Mapacha walioungana katika vita dhidi ya ufisadi? Bunge na C.C.M

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Mapacha walioungana katika vita dhidi ya ufisadi? Bunge Kukosa Meno na Sintofahamu za Spika Sita.

Nimejaribu kufuatilia mjadala kuhusu suala la spika kukataa hoja binafsi ya Mh. Daktari Slaa ya kutaka kujadiliwa suala la kuingiliwa kwa mchakato wa kuitafuta kampuni utakayopewa dhamana ya kuchapisha vitambulisho.

Kama Mh. Sita ni mzalendo wa kweli kwa nini alitoa maelezo yenye kutia shaka kwamba ‘Kamati ya Usalama’ inalijadili suala hilo na kwamba mchakato umeshafika mbali kwa hiyo si busara kuingilia kati huo mchakato (paraphrased – I stand to be corrected on this).

Mh. Sita, huoni tunarudi kule kule kwenye suala la Richmond lilivyondeshwa. Hivi lini tutaweza kuwa na political will kuondoa hizi impunity. Manake sasa hivi ni kama ‘conjoined twins’ kati ya bunge , dola na chama tawala. Kwa nini maamuzi nyeti yanayopaswa kufanywa na bunge yanafanywa nyuma ya pazia la ‘kamati maalumu?’ Ushahidi wenye kutia shaka utendaji wa kazi wa baadhi ya mawaziri na umma umeona hilo lakini huyu ‘pacha’ yeye anakaa kimya wakati wa kuchukua hatua. Yote haya ni kuwa pacha huyu ameungana sana na ndugu yake ‘CC.M’ kiasi ambacho hawezi kupumua vizuri. It is time to test the water.

Ombi langu kwa wananchi: huyo pacha aliyeshikamana anahitaji upasuaji mwaka 2010. Bunge linatakiwa liwajibike kwa waajiri wake sisi wapiga kura na si vinginevyo. Kitakachotokea katika hiyo Tenda ni hoja kuletwa mwakani kuhusu bunge kuunda kamati ya kina Mwakyembe kuchunguza mchakato mzima wakwati vitu hivyo vyaweza kushughulikiwa na bunge wakati mambo hayajaaribika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom