Elections 2010 Mapendekezo ya spika CCM yamevunja katiba?

Percival Salama

Senior Member
Feb 3, 2010
118
7
Je hatua ya CCM kufanya mapendekezo ya spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kigezo cha Jinsia kimekanya katiba sehemu ya 9 kifungu kidogo cha (g)? wadau naomba masaada hapo.
9.​
Lengo la Katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa
chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na
kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, amabyo inasisitiza
utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira
yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano. Kwa hiyo, Mamlaka ya
Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na

shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha-

(g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma
vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya​
mtu;
 
madhumuni hayo ya kumpitisha ke bila shaka pengine ni kwa hatua ya chama chao. kumbuka chama chochote ni kikundi cha watu na katika kikundi kwa kawaida kuna kundi dogo lenye influence.

ndani ya ccm tunaambiwa waliofanya maamuzi hayo ni cc ambayo kama sikosei hawafiki hata 50 kwa idadi; aidha chama hicho sasa tunaambiwa kinashikiliwa na watuhumiwa wa ufisadi na wale wapiganaji wamepoteza vita rasmi kwa kushindwa kwa sitta.

kwa mawazo yangu kifungu hicho hakikiukwi kwa sababu ni kwa ngazi ya chama/kikundi; lakini ingekuwa bungeni kisha uamuzi ukatolewa kwamba sasa spika atakayechaguliwa lazima awe mwanamke, ndipo hapo sasa hiyo article itakuwa contravened.
 
Back
Top Bottom