Maoni yenu wakuu

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,314
7,730
Wahishimiwa, jana kuna mshikaji wangu mmoja alinifuata na kuniambia ishu fulani hivi, ishu yenyewe anasema imetokea kama miaka 3 iliyopita, ila kwa muda wote huo alikuwa anajiuliza bila kupata majibu. Binafsi nilikosa jibu, so ikabidi nimwambie nitajaribu kutafuta jawabu. Ishu yenyewe ni hii.

Siku mmoja rafiki yake huyu rafiki yangu alimpigia simu na wakawa wanaongea, just a salamu, then baadaye akasema amemuona baba yake maeneo fulani akinunua nyasi za ng'ombe, jamaa alikuwa akimwambia as friend na wala hakua na nia mbaya. But huyu rafiki yangu akapata maswali mengi sana, kwani kwao hawana ng'ombe wala mbuzi, halafu kusema kuwa labda ametumwa na bosi wake ni kitu kigumu kuingia akilini kwani baba yake ni vice chairman of one of the Company. So anahisi baba yake ana nyumba ndogo. So jamaa amekaa na swali hilo kwa muda mrefu, akitaka kumuuliza baba yake, anashindwa pa kuanzia, pia akitaka kwa mama yake anaona huenda akazua tatizo.

So waheshimiiwa naombeni mchango wenu, ninyi mnafikiriaje kwani mshikaji amekaa nalo,but limemshinda.
 
...ishu ndogo sana hiyo kujiumiza nayo kichwa miaka mitatu. Atajiskiaje baba yake akimjibu hakuwa yeye (case of Mistaken identity)? ...atamuamini baba yake au rafiki yake?

Aachane na utoto huo.
 
huyo ni rafiki yake na anamjua mshua wa msela kwani ni watu ambao wanaishi karibu na mara nyingi huyo rafiki yake hushinda kwao, pia hata gari aina ya pick up ni ya mshua wa msela.
 
Mbona mie sielewi! Naona kama hii issue ipo a bit too odd! Sasa kama babake ana nyumba ndogo yeye anataka kujua ili iweje? Asubiri tu umri ukiruhusu ataonyeshwa tu 'mamaake mdogo' na 'wadogo zake' kama wapo.
 
huyo ni rafiki yake na anamjua mshua wa msela kwani ni watu ambao wanaishi karibu na mara nyingi huyo rafiki yake hushinda kwao, pia hata gari aina ya pick up ni ya mshua wa msela.

...kinachonishangaza, kwanini katika yooooooote anafikiria baba yake ana nyumba ndogo? Kuna ajabu gani mzee kununua/kukata majani ya ng'ombe hata kama hana mifugo? Huenda ni mifugo ya rafiki yake je?
 
Inaitwa maumivu ya kisaikolojia ympatayo rafikiyo, na asipopata ufumbuzi ataingia kwenye ugonjwa wataalam wanauita Syndom of Eksesiv thinking....

There4 hana jinsi,
Nakumbuka kuna mtu aliwahi kunifanyia kitu ambacho kiliniumiza saana, nilitamani kumwambia ila on process huyo mtu akafariki.

Nashauri amconfront huyo mshua, it cost, but pays...
Anaweza hisi ni jambo zito kumbe ni lepesi tu kujadilika, ila before its too late...
anaweza pia kumsaidia mamaye kwa kumfunua macho baba pale tu atapofahamu ishu inajulikana na akajaribu kuchange....

Ila atafute a positive approach ya kuongea na babaye.

Kila la Kheri.
 
Back
Top Bottom