Mapendekezo katiba mpya: Tunahitaji makamu wa rais?

wakurugenzi wa halmashauri unawadhibiti vipi kwa wizi na ubadhirifu?
maana waliopo sasa karibu wote ni majambazi wakubwa..
Tunapojadili katiba mpya maana yake ni kwamba tunataka kubadili mifumo ya utawala, kwahiyo swala la kuwadhibiti linawezekana na liko ndani ya uwezo wetu, hakuna mtu anaezaliwa akiwa mbadhirifu, hawa wakurugenzi wote kabla ya kupewa ajila serikalini semina elekezi inatakiwa iwe China, wakirudi kutoka kule China na wakakuta hapa katika mfumo wetu wa sheria tume endorse vifungu vile wanavyovitumia Wachina kwa wabadhirifu na wala rushwa hatutokuwa natabu kuhusu wabadhirifu, Nyerere alifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu alimaanisha kwa vitendo kwamba rushwa ni adui wa haki.
 
semina elkezi iwe China?
you are not serious....
 
semina elkezi iwe China?
you are not serious....
Niko serious,.....
Namaanisha kwamba wachina walikuwa wako Third wolrd kama sisi lakini baada ya kuweka mifumo ya sheria inayochukia aina yoyote ya ufisadi wenzetu wamefanikiwa kwa haraka kufikia hapo walipo.
Semina za Ngurdoto hazina tija, hawa wateule wakifika kule na kukuta ni watumishi wangapi wa umma wamenyongwa kwa makosa ya ufisadi na huku wakijuwa hiyo sheria na kwetu imeingizwa hakuna ambaye atatamani ufisadi.
 
hapa tunajadili katiba
na vipengele vya kuwekwa humo
hilo la china huwezi weka kwenye katiba..
sanasana ni utashi wa mtu tu..

kuhusu kunyongwa watu
zama hizi za 'haki za binadamu pia sio rahisi'
actually kuna rushwa zaidi China kuliko
DENMARK NA Sweden...sasa jiulize kama kunyonga ndo dawa
 
Mie nataka ndani ya Katiba mpya kuwepo na kipengele ambacho kitaruhusu Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kama Bunge haliridhiki na utendaji wake. Tungekuwa na kipengele kama hiki labda Kikwete tungekuwa tumemshasahau miaka mingi iliyopita.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mawazo mazuri hayo Billy. Mimi naunga mkono kundokana na waziri mkuu na kubakiza makamu wa raisi tu.
 
System ya utawala wa Tanzania inachanganya baadhi wa watu. Wengi wanadhani hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa na muungano lakini sidhani kama ni hivyo. On one hand tunaweza kusema tunafuata presidential system ambapo kunakuwa Rais na Makamu wa Rais. On other hand, tuna Primie Minister ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali bungeni. Hapa itaonekama kama vile tunafuta parliamentary system. However, interestingly, japokuwa bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Prime Minister bado anaonekana yupo more accountable to the President.

Ukiwauliza watu tunafuata system gani ya utawala, wengi watasema ni presidential system. Lakini ukiangalia kwa undani tunafuata semi-presidential system ambapo Rais na Prime Minister wote ni wahusika wakuu in the day-to-day administration of the State wakati Vice President yupo yupo tuu. Bado sijaelewa ilikuwa vipi mpaka tukawa na semi-presidential system kwa sababu mara nyingi semi-presidential system inatokea pale ambapo Rais na Prime Minister wanatoka vyama tofauti. Kwa mfano, Kenya walikuwa na post ya Prime Minister lakini wakai-abolish mwaka 1964 kabla ya kuirudisha tena kwaka 2008 due to the power sharing agreement between political parties.

Semi-presidential system au kwa jina lingine "cohabitation" ni effective katika check and balance au wakati ambao kuna "bitter and tense stonewalling" kati ya Rais and Prime Minister hasa pale wanapotoka vyama tofauti. Kwa upande wa Tanzania, sidhani kama haya yatatokea kwa sababu Rais na Prime Minister wanatoka chama kimoja. Na unapokuwa na Prime Minister kama Pinda ndio kabisaaa.

Sidhani kama watawala wetu watakubali kufuata parliamentary system ili wawe more accountable to the parliament. Parliamentary system ingetufanya tu-abolish cheo cha Urais and Makamu wa Rais na kubakia na Prime Minister na Deputy Prime Minister kama Uingereza. So, kilichobakia ni either kuendelea na semi-presidential system au kuwa na full presidential system. Kama tukiwa na full presidential system, inabidi cheo cha Prime Minister kifutwe na kubakia na President and Makamu wa Rais. Prime Minister ndie anayefanya cheo cha Vice President kiionekane obsolete.

