Maonyesho ya Maiti Zikijamiiana Nchini Ujerumani

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Maonyesho ya Maiti Zikijamiiana Nchini Ujerumani
3109866.jpg

Unaweza kuamini kuwa hili si sanamu ni maiti ya mtu aliyejitolea mwili wake kwa bwana Hagens, Picha zaidi nenda kwenye Photo GalleryThursday, September 17, 2009 8:03 AM
Mtaalamu maarufu wa elimu ya mwili na viungo vya binadamu (Anatomy) wa nchini Ujerumani amezua mjadala mrefu kutokana na maonyesho yake ya maiti za binadamu zikiwa katika staili mbali mbali za kujamiiana. Gunther von Hagens mtaalamu maarufu wa elimu ya mwili na viungo vya binadamu na wanyama (Anatomy) amezua mjadala mrefu nchini humo kutokana na maonyesho yake aliyoyaandaa ya maiti za binadamu zikiwa katika mikao mbali mbali ya staili za ngono.

Hagens anatumia njia aliyoigundua mwenyewe inayojulikana kitaalamu kama "plastination" ambapo maiti hutolewa ngozi yote na kisha majimaji yote kwenye maiti kukaushwa.

Hagens hutumia plastiki zilizotengenezwa kwa madini ya silicon kuziweka maiti hizo katika maumbile mbali mbali kuonyesha maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Hagens na mkewe Angelina Whalley wameishafanya maonyesho kama hayo katika sehemu mbali mbali duniani na inakadiriwa watu milioni 27 toka sehemu mbali mbali duniani wameishahudhuria maonyesho yake.

Lakini katika maonyesho yake mapya yanayofunguliwa hivi karibuni Hagens ameamua kuziweka maiti zionekane kama zinajamiiana na kuzua mjadala mkali nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanasiasa nchini Ujerumani wamesema kuwa maonyesho hayo hayaonyeshi heshima kwa maiti na wamesema hayakubaliki katika jamii.

Hagens alisema kuwa maiti anazozitumia kwenye kazi zake ni za watu waliojitolea miili yao kwake kabla hajafariki. Hagens aliongeza zaidi kuwa yeye mwenyewe ameishajitolea maiti yake itumike namna hiyo akishafariki.

Hata hivyo baada ya jumba lenye ukumbi ambao angefanya maonyesho yake hayo kukataa maiti zinazoonekana kama zinajamiiana, Hagens alisema kuwa atapeleka maiti zake zingine katika maonyesho hayo zikiwa katika hali tofauti kwa mfano kuna maiti zinazoonekana kama vile zinacheza drafti, soka na mpira wa kikapu. GONGA HAPA KWA PICHA ZA MAITI HIZO


www.nifahamishe.com
 
Mungu atuepushe na haya


Maonyesho haya yanafanyika sehemu mbali mbali duniani, cha kusikitisha source ya hizi maiti ni pamoja na watu kuuawa nchi kama China au maiti za wafungwa wa adhabu ya kifo.

Ukiwa unafurahi hayo maonyesho ya maiti ujue sio wote walijitolea bali kuna watu maisha yao yamekatishwa.
 
Jamani hii Dunia naona tumefika mwisho. Kweli hivi wapi tunakokwenda?

Mkuu Ng'wanza maonyesho hayo sio mabaya kama hivyo unavyofikiri...Nadhani hiyo habari ya watu kujamiiana ni kipande kidogo tu cha maonyesho mazima,na kuna sehemu nyingi hawaonyeshi jambo hilo....Nami nimekwishaaangalia maonyesho hayo,ni mazuri na unapata nafasi nzuri ya kuona jinsi baadhi ya viungo vyako vya mwili vinavyofanya kazi..tafuta muda uangalie wapi unaweza kwenda kuona Elimu hiyo!
 
nami nimependa hiyo, nadhani ni vizuri tukijua mabo mbali mbali ya binadamu, kwani kuna ubaya gani? sidhani kama kuna tatizo katika hili
 
Maonyesho haya yanaitwa "HUMAN BODY WORKS" nimeona ads around the city ila sijawahi kufika, Hopeful next time when they are intown nitaweza kuhudhuria.

Kwa majority ya watu wa Science itamake sense ila kwa wengine sidhani kama wataelewa.

Kaka'B.
 
Uzuri wake nini bana acha kutuyeyusha.......!

Uzuri wake ni mafundisho na ufahamu zaidi unaoupata kuhusu mwili wa binadamu! Kwa mfano, mimi nilikuwa sijui kuwa pelvic bone ya binadamu wa kike inafanana kabisa na pelvic bone ya Nyangumi wa kike! Tofauti ni size tu.
 
Maonyesho haya yanaitwa "HUMAN BODY WORKS" nimeona ads around the city ila sijawahi kufika, Hopeful next time when they are intown nitaweza kuhudhuria.

Kwa majority ya watu wa Science itamake sense ila kwa wengine sidhani kama wataelewa.

Kaka'B.

Wenye lugha yao wanaita Körperwelt, wakati wa kuangalia huitaji kutafsiri sana unachokiona
 
Back
Top Bottom