Mapenzi ktk vyuo kuu

Unafikiri kwanini alikupenda wewe na je alikotoka unafikiri hakua na mwingine na je wewe hukuwa na mwingine? Chuoni mapenzi ya pesa na Elimu tu huna msaada wa hayo hakuna atakayekupenda.
Mapenzi ya dhati chuon yawezekana ila inategemea na watu(walengwa)mfn mm mbona nimekutana na mchumba wngu chuon na mwez wa 5 twaoana,ila kiukweli kuna uchakachuaji wa hali ya juu sn wenyewe wanaita kulindana
 
ili kudetermine kama mapenzi ya chuoni yanaweza kuwa ya kweli au la,yategemea na wenyewe walengwa mlipokutana mlikua na nia gani na mna malengo gani juu ya mahusiano yenu,kuna wengine hata wao wenyewe tu wakiwa pamoja wanajua fika wanapass tym tu, na wengine hudhamiria kuwa na uhusiano wa muda mrefu..

Sasa kwa wale wenye nia na dhamira ya kuwa pamoja kwa muda mrefu,wakiweza pendana kweli,heshimiana na jaliana haswaaa, watapitia stage nyingi sana za malumbano,maugomvi,ma break up na make up lakini experience zote hizo zitawafanya wawe stronger na wadumu sana..

Mbona mimi na mama watoto tulianzia maisha yetu ya mapenzi chuoni!!!!hadi leo hii tuko pamoja bado
 
Inaonekana wanafunzi wengi wa vyuo/vyuo vikuu hawaaminiki kuwa na mapenzi ya dhati.hii ni asa kwa wanafunzi walio acha wapenzi wao maskani. mnasemaje nawasikiliza

Ilonza, chuoni kuna mapenzi yanayotokana na kukidhi matamanio ya kimwili na sio mapenzi yanayotokana na upendo wa dhati.

Chuon ni rahisi sana kufanya Sex Games kuliko uraiani

Chuoni in most cases sio sehemu ya kutafuta mpenzi, ni sehemu ya kufanya mapenzi
 
Inauma sana watu kusaliti ndoa zao kisa tamaa ya siku moja.

si unajua tena wale wadudu wa @-)(ge wanavyosumbua especiall kwa wanandoa wamezoea ku do weekly mara ghafla wakuwa mbali hivyo kifuatacho ni usaliti.
 
lakini ni asilimia ngapi wanaoanzisha mapenzi chuoni wanakuja kuoana na hao wapenzi wao? Kama sio pass time

Asilimia ni ndogo sana. Nakumbuka wakati naingia chuo ulikuwa wakati serikali ilipoanzisha zile juhudi za kuwa na wasichana wengi vyuo vikuu. Watu tulifurahia hiyo, lakini tulikuwa tunapigwa vibuti ile mbaya. Yaani ilikuwa vingumu kumtongoza mtoto wa chuo akakubalia. Walikuwa wanajiconsider kama high class. Labda hali imebadilika kwa sasa.

Kwa experience yangu ya chuo wakati huo,nwasichana wengi walikuwa wakitembea na wanaume wa mtaani. Na hawa wanaume walikuwa sio uchwara. Walikuwa ni wanaume wenye pesa zao za kutanua. Ilikuwa ikifika ijumaa jioni unaona tuu magari binafsi yantinga cumpus kupick up girls. Wasichana wa chuo walikuwa na hulka ya kutowadate wanaume wa chuo kwa sababu tulikuwa tunapata income sawa. income yenyewe tulikuwa tunaiita ngororo (jina la aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya sayansi, teknologia na elimu ya juu wakati huo).

Kuona hivyo wanaume wa chuo nao wakaamua kwenda kudate mtaani. Pia ilikuwa kipindi hicho ambacho wamaume walikuwa wakiwaajiri mahousegirls kwa nia ya kuwapikia, kupiga soap soap room, na wengine walikuwa wanajishindia hapo hapo. Tulikuwa na pesa kipindi hicho.

Interesting thing ni kuwa tulipokuwa mwaka wa mwisho wasichana wengi walijikuta wako single. Ilionekama kama vile wale wanaume wa mtaani walikuwa hana long plans na hawa wasichana. By the way, walishakuwa wakubwa na hawakuwa tena na ule mvuto wa first year. Hapo sasa walijaribu kujiaatch tena na wanaume wa chuo lakini haikuwezekana b'se these guys have already moved on. In addition, walikuwa tayari walishajua CV za hawa wasichana, so they were no longer interested in them. Pia wakati huo kulikuwa na wanaume chuoni na mitaani waliokuwa na zile fikra za kutooa wanawake waliopiga shule.

Wasichana ambao walikuja kuolewa na watu waliokuwa nao chuo ni wachache. Tena wengi wao walikuwa tayari na mahusiano hata kabla ya kuja chuoni. Wanaume wengi walienda kuoa mitaani. Pia baadhi ya wasichana waliolewa na watu wa mitaani lakini bado kuna ambao wapo single though walikuwa na life kiaina chuoni.
 
Ilonza, chuoni kuna mapenzi yanayotokana na kukidhi matamanio ya kimwili na sio mapenzi yanayotokana na upendo wa dhati.

Chuon ni rahisi sana kufanya Sex Games kuliko uraiani

Chuoni in most cases sio sehemu ya kutafuta mpenzi, ni sehemu ya kufanya mapenzi

mkuu nakuunga mkono...chuo ni sehemu ya kujamiiana2..
 
kati ya makundi hatari katika maambukizi ya ukimwi ....JAMII ZA VYUO VIKUU IMEONGEZEKA....sasa hakuna tofauti na makundi kama WACHIMBA MADINI,MADEREVA WA MASAFA MAREFU,WAHUDUMU WA BAA NA MAKAHABA....japo ukweli unabaki kuwa katika mtu mmoja mmoja wote tupo hatarini lakini katika makundi jamii hii ya wasomi inashika kasi ya ajabu hasaa kipindi cha BOOM....!
 
Mapenzi ya chuo matamu jamani maana unajikuta unasahau matatizo yako yote hasa ukimpata anaeyajua kiasi kwamba hata likizo unajikuta huna hamu ya kwenda nyumbani kukutana na uliyemwacha.

This is vere true,
kwanza unakuwa unapenda chuo kuliko kawaida, kikifunguliwa unawahi kwenda, na kikifungwa unajichelewesha kuondoka ilimradi tu...! mbaya ni pale mmoja akifeli au kupata maksi za chini hasa mwanamke, ndo mnaanza kulaumiana, au mwenzio anamtafuta mwingine atakaye msaidia kusoma zaidi na kumpa mapenzi zaidi, ndo hapo kama unaye uliemwacha nyumbani unamsahau akikupigia unamwambia niko library, mara lecture, mara discussion.... aah bora tulishaga maliza
 
Inaonekana wanafunzi wengi wa vyuo/vyuo vikuu hawaaminiki kuwa na mapenzi ya dhati.hii ni asa kwa wanafunzi walio acha wapenzi wao maskani. mnasemaje nawasikiliza
chuo ni mahala pa kukulia na kujamiana,hamna kitu kama mapenzi hata siku mmoja.YAANI WANACHUO TUNAPENDA CHUO KULIKO KAWA..
Mdada wa chuo akimpata jamaa wa mtaa aliyena noti basi kila wikiend hatalala chuo hata kama jpili kuna pepa ya kikomando.
wanamtaa lazma wawe macho na hawa wadada.
 
Back
Top Bottom