Songambele
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 4,695
- 2,553
TFF wametoa taarifa ya mapato yaliyopatikana katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga kuwa ni TZS 239 millioni na jumla ya watu 52,890walishuhudia mpambano huo wa kukata na shoka. Idadi hii wa watazamaji halingani kabisa na taarifa zote zilizotolewa kuhusiana idadi ya watazamaji.
Lakini ni kwa mara ya kwanza uwanja ulijaa kuliko katika mechi zilizotanguliwa na imani ya watu ni kuona na mapato pia yanavunja rekodi mapaka VIP watu walisimama. Uuzwaji wenyewe wa Tiketi ulikuwa na utata mie nilipata tiketi ya Taifa stars na Cameroun. Vyovyote vile watu wamepiga hela hapa na hesabu ya TFF sio sahihi kwa justification yoyote ile. Sababu ya kusema waliingia watu wengi zaidi kwa TZS 3,000 basi kuna watu zaidi ya 70,000 waliingia uwanjani kwa hiyo kuna idadi ya watu kama 18,000 hawako katika vitabu vya TFF na si chini ya TZS 54,000 hazipo kabisa katika mahesabu.
Kuna haja ya kuchunguza TFF na kujiridhisha kama hakuna ufisadi manake kuna kila dalili kama TFF pia ni chaka la mafisadi. watu wanatengeneza mazingira tata ya tiketi na wanacapitalize. Kwa kuwa hakuna jiwe litakalo achwa bila kugeuzwa basi iwe zamu ya TFF sasa.