Mapenzi motomoto hayaji yenyewe lazima muwe wabunifu na wavumbuzi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
[h=3]Moto Umezima[/h]


SWALI
Mimi na mume wangu tumekuwa kwenye ndoa sasa ni mwaka wa 11, maisha yetu ni mazuri sana kila eneo la ndoa yetu isipokuwa suala la sex. Najiona kukumbuka sana namna moto wa mapenzi (passion) ulikuwa huko nyuma na sasa kila kitu kinaenda ovyo Linapokuja suala la sex.
Je tufanyeje ili mambo yarudi kama zamani?
Ni mimi Edna
JIBU:
Swali lako ni zuri na si mara ya kwanza kuulizwa hapa.
Pia nikupongeze kwa kufikisha miaka 11 pamoja Kwani maisha ya mahusiano siku za leo ni Tofauti sana.
Jambo la msingi ni kufahamu kwamba umekuwa na ndoa nzuri kwa miaka 11 kwa Sababu kila siku mmekuwa mnajitahidi kufanyia kazi ndoa yenu na pia maisha ya sex yameanza kuelekea kwenye velanda ya ICU kwa Sababu mmejisahau na kuacha kufanya vile mlikuwa mnafanya huko nyuma.
Inawezekana mnafanya kila kitu kwa kuzoeana na mazoea kuanzia kabla ya kuingia chumbani hata wakati mkiwa chumbani.
Je, unawezaje kurudisha moto wa mapenzi wewe na mumeo?
Jambo la msingi ni namna kila mmoja anajitoa (committed) kuwa wa motomoto kimapenzi na suala zima la maisha ya mapenzi kwa pamoja.
Baada ya kujitoa suala linalofuata ni kupanga, panga na fikiria vitu ambavyo mnaweza kufanya pamoja, vitu vipya, kuwa wabunifu wa nini mfanye pamoja na kile kitendo tu cha kufanyia kazi yale mnataka kufanya pamoja tayari kitaanza kuwapa furaha na msisimko wa pamoja kimapenzi.
Sasa Hakuna moto wa mapenzi kwa kuwa ule moto mmeuzima au umeenda kulala usingizi mzito, ni muda wa kuwasha na kuamka, jaribu vitu vipya, jaribu mlalo mpya wakati wa sex, jaribu kwenda kufurahia miili yenu sehemu Tofauti na hapo chumbani kwenu, jaribu muda Tofauti wa sex, jaribu kugusa sehemu Tofauti katika mwili wakati wa kufanya maandalizi na fanya yote kwa upendo na kwa kupokea na kutoa.
Jaribu kusafiri au kutembelea sehemu mpya pamoja kama mke na mume (mbuga za wanyama, beach au hotel)
Pika pamoja, cheza pamoja, piga story pamoja, mlishe chakula mpaka ashibe, kumbatianeni, shikaneni, mwambie maneno matamu ambayo hujawahi kuyasema, mtie moyo, msifie, mpende nk
Mapenzi motomoto hayaji yenyewe lazima muwe wabunifu na wavumbuzi
Uwe mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu, mbunifu…………
 
Unfortunately mambo mengi ambayo hua recommended au ambazo ni njia sahihi kwa kurudisha mapenzi moto moto ndani ya ndoa ni vigumu saana kwa couples nyingi kufanikiwa zifikisha... hasa kama ndoa ina more than seven years... Hii ni tokana na the simple fact kua mnakua na mambo mengi yameongezeka as well as majukumu... Watoto... responsibilites... na unakuta both parties ni wafanya kazi... woote mwarudi mko hoi huku mkifanya tena shughuli za nyumbani... Ndo maana kazi ya watu kucheat (sababu anaona exitements huko nje) ni kubwa saana kwa wanandoa wanao ishi out of obligation ambayo sex inachukua nafasi ndogo katika priorities...
 
Ashadii umesema kweli kabisa kwenye ndoa moto wa sex unapotea pind majukumu yanapoongezeka. na wakat mwengine m1 atajaribu kuyaamsha lkn mmoja atakuwa kama gogo linalo hitaji kukatwa kila cku
 
Back
Top Bottom