Personally, naunga mkono kufutwa kwa cheo cha Waziri Mkuu na kubakia na cheo cha Makamu wa Rais. BTW, Pinda si alishasema hatarudi tena serikalini baada ya uchaguzi ujao kama CCM ikishinda? Kwa nini tusitumie hii opportunity kufuta hiki cheo once and for all hadi tutakapokuwa serikali ya mseto kama Kenya?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
- Wakati umefika wa kupunguza msururu wa Viongozi wa juu, na hasa gharama za kuwatunza waki-retire, I mean people naomba kuuliza hivi kweli tunawahitaji Waziri Mkuu na Makamu wa Rais katika Serikali yetu? kwa maoni yangu one has to go kwenye katiba mpya na hasa Makamu wa Rais, kama ni muhimu kuwa naye basi Waziri Mkuu ashike hiyo nafasi kama zamani.

- The idea kwamba hata Visiwani kunakuwa na Makamu wa Rais, tena wawili it does not make a sense at all, wanafanya nini? Hivi vinakuwa ni vyeo vya huruma tu, under whose expense? kodi yetu wananchi wakati ni sasa kwenye katiba mpya kuondokana na na huu msururu wa Viongozi wa juu, tuwe na huruma kwa Walalahoi kidogo jamani!

MUCH RESPECT PEOPLEs!

William @..NYC, USA: Mutuz Le Baharia!

Kwenye Muswada wa kuunda Tume ya Kukusanya maoni, 2011 imetamkwa kwamba ni marufuku kujadili juu ya mihimili 3 ya dola yaani Serikali (utawala), Mahakama na Bunge. Sasa hii hoja yako itaingiaje kwenye kubadili Katiba mpya?
Jua kuwa CCM wameshaweka mazingira ya kuunda katiba ya kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani! Kwa hiyo ukijifanya unatoa maoni huku umeelekezwa vitu vya kujadili na kuacha hayo sio maoni huru!
 
Mie nataka ndani ya Katiba mpya kuwepo na kipengele ambacho kitaruhusu Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kama Bunge haliridhiki na utendaji wake. Tungekuwa na kipengele kama hiki labda Kikwete tungekuwa tumemshasahau miaka mingi iliyopita.
Watanzania wengi hawaijui katiba ya sasa. Kumbe hata wewe BAK uu miongoni mwao?!. Kipengele cha Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, kipo!.
 
System ya utawala wa Tanzania inachanganya baadhi wa watu. Wengi wanadhani hii imesababishwa kwa kiasi kikubwa na muungano lakini sidhani kama ni hivyo. On one hand tunaweza kusema tunafuata presidential system ambapo kunakuwa Rais na Makamu wa Rais. On other hand, tuna Primie Minister ambaye ni kiongozi mkuu wa serikali bungeni. Hapa itaonekama kama vile tunafuta parliamentary system. However, interestingly, japokuwa bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Prime Minister bado anaonekana yupo more accountable to the President.

Ukiwauliza watu tunafuata system gani ya utawala, wengi watasema ni presidential system. Lakini ukiangalia kwa undani tunafuata semi-presidential system ambapo Rais na Prime Minister wote ni wahusika wakuu in the day-to-day administration of the State wakati Vice President yupo yupo tuu. Bado sijaelewa ilikuwa vipi mpaka tukawa na semi-presidential system kwa sababu mara nyingi semi-presidential system inatokea pale ambapo Rais na Prime Minister wanatoka vyama tofauti. Kwa mfano, Kenya walikuwa na post ya Prime Minister lakini wakai-abolish mwaka 1964 kabla ya kuirudisha tena kwaka 2008 due to the power sharing agreement between political parties.

Semi-presidential system au kwa jina lingine "cohabitation" ni effective katika check and balance au wakati ambao kuna "bitter and tense stonewalling" kati ya Rais and Prime Minister hasa pale wanapotoka vyama tofauti. Kwa upande wa Tanzania, sidhani kama haya yatatokea kwa sababu Rais na Prime Minister wanatoka chama kimoja. Na unapokuwa na Prime Minister kama Pinda ndio kabisaaa.

Sidhani kama watawala wetu watakubali kufuata parliamentary system ili wawe more accountable to the parliament. Parliamentary system ingetufanya tu-abolish cheo cha Urais and Makamu wa Rais na kubakia na Prime Minister na Deputy Prime Minister kama Uingereza. So, kilichobakia ni either kuendelea na semi-presidential system au kuwa na full presidential system. Kama tukiwa na full presidential system, inabidi cheo cha Prime Minister kifutwe na kubakia na President and Makamu wa Rais. Prime Minister ndie anayefanya cheo cha Vice President kiionekane obsolete.

Personally, naunga mkono kufutwa kwa cheo cha Waziri Mkuu na kubakia na cheo cha Makamu wa Rais. BTW, Pinda si alishasema hatarudi tena serikalini baada ya uchaguzi ujao kama CCM ikishinda? Kwa nini tusitumie hii opportunity kufuta hiki cheo once and for all hadi tutakapokuwa serikali ya mseto kama Kenya?

Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuu wa Nchi awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Muungano liwe ni kama upper house ambapo litakuwa na wajumbe sio zaidi ya 100 watakaochaguliwa na kila mkoa (kila mkoa wabunge 2 na idadi inayobakia wanatokana na uwiano wa kura). Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano anakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano.

Nadhani mfumo huu utahakikisha muungano wa Serikali 3 bila kuathiri muungano, utaongeza uwajibikaji kwani Serikali za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na Executive PMs na watawajibika moja kwa moja Bungeni, tutaepuka kuwa na marais 3 (Rais wa muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar). Migogoro yeyote itakayotokea kuhusu muungano itakuwa resolved na Baraza la Muungano ambao litakuwa na wawakilishi wa pande zote mbili.
So Presidential system at Union level, Parliamentary system at States levels. Unaonaje pendekezo hilo
 
@ Zitto, mawazo ya mfumo ulioupendekeza ni mzuri , je mfumo huu unaweza kushabihiana vipi na resources za pande mbili za muungano? how should the resources of both territories being shared relevant to the proposed state union system?
 
Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuu wa Nchi awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Muungano liwe ni kama upper house ambapo litakuwa na wajumbe sio zaidi ya 100 watakaochaguliwa na kila mkoa (kila mkoa wabunge 2 na idadi inayobakia wanatokana na uwiano wa kura). Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano anakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano.

Nadhani mfumo huu utahakikisha muungano wa Serikali 3 bila kuathiri muungano, utaongeza uwajibikaji kwani Serikali za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na Executive PMs na watawajibika moja kwa moja Bungeni, tutaepuka kuwa na marais 3 (Rais wa muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar). Migogoro yeyote itakayotokea kuhusu muungano itakuwa resolved na Baraza la Muungano ambao litakuwa na wawakilishi wa pande zote mbili.
So Presidential system at Union level, Parliamentary system at States levels. Unaonaje pendekezo hilo

Naunga mkono hoja isipokuwa kwenye kipengele cha makamu wa rais. Bado napendekeza makamu wa rais afutwe. Napendekeza mfumo ambao unamtaka rais kuingia bungeni na kujibu hoja za serikali yake. Rais ambaye yupo tu ikulu, hahojiwi popote anajisahau na mwisho ni kujijengea kiburi kama JK!
 
Watanzania wengi hawaijui katiba ya sasa. Kumbe hata wewe BAK uu miongoni mwao?!. Kipengele cha Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais, kipo!.

Pasco,

Nimekusoma mara nyingi lakini naomba niseme kitu kimoja. Sometimes, huwa unapotosha sana kwa ku-cite a wrong law. Kama hapa unajaribu kupotosha kuwa kwenye Katiba kuna ibara inayowezesha Bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais. That is not true. Kama hiyo ibara ipo, tuwekee hapa tafadhali. Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu lakini sio Rais. Insted, Bunge linaweza kupitisha tuu azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais.

Nafikiri utakuwa ni mmoja wa wale wachache ambao mnashindwa kutofautisha kati ya vote of no confidence na impeachment. The two phrases mean different things. Impeachment implies that a crime has been committed by the President whilst a vote of no confidence does not imply that the person under vote has committed a crime.

Kwa hiyo BAK yuko right kabisa kutaka kuwepo kwa kipengele cha kutokuwa na imani na Rais kwenye Katiba mpya kwa sababu hakuna kipengele kama hicho kwenye Katiba ya sasa.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Tatizo liko kwenye muundo wa muungano. Kama muungano utabakia kama ulivyo sasa (serikali 2) hatuwezi kukwepa Makamu wa rais kwa sababu nafasi hii ni ya kisiasa zaidi na inalenga kuweka 'balance'.Ki-ukweli ni ceremonial post lakini ipo kwa sababu za kisiasa.

Hofu yangu ni kwenye muswada wa sasa. Ukisoma ukisoma vizuri huu muswada wa katiba mpya kuna uwezekano tukaendelea na mfumo wa sasa!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Unaonaje katika Katiba mpya tuwe na Parliamentary system kwa Zanzibar and Tanganyika governments and Presidential system kwa Union Government? Kwa hiyo Mkuu wa Serikali ya Tanganyika awe Waziri Mkuu na atokane na chama chenye Wajumbe wengi katika Baraza la Wawakilishi Tanganyika, Mkuu wa Serikali ya Zanzibar awe Waziri Mkuu wa Zanzibar na atokane na chama chenye Wawakilishi wengi katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mkuu wa Nchi awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la Muungano liwe ni kama upper house ambapo litakuwa na wajumbe sio zaidi ya 100 watakaochaguliwa na kila mkoa (kila mkoa wabunge 2 na idadi inayobakia wanatokana na uwiano wa kura). Mkuu wa shughuli za Serikali ya Muungano katika Bunge la Muungano anakuwa ni Makamu wa Rais wa Muungano.

Nadhani mfumo huu utahakikisha muungano wa Serikali 3 bila kuathiri muungano, utaongeza uwajibikaji kwani Serikali za Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na Executive PMs na watawajibika moja kwa moja Bungeni, tutaepuka kuwa na marais 3 (Rais wa muungano, Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar). Migogoro yeyote itakayotokea kuhusu muungano itakuwa resolved na Baraza la Muungano ambao litakuwa na wawakilishi wa pande zote mbili.
So Presidential system at Union level, Parliamentary system at States levels. Unaonaje pendekezo hilo

Zitto, nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa hasa suggestion yako ya kuwa na 'Parliamentary system' Hii hoja inaweza kuuzika zaidi
upande wa Tanganyika kuliko Zanzibar. Itabidi ifanyike kazi ya ziada kuwashawishi wajumbe wa baraza la wawakilishi wakubali hili.

Faida ninazoona kwenye huu mfumo wa parliamentary ni kuwa na 'National leadership' a point of reference na ambayo is beyond party-politics.Lazima tuwe na mfumo wa ku-safe guide country. Kwa mtazamo wangu Tanzania hatuna Rais kwa maana kiongozi wa kitaifa, tuna rais kwa maana ya kiongozi wa chama cha siasa.Katika hali hii nafasi ya Waziri mkuu inakuwa haina maana hata kidogo kwa sababu yeye ni mteule wa Rais! Ni hivi, Mkuu wa shughuli za kila siku za serikali ni Waziri mkuu, na huyu waziri mkuu anawajibika kwa rais, na rais (kwa hali ya sasa) anawajibika kwenye chama chake! Hapa tuna kiongozi wa kitaifa? Tanzania wanatakiwa waachane na hii governance structure ya kichina. Inafanya kazi vizuri China lakini sio hapa Tanzania.

Now, hoja ya uwepo wa upper house ni nzuri sana lakini ni muhimu sana kwa wabunge wote kupatikana kwa mfumo wa kura. Tusiruhusu hata kidogo kurudia makosa ya wabunge wa kuteuliwa. Ni lazima kila mbunge awe na pressure toka wananchi. Bunge la sasa lina wabunge takribani 30% wa kuteuliwa (viti maalum) na CCM ndio wanafaidika zaidi na huu mfumo. Wabunge hawa wanawajibika kwa chama cha siasa maana ndio mwaajiri wao! Kwa hiyo hata kama jambo ni jema kwa watanzania wengi lakini chama chake kinasema vingine wabunge hao watafanya kama chama kinavyoagiza. Nchi inatelekezwa kwa sababu za kisiasa.
Wabunge wote lazima wapitie sanduku la kura. Hakuna cha salia mtume.hakuna!
 
Mi nafikiri cha msingi ni kuwa na rais na makmu wake basi....nafaciya waziri mkuuinaweza kufutwa kama ilivyo kwa kenya, na mawaziri wote kuwa responsible kwa president, na kuna umuhimu wa nafaci za wizara kutajwa kwenye katiba sio kila rais anakuja na zake
 
...naomba niseme kitu kimoja. Sometimes, huwa unapotosha sana kwa ku-cite a wrong law. ...Impeachment implies that a crime has been committed by the President
Mkubwa, na wewe pia unachemka.

Impeachment does not necessarily "imply that a crime has been committed by the President." Angalia articles of impeachment kwenye katiba uone ni vitu gani vitatu vinavyoweza kutumika kuleta mashitaka bungeni.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom