Kuanzia tarehe 1/10/12 mpaka 10/10/12 kutakuwa na maonyesho ya ufugaji wa nyuki pale uwanja wa Nyerere Dar es Salaam. Haya maonyesho yana maana gani kwetu?
Mimi naona ni fursa nzuri ya kuunganisha nguvu zetu ili na sisi tuingie katika fursa hii na kuanzisha usindikaji wa asali. Mzinga mmoja ni Tsh 60,000/( top bar type), ina maana ukiwa na Tsh 300,000/ unakuwa na mizinga mitano.Tukiwa watano hivi ni kwamba tunakuwa na mizinga 25 ya kisasa.
Tunanunua shamba eka kumi kwa sh kama laki nne, na usafirishaji wa mizinga tuweke wastani wa laki mbili. Kununua pro polis kama sh 10,000/. Mzinga mmoja ukitoa debe moja na nusu sawa na lita 30 zidisha na mizinga 25 zidisha na bei la lita moja, Tsh 10,000/
Kila mwaka tunaongeza mizinga mitano mitano, nina hakika baada ya miaka mitano ni lazima tujenge kamtambo ketu.
Nawaomba nyie wenye hela na nafasi ya kwenda porini hamna, leteni hela hizo watu tuingie porini tutoke na nta. Nataka kusema, wewe kama uko b/ze sana na hela unayo, toa tufanyie kazi na wewe tutakupa gawio lako. Vinginevyo Wachina watajenga kiwanga cha pili sisi bado tunabonyeza key board kuilaumu serikali.