Mapendekezo ya muundo wa baraza la mawaziri - 2010-2015

40 kuunda baraza jipya la mawaziri
Sunday, 21 November 2010 21:29

kikwete-kuapishwa.jpg
Rais Jakaya Kikwete ambaye siku za hivi karibuni anatarajiwa kutangaza baraza jipya la mawaziri ambalo amedai litakuwa na wamtu waadilifu na wachapakakzi

Sadick Mtulya
BARAZA jipya la mawaziri linalotarajiwa kutangazwa wiki hii na Rais Jakaya Kikwete linatarajiwa kuwa na mawaziri kati ya 40 na 45, kati yao 23 wakiwa ni mawaziri kamili.Kwa maana hiyo, baraza hilo litakuwa na wizara 23 tu, Mwananchi imedokezwa.Habari ambazo Mwananchin imezipata zinaeleza kuwa katika baraza hilo jipya, ambalo litakuwa la tatu kwa Rais Kikwete tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, waliokuwa manaibu waziri watano katika baraza lililopita, watapandishwa na kuwa mawaziri kamili.

Vyanzo vyetu vya kuaminika vimeeleza kuwa idadi ya mawaziri wanawake itaongezeka kulinganishwa na baraza lililopita na kwamba uteuzi umezingatia umri, uzoefu pamoja na uwiano wa mikoa.Pamoja na kuwepo kwa sura mpya, idadi kubwa ya waliotajwa katika baraza hilo ni wanasiasa wakongwe ambao wengi wao walikuwamo katika baraza lililopita.
Chanzo chetu kimeeleza kuwa Rais Kikwete amekataa kuwapa nafasi ya uwaziri wabunge waliopata ushindi kwa kura chache katika uchaguzi mkuu uliopita.
Miongoni mwa wabunge waliokuwa manaibu kwenye baraza lililopita ni Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Adamu Malima (Mkuranga) aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Christopher Chiza (Buyungu) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji.
Wengine ni Dk David Mathayo (Same Magharibi) aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika pamoja na Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini) aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.

Habari hizo zinasema kuwa Wizara ya Fedha na Uchumi itaendelea kuwa na manaibu waziri wawili kama ilivyokuwa katika ngwe ya kwanza ya miaka mitano ya serikali ya Rais Kikwete.
Mbali na wabunge 27 waliotajwa na gazeti hili jana wengine ambao wametajwa kuwemo kwenye serikali mpya ya Rais Kikwete ni Muhammed Seif Khatibu kutoka Jimbo la Uzini ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Stephen Wasira(Bunda) aliyekuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, na Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini) aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma.

Wengine ni Mustapha Mkulo (Kilosa) aliyekuwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mathias Chikawe (Nachingwea) aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria pamoja na Aggrey Mwanri (Siha) aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi).
Wengine ni Bernard Membe (Mtama) ambaye katika serikali iliyopita alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa na Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mawaziri wengine waliokuwa katika Serikali iliyopita wanaotajwa kurejeshwa katika kipindi hiki cha mwisho cha utawala wa Kikwete ni Ezikeil Maige (Msalala) ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, William Ngeleja (Sengerema) aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, na Celina Kombani (Ulanga Mashariki) ambaye alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi),
Wengine ni Profesa Juma Kapuya (Urambo Magharibi), aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, Profesa Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), ambaye alikuwa Waziri Maji na Umwagiliaji, Dk Hussein Mwinyi (Kwahani), aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Shukuru Kawambwa (Bagamoyo), aliyekuwa Waziri wa Miundombinu na John Magufuli (Chato) ambaye alikuwa Waziri wa Maendeleo Mifugo na Uvuvi.

Wabunge wanaotajwa kuingia katika baraza la mawaziri kwa mara ya kwanza ni Anna Tibaijuka (Muleba Kusini), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na ambaye alikuwa spika wa Bunge la Tisa, Dk Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Kilango (Same Mashariki).
Wengine ni Januari Makamba (Bumbuli) ambaye alikuwa msaidizi wa rais katika awamu ya kwanza ya utawala wa Rais Kikwete, Salehe Pamba (Pangani), Steven Masele (Shinyanga Mjini), Gerson Lwenge (Njombe Magharibi) na Nyambari Nyangwine (Tarime).

Wengine ni Shamsi Vuai Nahodha (mbunge kuteuliwa) na alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Angela Mkwizu (Viti Maalum) na Amos Makala (Mvomelo) ambaye ni Mweka Hazina wa CCM, Said Bwanamdogo (Chalinze), Lazaro Nyarandu (Singinda Kaskazini) na Zakia Meghji (wa kuteuliwa).
Chanzo hicho kimebainisha kuwa Rais Kikwete amedhamiria kuunda baraza dogo la mawaziri litakalo kuwa na tija ikilinganishwa na alilounda wakati akiingia madarakani mwaka 2005, ambalo lilikuwa na mawaziri wapatao 60 na ambalo alilivunja Februari 2008 baada ya Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu.

Lowassa alijiuzulu kutokana na kashfa ya zabuni tata ya ufuaji umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond.
Hata hivyo, baraza jipya aliloliunda baadaye chini ya Waziri Mkuu mpya, Mizengo Pinda lilikuwa na mawaziri 27 na manaibu mawaziri 21.
Kati ya mawaziri ambao hawatarajiwi kurejea kwenye baraza jipya ni wale walioanguka katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM na wengine waliangushwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu.
Akilihutubia Bunge Alhamisi iliyopita, Kikwete alidokeza kuunda serikali itakayokuwa na watu waadilifu, makini na wachapakazi hodari.
Pia alisema ataunda serikali ya watu wachache ambao wataondoa urasimu watakaokuwa karibu na wananchi na kushirikiana vizuri na wabunge wote bila kujali vyama vya siasa wanavyotoka.
Source: Mwananchi.

Mbona hili baraza halia tofauti na baraza lililopita, au ni hisia za mwandishi wa habari hii.
 
Kwa idadi ya ukubwa ambayo ni 40 sio mbaya, kwani lililopita walikuwa 60. Hii itatupunguzia matumizi ya serikali.
 
Mimi hata sina matumaini na hilo baraza jipya.
Sijui safari hii watapelekwa hotel gani ya kifahari kupewa semina ya jinsi ya kufisadi!
 
Wizara ya maji na umwagiliaji NA Wizara ya kilimo, chakula na ushirika!! seems the same thng to me...changanya zote..!!
 
Wiki hii mkulu anatarajiwa kutaja baraza la mawaziri wasiopungua 40 au chini ya hapo (si unajua anadesa sera za CHADEMA) sasa katika dodosa dodosa yangu natabiri wafuatao kuwepo katika baraz hilo...MAGUFULI...NISHATI NA MADINI, ADVOCATE RWEIKIZA...KATIBA NA SHERIA, SITA...MALIASILLI NA UTALII, MEMBE....MAMBO YA NJE, LOWASSA....MIFUGOLowasa-TAMISEMI, Rostam-fedha, Meghji-maliasili, Magufuli-samaki, Ngeleja-nishati na madini, Sitta-Africa mashariki, Membe-mambo ya nje, Ngeleja-mambo ya ndani, Kilango-wanawake, jinsi na watoto, RZ1, Janu........

JE wewe unatabiri au una hisi mkuu atawataja kina nani kuwa mawaziri???
 
Kuna kila taarifa za uhakika kuwa mbio za kusaka ulaji wa wizara zinakamilika saa mbili na nusu kuanzia sasa. Wateule mlioenda mlingotini kuomba dua sasa tazameni juu mngojee kulia ama kucheka.
 
Chomeka CCTVdom ikulu nadhani wapo wadau watupe data sahihi. Au Mheshimiwa anatembea na list kwenye porch? ITAJULIKANA TUU!
 
mhh lazima nimo kwenye hiyo listi maana nimeroga vibaya sanaaaaa
 
Kama Rais ni yuleyule na WATEULE wake ni WALEWALE ilimradi hakuna chombo wala taasisi yenye kuhoji uteuzi huu. Huku kuchelewachelewa ni geresha tu na kuwaonyesha wateule wake nguvu alizonazo juu yao.
 
we chezo hujaloga kama mimi, nimeenda zaire lazima anipe wizara ya maliasili
 
akipewa mtu mwingine hiyo wizara yangu lazima nimtoe mtu busha,teh teh....................
 
Nalingojea na redio yangu pembeni nikitarajia baraza dogo lenye watu wenye ujuzi na uwajibikaji bila kusahau baraza dogo lenye mawaziri wachache...............
 
Attachments

  • blw.jpg
    blw.jpg
    38.4 KB · Views: 48
Ile wizara aloowahi kushika Kingunge enzi za Mkapa hairudi kweli? Maana CHADEMA wamewakalia vibaya hawa jamaa.
 
Back
Top Bottom