Mapato ya mbunge wa bunge la Tanzania kabla ya kujiongezea posho

Inabidi soooote tugombee ubunge.

Lakini utauweza unafiki? Utawaahidi wananchi wakupigie kura baadae utashindwa kuwatimizia.

Yapasa tujifunze DIRECT DEMOCRACY na tuache REPRESENTATION.
 
Hata mama yetu makinda hajajenga sijui miaka yote 17 alikjuwa anakula gudtym tu au?
 
Hakika inasikitisha kuona wasinziaji bungeni wanalipwa kiasi hicho cha fedha wakati wakeshaji mahospitalini, shuleni, viwandani, n.k. wanalipwa viposho kiduchu na kucheleweshewe malipo yao.
 
1.Mshahara kwa mwezi tshs 2,300,000/=
2.Mafuta ya gari kwa mwezi 2,000,000/=i.e ltr 1000 kwa mwezi
3.Posho ya ubunge kwa mwezi 1,000,000/=
4.Posho ya kukaa bungeni kwa siku 80,000/=
5.Posho ya kuendesha ofisi kwa mwezi 700,000/=
6.Simu ya mkononi kwa mwezi 500,000/=
Jumla ya mapato hayo ni7,200,000/=ukiachilia mbali posho za vikao vya kamati mbali mbali na safari za nje. bado wameona pato hilo kwa mwezi halitoshi wamejiongezea posho ya vikao mpaka 200,000/= kwa kisingizio kuwa maisha ni magumu. madaktari walipogoma posho imeongezwa kufikia 25,000/=. waalimu wanalalamika hakuna anayejali. Hii imekaaje? na nini kifanyike?. Tafadhali changieni bila ghadhabu. Nawasilisha.


source: gazeti la mwananchi jumatano 29/02/2012 page 3

Kweny nyekundu mwandishi kakosea. Kuna posho ya kukaabungeni kwa siku sh 70,000/= ambayo ndo wanataka iongezwe kuwa 200,000/=. Sh 80,000/= kwa siku ni posho ya kuwepo dodoma au anapokuwa nje ya jimbo lake kikazi kwa siku. Hii posho inaitwa daily subsistence allowance au wafanyakazi wengi huiita per diem. Kwa maana hiyo huwa wanapata 150,000/= kila siku anapokuwa dodoma ambapo wanataka ipande ifikie 280,000/=
 
Wana jf,sio kwamba posho hazitoshi kwa hawa "waishiwa" wetu tatizo ni mikopo waliyokopa ndiyo inawasumbua! unakuta mbunge kakopa 100M so unadhan anakatwa kiasi gani kwa mwezi na yy atabaki na kiasi gan..ndio maana wanasema posho hazitoshi
 
walipokuwa wanaomba kuchaguliwa ubunge walikuwa wanaomba KULA siyo KURA.Ndiyo maana kila siku wanataka posho iongezwe.
 
Wana JF naomba mwongozo hapa:
Hivi Mbunge wa VITI MAALIM ambaye pia ni Waziri/Naibu Waziri, ANAMWAKILISHA NANI?
 
Daaaa! Mwalimu anapokea amejitaidi sana laki nne kima cha juu, na huyo ni wa degree...milioni saba wabunge fedha ya kumlipa mwalimu miezi 14 hiyo wa degree anapewa kwa mwezi mmoja....kweli nchi inasubiri kuzikwa na sasa ipo mochwari!
 
Tatizo ni kwamba pesa zote hizo washakopa na kutumia kulipa madeni ya waliowapa pesa za kutoa rushwa....so wanataka nyongeza ili waweze kusavaiv
 
nIMECHOKA!
KAMA hata wabunge wa viti maalum kama Mama Lwakatare wanalipwa hela kama hizo basi inatakiwa walipwe nusu ya hiyo hela!
huyo mama anamuwakilisha nani walokole au? mbona sioni shehe au padri....unanikumbusha kale kabibi eti pesa wanayopata wabunge ni ndogo au kwa vile katoa lile wigi kichwa kimekuwa chepesi ndio maana kaongea pesa kigogo?

 
Kwa mapato haya naomba wale aliosema Makinda wanataka kuacha kazi waache ili sisi wenye njaa tuingie...Kweli Makinda hana aibu,kwa mapato haya anasema kuna wabunge wanataka kuacha kazi..hebu aache kututania na kutuchezea akili.
 
mwalimu wa degree analipwa pungufu ya 450000/= ya makaratasi ,yaani ni posho ya siku 3 ya mbunge kwa kiwango cha sasa.This is tanzania we want ,watu wakisema nchi inaliwa na wajanja utakuta kuna watu wanatetea humu utafikiri wametumwa
 
Wanangu Tanzania haina wabunge bali wala ubuge. Wanawakilisha matumbo yao yasiyotosheka ili kuridhika roho zao za fisi. Hawana jipya zaidi ya kutaka waendelee kuiba na kuiba na kuiba na kuiba hadi wakiambiwa hata damu yetu ni deal wauze. Wanangu, mkiendelea na watawala wa namna hii watawauza utumwani kama litapatikana soko popote pale mradi pasiwe peponi. Hata hivyo mnapaswa kulaumiwa kwa kuwa mashahidi wa wenzenu wakiwatimua watawala mafisi kama ilivyotokea Libya, Misri na Tunisia. Msibaki kujadili mapinduzi haya vijiweni bali muyaigize na kuingia mitaani kujikomboa.
 
1.Mshahara kwa mwezi tshs 2,300,000/=
2.Mafuta ya gari kwa mwezi 2,000,000/=i.e ltr 1000 kwa mwezi
3.Posho ya ubunge kwa mwezi 1,000,000/=
4.Posho ya kukaa bungeni kwa siku 80,000/=
5.Posho ya kuendesha ofisi kwa mwezi 700,000/=
6.Simu ya mkononi kwa mwezi 500,000/=
Jumla ya mapato hayo ni7,200,000/

Kwa mujibu wa Spika mtu anayepokea pesa zote hizi ni maskini wa kutupwa Tanzania.
 
hesabu ulizoweka na hiyo Total hai tally kabisa, kwanza teguwa kitendawili hicho.
 
Back
Top Bottom