Mapendekezo ya serikali hayatawezesha kikamilifu uchaguzi huru wa viongozi

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
KWA kuwa siasa (nikimaanisha siasa safi) ni hitaji muhimu la maendeleo kama alivyowahi kusema hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere; basi uendeshwaji wa uchaguzi (kwa maana ya uchaguzi huru na haki); ndio njia ya kulipata hitaji hili.
Uendeshwaji wa uchaguzi huru na haki hutupatia pia hitaji jingine la msingi kwa maendeleo - yaani “Uongozi Bora”. Suala kuu ni kuwa na mifumo ya kikatiba na kisheria na kiuwanja wa kisiasa ambayo inahakikisha uchaguzi huru na haki.
Katika siku za karibuni pamekuwepo na mjadala kuhusu sheria za uchaguzi uliotokana na uamuzi wa serikali kutoa miswada miwili: Muswada wa Marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Sheria ya Fedha za Uchaguzi wa mwaka 2010.
Hata hivyo, mjadala huo kwa kiasi kikubwa umejikita katika mapendekezo ya serikali yaliyomo kwenye sheria mpya ya fedha za uchaguzi na kufunika mjadala kuhusu marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo kwa maoni yangu ndio msingi wa uchaguzi wenyewe.
Hivyo, katika makala hii sitachambua muswada mpya wa fedha za uchaguzi bali nitajikita katika maudhui ya marekebisho ya sheria ya uchaguzi.
Ikumbukwe kwamba tume ya uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa Aprili 21, 2009 mkoani Dar es Salaam mkutano ambao nilishiriki.
Katika mkutano huo nilieleza masikitiko yangu kwamba tangu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka 2005, Tume ya Uchaguzi haikuitisha mkutano na vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu hadi mwaka 2009, takriban mwaka mmoja tu kabla ya uchaguzi.
Hii inaacha maswali kuhusu dhamira ya tume katika kuhakikisha taifa linakuwa na uchaguzi huru na haki; hasa ukizingatia kwamba toka mwaka 2006; CHADEMA na wadau wengine tumekuwa tukihitaji kukutana na tume na pia tukihimiza mchakato wa mabadiliko ya kweli kuanzishwa.
Niliweka bayana mashaka yangu nikizingatia kuwa masuala ya uchaguzi mkuu yanahusu mabadiliko ya kisheria, kimfumo n.k, ambayo huchukua muda mrefu kuweza kupitishwa na kutekelezwa, hivyo kitendo cha kuanza majadiliano wakati huu, kinaashiria kuwa sehemu kubwa ya yatakayojadiliwa; hayataweza kutekelezwa.
Kwa upande mwingine nilishukuru kuitishwa kwa mkutano huo nikiwa na matarajio kuwa baada ya kukutana huko tume kwa kushirikiana na serikali ingeweza bado kuchukua hatua za haraka kuweza kufanya mabadiliko yanayokusudiwa katika kipindi kifupi kilichobaki.
Mkutano huo, baada ya kupokea maoni ya ujumla kutoka kwa vyama vya siasa uliahirishwa baada ya muda mfupi bila maamuzi yoyote ya msingi kufikiwa kwa maelezo kwamba ungeitishwa mkutano mwingine baada ya kufanya mapitio ya hoja na vielelezo vilivyotolewa na wachangiaji mbalimbali.
Takriban miezi minane, yaani zaidi ya nusu mwaka ukapita mpaka ikafika mwezi Desemba 2009; siku chache kuelekea 2010, si Tume ya Uchaguzi wala serikali ilikuwa imefanya kikao na vyama vya siasa kufikia makubaliano kuhusu marekebisho yanayokusudiwa.
Hata hivyo, katika mwezi wa Desemba 2009 vyombo vyote viwili; tume ya uchaguzi na serikali viliibuka na kutoa kauli zinazoashiria kwamba tayari maamuzi yameshafikiwa kuhusu suala hili nyeti linalohusu mustabali wa wananchi wote bila kujali vyama.
Ilianza Tume ya Uchaguzi ambayo Desemba mosi, 2009 ilifanya mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuelezea kile ilichokiita mkutano wa kubadilishana mawazo na kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu 2010.
Katika mkutano huo mada na hotuba zilionyesha bayana kwamba tayari yapo marekebisho ambayo tume kwa kushirikiana na serikali wameshakusudia kuyafanya; huku mabadiliko mbalimbali ya msingi yakiwa ni sehemu ya hoja zilizowasilishwa.
Siku chache baadaye Desemba 2009 11, serikali ikachapisha kwenye gazeti la serikali miswada miwili yenye kulenga kufanya marekebisho katika sheria za uchaguzi. Siku kumi baadaye serikali ikafanya kile kilichoitwa kuweka hadharani miswada hiyo miwili kupitia taarifa yake fupi kwa vyombo vya habari Desemba 21, 2009.
Serikali ilitangaza marekebisho hayo yakiwa na mapendekezo ya kufanyia marekebisho sheria ya uchaguzi sura ya 343 na sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa sura ya 292, lengo lililoelezwa kuwa ni kuondoa upungufu mbalimbali uliojitokeza katika chaguzi zilizopita kuiwezesha NEC kuendesha uchaguzi kwa ufanisi.
Serikali ikaeleza kuwa upungufu uaokusudiwa kurekebishwa katika muswada huo ni pamoja na NEC kutokuwa na madaraka ya kuteua waratibu waandikishaji wa mikoa.
Pia kushughulikia suala la kipindi cha kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura kutotajwa bayana katika sheria na sheria kutoruhusu baadhi ya watendaji wa tume kuingia katika vituo vya kupigia kura ili kufuatilia zoezi la upigaji kura.
Ibara ya 6 imependekeza marekebisho katika fungu la 15 la sheria, ili kuweka bayana kipindi cha kufanya uboreshaji wa daftari la taifa la kudumu la wapiga kura kuwa mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na unaofuata.
Aidha, sehemu hiyo inasisitiza kwamba, kwa lengo la kuongeza uwazi katika zoezi la uandikishaji wapiga kura, imependekezwa katika ibara ya 7 kuwa na fungu jipya la 15A katika sheria linatoa nafasi kwa vyama vya siasa kuteua mawakala wakaokuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura kama ilivyo wakati waupigaji kura.
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imetangaza kuwa imeandaa marekebisho ambayo imeyaita ‘makubwa’ ya sheria za uchaguzi ambayo pamoja na mambo mengine, imependekeza kupunguzwa kwa muda wa kusubiri kabla ya kufanya uteuzi wa mgombea mwingine wa nafasi ya urais au umakamu inapotokea mmoja wao anafariki kabla ya uchaguzi ambayo imejinadi kuwa yanalenga pia kuipunguzia nguvu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Ibara ya 9 inapendekeza marekebisho katika fungu la 35A la sheria kwa lengo la kupunguza muda wa kusubiri kabla ya kufanya uteuzi wa mgombea mwingine wa urais au umakamu wa rais inapotokea wagombea hao wamefariki.
Sehemu ya muswada huo wa sheria ya uchaguzi imependekeza kufutwa kwa vifungu vya sheria vinavyoruhusu utoaji wa takrima.
Muswada unapendekeza pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ipewe mamlaka ya kuteua wasimamizi wa uchaguzi kutokana na ofisi au sifa zao tofauti na ilivyo ambapo tume huteua wasimamizi wa uchaguzi kutokana na ofisi pekee.
Marekebisho hayo pia yanapendekeza kuongeza muda wa rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu, katika Mahakama ya Rufaa kwenye kesi za uchaguzi na kuongezwa kwa muda wa kufungua kesi kutoka siku 14 za sasa hadi siku 30.
Ibara ya 10 imependekeza marekekibisho katika fungu la 37 la sheria ili kuweka ukomo wa muda wa kufanya chaguzi ndogo za Bunge kama inavyobainishwa katika ibara ya 76(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977.
Katika Ibara ya 3, muswada unapendekeza kuongeza tafsiri ya maneno mbalimbali katika sheria ya uchaguzi; unapendekezwa kurekebisha tafsiri ya maneno “nomination” na “Member of Parliament” ili kujumuishwa katika tafsiri ya uteuzi (nomination) uteuzi wa wabunge wanawake wa viti maalumu na katika tafsiri ya mbunge (member of Parliament) mbunge wa kuteuliwa wa viti maalumu vya wanawake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ibara ya 13 inakusudia kufanya marekebisho katika sura ya V ya sheria kwa kuongeza sehemu mpya ya III inayohusu mchakato wa mamlaka ya tume kuwatangaza wabunge wanawake wa viti maalumu walioteuliwa na vyama vyao kuwa wabunge.
Marekebisho hayo ambayo serikali imeyapendekeza yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha Bunge hivi karibuni ili yatumike kwenye uchaguzi wa mwaka 2010.
Hata hivyo, marekebisho hayo hayajitoshelezi kabisa ukilinganisha mapungufu yaliyopo, muda uliopo, hoja za wadau na rasilimali ambazo zimetolewa na wadau mbalimbali kuwezesha mchakato wa marekebisho ya kisheria na kitaasisi nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Hivyo mjadala utakaowezesha kuunganisha nguvu za kidemokrasia na kimaadili ili kudai na kushawishi mabadiliko ya sheria za uchaguzi na mazingira ya kisiasa ni muhimu uibuliwe na kuendelezwa.
Kuna haja ya serikali kufanya marekebisho mapana zaidi au vyama vya siasa na wadau wengine waelekeze jitihada bungeni na mahakamani kudai mabadiliko ama kufutwa kwa vipengele vya sheria nyingine ambavyo vinafanya mazingira ya kisiasa na kiuchuguzi yanayokwaza uchaguzi huru na wa haki.
Kwa muhtasari lazima kuzipitia sheria na/ama kufanya mabadiliko/marekebisho ya msingi yafuatayo ambayo hayajaguswa katika miswada iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Mosi, tume lazima iwe huru na ya kudumu yenye kufanya kazi muda wote na kuwekewa bajeti maalumu na watumishi wa serikali wasitumike katika uchaguzi badala yake kuwe na watendaji huru wa tume katika ngazi zote kama ilivyo kwa mahakama.
Pili, kupanua wigo wa mfumo wa uwakilishi wa uwiano na kuweka mfumo mchanganyiko/mchanyato. Tatu; Kufuta vipengele katika sheria vinavyoruhusu mapingamizi yanayokwenda kinyume na misingi ya masharti ya kikatiba ya wagombea.
Nne, kuchunguza na kukabiliana na tatizo la mwitiko mdogo wa wapiga kura. Tano, kuhakikisha kwamba mafunzo ya pamoja yanafanywa baina ya wasimamizi/wasaidizi wa vituo na mawakala wa vyama; na kuhakikisha wgombea/vyama vinakuwa na rasilimali za kuwezesha kuwa na mawakala katika vituo.
Sita, kutoa uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo wakati wa uchaguzi; Kuweka usawa katika matumizi ya vyombo vya habari ikiwamo kuhusu matangazo ya kisiasa ya kulipia wakati wa kampeni.
Ni wazi: Sehemu kubwa ya mabadiliko haya yanahitaji kitu kimoja tu: mabadiliko ya katiba ya nchi. Hakuna uhuru na haki kwa vyama vya siasa kushiriki kwenye chaguzi zijazo kama mazingira ya kisiasa na kiuchaguzi hayatabadilika katika nchi yetu!



Imetoka: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=12317
 
Ahsante JJ,

Kwani mapendekezo ya sasa bado yanampatia mamlaka rais (wakati mwingine mwenye kiti wa chama tawala au kiongozi wa juu wa chama tawala) kuteua mwenyekiti wa tume na makamishna? Je suala la upuuzi wa kuapa ama kwa wakili au hakimu limeachwa? Na tume itaendelea kutumia watumishi wa halmashauri kusimamia uchaguzi? Uchaguzi wa mitaa utasimamiwa na tume? Samahani, maswali ni mengi ila naamini tunaweza kupata majibu toka kwa wale waliosoma hiyo rasmu ya mswada.
 
Ahsante JJ,

Kwani mapendekezo ya sasa bado yanampatia mamlaka rais (wakati mwingine mwenye kiti wa chama tawala au kiongozi wa juu wa chama tawala) kuteua mwenyekiti wa tume na makamishna? Je suala la upuuzi wa kuapa ama kwa wakili au hakimu limeachwa? Na tume itaendelea kutumia watumishi wa halmashauri kusimamia uchaguzi? Uchaguzi wa mitaa utasimamiwa na tume? Samahani, maswali ni mengi ila naamini tunaweza kupata majibu toka kwa wale waliosoma hiyo rasmu ya mswada.

Dark City

Nimeusoma muswada wote mwanzo mpaka mwisho. Hayo maswali yote uliyouliza hayajajibiwa na muswada huo, kwa maneno mengine mapendekezo hayo yote hayapo.

Muswada wa marekebisho haujagusa mambo yote hayo, jana kamati ilikuwa na public hearing. Leo wanaendelea na vikao vyao.

Ni muhimu umma ukapaza sauti zaidi kutaka marekebisho ambayo kwa kweli ndio yanayotakiwa katika sheria ya uchaguzi.

Tuendelee kujadili, kuchambua na kufikisha ujumbe kwa watawala na wabunge wetu.

JJ
 
Mnyika.. huu mswada utapita kama ulivyo; mna mpango gani? au mtaitisha waandishi wa habari kuelezea kwanini hamkufurahia wabunge wa CCM kupitisha mswada ambao wao unawasaidia?

Kwanini mnafikiria CCM itapitisha sheria ambazo zitachangia kuondolewa kwake? Yaani, mnataka papa ajiwekee mafuta na vitunguu , limau na pilipili halafu nyie mje kumkaanga?
 
Mnyika.. Kwanini mnafikiria CCM itapitisha sheria ambazo zitachangia kuondolewa kwake? Yaani, mnataka papa ajiwekee mafuta na vitunguu , limau na pilipili halafu nyie mje kumkaanga?

Hii nimeipenda sana, kumbe hata jogoo wa kienyeji inabidi umuanzishie mbio ndio uweze kumgeuza kitoweo.

Kwa maana hiyo ukweli utabaki palepale kuwa ccm hawawezi kujitengenezea mazingira ya wao kuondoka madarakani. Ni jukumu la wapinzani kuwashirikisha watanzania ipasavyo ili wakiona inafaa basi wailazimishe serikali ya ccm kukubaliana hali halisi. Haya yameonekana kwingineko, ila Tanzania nasita kusema. Kuna mikakati yoyote katika hili? au tunasubiri jaji makame atangaze matokeo yake kumfurahisha mwajiri wake?
 
Kwanini mnafikiria CCM itapitisha sheria ambazo zitachangia kuondolewa kwake? Yaani, mnataka papa ajiwekee mafuta na vitunguu , limau na pilipili halafu nyie mje kumkaanga?
hilo ndilo tatizo la siasa na wanasiasa wenzangu wa kambi ya upinzanii, kweli tunapenda siasa laini, hatupendi kulipa gharama kwaajili ya vizazi vijavyo, Upinzani wa Tanzania umejaa makapi ya CCM, hawa kina Cheyo, Mrema , Chipaka wanajiona kama sehemu ya CCM, CCM masalia.
Kweli tunahitaji wanasiasa wanaharakati walio tayari kushiriki siasa hata kukubali kwenda jela ama kupoteza maisha kwa ajili ya ukombozi wetu, angalia walivyokufa kina Malcom X, Martin Luther King JR, Didan KIMATH, Mungu azilaze roho zao mahala pema peponi, angalia walivytofungwa kina Raila Odinga, Nelson Mandela...na wengine wa kariba hiyo, hii yote ili kuwatoa watu wao katika lindi la ukandamizwaji.
 
Inavyoonekana si Tume ya uchaguzi wala serikali iliyo na nia ya kufanyia mabadiliko sheria ili ziendane na matakwa ya wengi na chaguzi ziwe huru na za haki.

Kama ulivyosema toka baada ya uchaguzi wa 2005 ni mara moja tu Tume imekutana na wadau wake wakubwa ambao ni vyama vya siasa inasikitisha, na nina uhakika haya mapendekezo yaliyotolewa yatapitishwa na bunge lijalo.

Ni kweli kuna juhudi zingine zinaonekana kama NCCR kufungua kesi kudai tume huru na vilevile tunaona CUF wanavyohangaika kwa balozi mbalimbali za nje kuhusiana na mambo ya uchaguzi Zanzibar lakini huku bara hatuoni hilo.

Sasa nyie kama chama/vyama ukiondoa niliyoyataja mna mkakati gani mwingine unaoonekana na usioonekana kama ni kufanya maandamano ya kupinga mswada au kupiga kelele kwa jumuia za kimataifa kuelezea matakwa yenu.
 
Kwa kile nimechoka binafsi na malalamiko ya mipango ya CCM na kutuonesha kile ambacho CCM wanapanga kufanya... sijaona kama wapinzani wanachukizwa kweli na mambo hayo. Inaonekana wameamua to function within and with the corrupt sysytem hoping for the best outcome.
 
ni kweli tanzania itakuja kukombolewa siku ambayo uchaguzi wetu utakuwa wa uhuru na haki.mie naona viongozi(na wabunge) wengi hawajitumi kwenye kuletea taifa maendeleo kwa vile wanajua siku uchaguzi ukifika wana njia ya kununua ushindi.nchi nyingi zenye demokrasia zimeweza kuendelea kwa vile viongozi wao wanawajibishwa kutokana na kazi waliofanyia wapiga kura na hapo ndio wanaongezewa mda kwa kupigiwa kura tena na kama hakuna kitu alichofanya basi huwa hapewi kura na wananchi.lakini tofauti nchini kwetu tuna wabunge hamna kitu chochote wanakifanya cha ajabu wako bungeni miaka nenda rudi na kinachowafanya kuwepo siokwamba ni wachapa kazi hapana ,kinachowafanya waendelee kuwepo ni kwa vile wanunuzi wa zuri wa kura kupitia uchaguzi wetu ambao ni mbovu .


tukiweza kupeleka nguvu kwenye kufanikisha uchaguzi wa haki na uhuru basi wananchi tutaweza kuona nguvu ya kura yetu.kama tutaendelea kuwa na uchaguzi huu wa sasa basi hatutapiga hatua yoyote kwani tutakuwa tunaendelea kuongozwa na watu wanaojali maslahi yao na sio ya nchi.
 
Mnyika.. huu mswada utapita kama ulivyo; mna mpango gani? au mtaitisha waandishi wa habari kuelezea kwanini hamkufurahia wabunge wa CCM kupitisha mswada ambao wao unawasaidia?

Kwanini mnafikiria CCM itapitisha sheria ambazo zitachangia kuondolewa kwake? Yaani, mnataka papa ajiwekee mafuta na vitunguu , limau na pilipili halafu nyie mje kumkaanga?


Mwanakijiji

Asante kwa maswali yako ambayo yanabeba dhana kweli kwamba ni rahisi kwamba ‘ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko CCM kufanya marekebisho ya kikatiba na kisheria kuweka uwanja sawa wa kisiasa wenye uchaguzi huru na haki”

“CCM haiwezi kukata mkono unaoilisha”; mfumo wa utawala ulioko madarakani unaendelea kuwepo kutokana na katiba, na sheria kutokuwa na misingi thabiti yenye kuvipa uhuru vyombo vya uwajibikaji. Lakini kubwa zaidi ni kuwa kutokuwa na uchaguzi huru na haki ndio kunakoweka madarakani viongozi mafisadi ama viongozi wasio na uthubutu na uthabiti wa kuchukua hatua. Hivyo, CCM inatambua wazi kwamba kwa kuweka uchaguzi huru na haki, mfumo huu wa utawala utaondolewa madarakani; hivyo kubadili sheria ya uchaguzi na kuweka sheria nzuri ni sawa na kukata mkono unaowalisha.

Katika muktadha huo, swali ulilouliza ni kuwa upinzani tuna mpango gani? Je, tuna mpango wa kuendelea kulialia na kulalamika kwa kufanya mikutano ya hadhara baada ya sheria kupitishwa?

Niseme kwa ujumla kwamba mwelekeo wa sasa ni kuchukua hatua badala ya kulalamika, ndio maana umeona binafsi nimelishikia bango suala hili kabla ya sheria kupitishwa.

Lakini ni wazi kwamba tupo kwenye mtanziko(dilemma). Kuna mitazamo miwili ndani yetu:

Mosi, wapo wenye mtizamo kwamba iwapo marekebisho ya msingi hayatafanyika basi tuchukue msimamo wa kususia uchaguzi. Hofu juu ya uamuzi huu ni kuwa kama vyama vikuu vya upinzani vitasusia uchaguzi, vipo vyama mamluki vitashiriki nap engine hata vinaweza kupewa viti vya ushindi baadhi kama mapambo (cosmetic). Hali hii itakuwa na athari ya kupoteza uwakilishi wa kwenye vyombo vya maamuzi wa vyama vikubwa vya upinzani na kupunguza sauti ambayo imekuwa ikisikika hivi sasa ya kuiwajibisha serikali, hii itakuwa na taathira kwenye uthabiti wa vyama kwa umma pia. Katika mazingira hayo, kunaweza kusiwe na athari kwenye marekebisho ya uwanja wa kisiasa na kiuchaguzi na hivyo kufanya mkakati mzima kuwa sawa na ‘kuwasusia mafisi bucha’.

Pili, wapo wenye mtizamo kwamba cha msingi ni kuunganisha nguvu ya umma kuchochea marekebisho hayo. Kama CCM na serikali watagoma basi iwe ni ajenda ya uchaguzi, kwamba mkituchagua wapinzani tutabadili katiba na sheria kuweka mifumo ya uwajibikaji, uwanja sawa wa kisiasa na kuruhusu uchaguzi huru na haki. Na kuamsha umma kuhakikisha wagombea wanashinda pamoja na kuwa Tume ni yao na sheria ni mbovu kama walivyoshinda Karatu, Pemba nk. Hofu ya mkakati huu ni kuwa ushindi katika mazingira haya utapatikana pale tu ambapo wananchi wamefikia hatua ya uasi wa kiraia(civil disobedience), lakini pale kwenye ushindani wa kawaida haitawezekana kushinda hata kama unakubalika. Kwa ujumla, katika mazingira ya ushindani wa namna hii unaohusisha uasi wa umma, uchaguzi unaweza ukawa chanzo za vurugu na umwagaji damu wa namna mbalimbali kwa kadiri utawala wa sheria na haki za binadamu zinavyopuuzwa; haya yameoneka Pemba, Kiteto, Tarime, Busanda, Biharamulo.

Kwa hiyo ni msimamo upi wa kuchukua na mpango upi wa kutekeleza; itategemea tathmini ya kina ya mitazamo hiyo hapo miwili.

Kwa maoni yangu, hiyo ni hatua ya baadaye kidogo. Lengo langu la kuibua mjadala huu hivi sasa ni tuanze na hatua ya msingi ambazo ni kuunganisha nguvu za pamoja kushinikiza marekebisho yanayokusudiwa. Changamoto ya msingi ni kwamba suala hili kwa sasa linatazamwa kama vile ni suala la wapinzani, badala ya kutazamwa kwamba ni hitaji la umma kwa kuwa linahusu uchaguzi ambao watanzania wote watapiga kura lakini linahusu kuchagua viongozi wa kutumikia watu wote. Hivyo, baadala ya kuuliza wapinzani mna mpango gani, ni vizuri mwanakijiji ukauliza; watanzania tuna mpango gani?

Nimesoma makala yako Tanzania Daima ya jana, usizungumzia kuhusu unabii wa kwamba CCM itaanguka na kwamba baadhi yao watahama. Ni muhimu kwa wanaCCM wanaokusudia kuhama chama hicho, na wachambuzi wao wakajua kwamba wakipitisha marekebisho hovyo hovyo ya sheria ya uchaguzi, ni marekebisho hayo hayo yatatumia na chama dola kuwasulubu nje ya chama hicho. Ni vizuri pia kwa wanaCCM wanaobaki, wanaojiita majemedari wa vita dhidi ya ufisadi, wakajua kuwa kupitisha sheria ya uchaguzi inayolinda ufisadi na kuweka mianya ya matumizi mabaya ya madaraka kwa watendaji walioteuliwa na serikali kuu kusimamia uchaguzi, ni watendaji hao hao ambao watawahujumu kwenye uchaguzi.

Hivyo ni muhimu kwa wachambuzi, wanahabari, wanaharakati, wanataaluma, viongozi wa dini na watanzania kwa ujumla kutambua kwamba suala la kuweka uwanja sawa wa kisiasa wenye kuwezesha uchaguzi huru na haki si hitaji la wapinzani pekee, litazamwe kama tunu ya kitaifa kama sehemu ya kulinda amani na kuchochea uongozi bora utakaosimamia maendeleo ya wote. Jiulize; wewe umefanya nini kuitetea tunu hii? Nini utafanya iwapo CCM itaipuuza sauti yako na kupitisha sheria mbovu na marekebisho kedekede lakini legelege?

JJ
 
Mnyika.. u guys are too much elitist! You are trying too much to look at political issues through a prism of intellectual quandary! You are looking at the political options you have and you don't want to be seen as political activists who match on the streets and get pushed over and chased by police or even get arrested for "disorderly conduct" like hooligans!

It seems the moden Tanzanian opposition leader despise those political tools used by Gandhi, Martin Luther and Ms. Wangari to bring political change in their respective countries. The Tanzania opposition is more interested in making a rational argument of why change is good and why CCM must bring this change after being persuaded through logical and intellectual arguments.

Unfortunately, this can not work and will never work.

What you guys are doing is like the proverbial hyena walking behind a man hoping that by an act of God or by mere chance or even by persuasion the human hand will fall off! This will probably even call for a press conference to explain to the media why the human hand is tasty and why humans should consider creating better environment for hyenas and other animals to enjoy their "meals"..

The same can not be said about a tiger, cheetah, or a lion who is hungry!
 
Back
Top Bottom