Mapambano police na wananchi ifakara

Gaza

Senior Member
Nov 3, 2010
102
8
nimepigiwa simu na jamaa aliyeko ifakara( kilombero) kumetokea mgogoro mkubwa kati ya wakulima na halmashauri ya W/ya kilombero kisa halimashauri kudai ushuru wa sh 3000 kwa gunia la mpunga ,wananchi wamegoma wanafanya maandamano mashine za kukoboa zimesimama hakuna mchele unaotoka hapo kwenda popote ,FFU mabom virungu mtindo mmoja. Kama kuna alie eneo la tukio atujulishe kwa ufasaha
 
Halmashauri inawaonea wananchi, waangalie namna ya kuwasaidia hawa wananchi siyo kuwakomoa kama ilivyo sasa. Na bado kuna maeneo mengi tu watu wanaoneo kwa sababu ya elimu duni na kutishiwa.

Mfano wilaya moja ya kishapu mkoani shy watu wengi wakitishiwa wanalala mashambani kwao na si nyumbani. Its so sad huku viongozi wanahubiri amani.
 
Ni kweli gaza ni mabomu ya machozi na marungu kwenda mbele mjini ifakara.
 
AWALI ILIKUWA GUNIA LA KILO 100 UNATOZWA TSHS 1000 SASA SUDDENLY JAMAA WAME HIKE MPAKA TSHS 3000 KWA GUNIA, WENYE MASHINE ZA KUKOBOA MPUNGA NA WENYE MAZAO HAYO KWA PAMOJA WAMELIPINGA HILO NA UMMA UKAWAUNGA MKONO WAKAWEKA MAGOGO BARABARANI NA MAWE MAZITO, POLICE FORCE IMETUMIKA KUPINGA MAANDAMANO HAYO.

WALIWASILIANA NA MH. MTEKETA a.k.a PAPAA AKAWAJIBU KUWA HILO LIKO NJE YA UWEZO WAKE NA NDIO MSINGI WA WAO KUTUMIA NGUVU YA UMMA.
 
Twala nae Ugali Rose Garden sasa hivi
 
Mhe. Mwema liangalie hilo. Najua wewe ni mwema na utatenda mema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
AWALI ILIKUWA GUNIA LA KILO 100 UNATOZWA TSHS 1000 SASA SUDDENLY JAMAA WAME HIKE MPAKA TSHS 3000 KWA GUNIA, WENYE MASHINE ZA KUKOBOA MPUNGA NA WENYE MAZAO HAYO KWA PAMOJA WAMELIPINGA HILO NA UMMA UKAWAUNGA MKONO WAKAWEKA MAGOGO BARABARANI NA MAWE MAZITO, POLICE FORCE IMETUMIKA KUPINGA MAANDAMANO HAYO.

WALIWASILIANA NA MH. MTEKETA a.k.a PAPAA AKAWAJIBU KUWA HILO LIKO NJE YA UWEZO WAKE NA NDIO MSINGI WA WAO KUTUMIA NGUVU YA UMMA.

Huyo mtu hakuna jambo litakalo kuwa ndani ya uwezo wake, yeye anachojua ni kuuza magari used basi! Wanakilombero wasubiri maumivu tu kwa miaka hii 5 ya uongozi wa PAPAA!
 
Mh!Tanzania ya leo ni tofauti na Tanzania ya jana!watanzania sasa wameshajua haki zao,CCM kaeni chonjo!!
 
POLICE FORCE IMETUMIKA KUPINGA MAANDAMANO HAYO.
Polisi wanatimiza wajibu wao ili kulinda amani. Serikali/Halmashauri zinao wajibu wa kubuni vyanzo vingine vya mapato. Si vizuri kumkandamiza Mwananchi / Mkulima kwenye kila shilingi anayojitafuta katika mazingira ya shida kubwa. Amini nawaambia Kilimo cha mpunga ni kigumu sana hasa kama hutumii Trekta, Dawa za kuua majani na mbolea. Hebu tujiulize Halmashauri imemsaidiaje mkulima huyu katika kuzalisha mpunga mpaka ifikie kupandisha ushuru kwa 300%. Tatizo la TZ maneno ya siasa ni mazuri mno lakini utekelezaji wake ni kinyume chake.
 
Viongozi wa halmashauri wana shida ya kubuni vyanzo vya mapato lakini pia hata sera za nchi hazilengi kuwaendeleza wakulima wetu. Tumieni nguvu zenu wana kilombero kupata haki yenu msirudi nyuma. 2015 angalieni mbunge atayefaa, mnachagua ma-papaa hamjui hayo masanii????
 
ndo wakome kuchagua mbunge mwizi wa kura kutwa ana kazi ya kuimbwa imbwa na mabendi ya mziki
 
ndo wakome kuchagua mbunge mwizi wa kura kutwa ana kazi ya kuimbwa imbwa na mabendi ya mziki

Hawakumchagua abli alicahaguliwa na NEC
7fc9c36a-1d78-4073-8e7c-c5ebf6350083.jpg
 
jaya nimtokeo ya umbumbumbu wetu wa Tz viongozi wa serekali ya Ccm hawawezi kumkomboa masikini wa nchi hii masikini ndio mwenye haki ya kulipa ushuru lakini wabunge wanauziwa magari bila kutozwa kodi tena kwa mkopo ,watanzania tudaini katiba bila woga wa huruma na mtu
 
Ebu waulizeni wale waliotinga barabarani kushangilia ushindi wake (Mteketa) baada ya Regia kunyang'anywa. Walivaa khanga na kofia za ccm kushangilia (na kumkebehi Regia) bila kujua wanashangilia kiama chao. Nawashauri leo hii wavae vilevile na kusema ccm oyee!!
 
Regia Mtema uko wapi? Huu ndiyo wakati wa kuwa karibu na wapiga kura usisubiri hadi 2015
 
Ivi viushuru si ndo ambavyo Tundu Lissu kavipiga marufuku kule kwao au nimechanganya madesa?
 
Sijaelewa, wanapigwa mabomu ili walipe kodi, au wawashe mashine za kukoboa?
 
Mh!Tanzania ya leo ni tofauti na Tanzania ya jana!watanzania sasa wameshajua haki zao,CCM kaeni chonjo!!

Sasa hivi hawakai chonjo, uchaguzi umekwisha!!! Watakuwa chonjo ikikaribia uchaguzi 2015!!! Huoni mapambano ya machinga yameanza wakati yalituli karibia uchaguzi? Kibaya zaidi yale majimbo ambayo upinzani ulichukua wanalipiza kisasi!! Hata kuungua soko mbeya nina wasiwasi na move hiyo!!!
 
Back
Top Bottom