)

Mbavu mbili

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
1,456
872
Dhahiri naweza kuwa sahihi kuamini kuwa siku hizi hakuna mapenzi ya kweli na ya dhati. Pesa huamua mahusiano ya wapenzi. Vipi kuhusu Elimu? je kuna umuhimu wa kuzingatia kigezo cha elimu kwa wanandoa, kama wafanyavyo kwa kuangalia chapaaaa
 
Lazima tuwe wakweli kwa maisha ya sasa yalivyo tight huwezi ukapenda tu hovyo hovyo. Eti umpende mtu ambaye yupoyupo tu eti kisa mapenzi hayachagui huu ni upuuzi kabisa. Unapoamua kuoa/olewa lazima upate mwenza ambaye mtasaidiana katika maisha kwa hiyo lazima uwe na vigezo vya mwenza ambaye unamuhitaji ambavyo unahisi akiwa navyo itakuwa ni msaada ktk maisha yenu.
 
Dhahiri naweza kuwa sahihi kuamini kuwa siku hizi hakuna mapenzi ya kweli na ya dhati. Pesa huamua mahusiano ya wapenzi. Vipi kuhusu Elimu? je kuna umuhimu wa kuzingatia kigezo cha elimu kwa wanandoa, kama wafanyavyo kwa kuangalia chapaaaa



Vigezo vya elimu vinaenda sambamba na pesa... unapopata mchumba msomi hata kama hajatoka bado kuna kale ka hope kua jamaa ananifaa na nikivumilia tutafika tu ninapopataka (pesa),,
 
wanasemaga mapenzi kitendawili….. uzuri,umri,elimu ,pesa yote hayategui hiko kitendawili bali ni watu kuelewana tu na hisia zao. hisia zikiisha mapenzi yanaisha kwa nyumba mnakuwa wapangaji tu hata muwe na pesa za kumwaga uzuri,elimu vyote havitakua na maana tena
 
What matters first is love...then elimu na pesa huja baadaye. Maana mapenzi ni kila kitu na mara nyingine ni vizuri kuangalia elimu na haswa kwa wanaume. Mke akikuzidi mara nyingi kuna inveriority complex kubwa sana toka kwa wanaume..na haswa kama mwanamke anarank kubwa kidogo kazini na haswa itakayomfanya awe anatoka sana, au anasafiri sana. Mapenzi ya dhahiri yapo itategemea na wewe tu choice na kipaumbele chako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom