Mapacha watatu ni nani hasa?

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Hivi karibuni karibuni habari kuhusu mapacha watu zimepamba moto. Lakini mpaka sasa hakuna mtu au chombo cha habari kilichohoji dhana ya mapacha watatu. Kwa muda mrefu tumeelewa mapacha watu kuwa ni Kikwete, Lowasa na Rostam kutokana na urafi wao wa kisiasa katika kutafuta urais mwaka 2005. Urafiki wa Lowasa na Kikwete umewahi kuthibitishwa na Lowasa mwenyewe aliyesema hakukutana na Kikwete barabarani. Makala nyingi za Tanzania daima zimewahi kuandika kwa kina urafiki huu wa Kikwete, Lowasa na Rostam. Sasa nashangaa ni kwa vipi mapacha watatu wamebadilika kuwa Lowasa, Rostam na Chenge?. Mapacha watatu ni Kikwete, Lowasa na Rostam. Lakini katika dhana ya kuvua gamba mapacha wamebadilika ghafla. Kwa nini hakuna hata mmoja aliyehoji mabadiliko haya ya kufikiria kuhusu mapacha watatu?
 
Pacha mmoja alifariki jana na kuwaacha wawili. Hii maana yake ni kwamba Lowassa ambaye ndiye roho ya mapacha anaanza kukwanyuliwa taratibu. Hawakujua mwenzao ni gobacholi ambaye akitishiwa nyau anaufyata!
 
Back
Top Bottom