Maoni yangu matokeo kidato cha nne 2010

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Hivi karibuni baraza la mitihani lilitangaza matokeo ya kidato cha nne ya Octoba, 2010.Kwa kiasi kikubwa matokeo hayo yanatoa picha halisi jinsi elimu yetu ilivyodidimia.Kama una mtoto wako anasoma katika shule hizi za sekondari za kawaida jaribu kupitia madaftari yake na kumwuliza maswali madogo madogo tu,majibu atakayo kupa yatakupa picha kamili ya mtoto huyo na shule anayosoma.Hakika sishangai hata kidogo matokeo hayo kuwa mabaya.

Nimejaribu kufanya zoezi dogo sana la kuthibitisha kile kilichofanyiwa utafiti na shirika lisilo la kiserikali la Twaweza.Nikagundua ni kweli haya jamaa walifanya utafiti wa kweli kabisa.Watoto wengi hawajuia kusoma na kiswahili achilia mbali kiingereza na kukokotoa hesabu.Huu ni ugonjwa ambao kama serikali hii haitachukua hatua za makusudi,tutazalisha mbumbu wengi miaka ijayo.Njoo kwa walimu wanaofundisha shule hizo.Wengi wao wapo kwa ajili ya mshahara tu hawana uwezo wowote.Na kosa ninaloliona au nimeligundua ni hili,serikali ilifanya makosa makubwa kuwaingiza walimu wa haraka haraka miaka kama minneau mitano iliyopita.Hii ikianzia na wale wa shule ya msingi hadi sekondari.Walimu wengi wanatumia vyeti vya kughushi si vyao.Tuna wwengi ambao awali majina ya shuleni yalikuwa mengine na sas wanaitwa kwa majina mengine.

Hawa ndio chanzo mojawapo cha kushuka kwa elimu.
Maoni yangu ni haya.Serikali ingefanya juhudi za makusudi kuchagua wanafunzi wanaomaliza kidato cha sita kwa kufaulu vizuri waende moj kwa moja katika fani hiyo badala ya kusubiri mtu achague mwenyewe apendavyo.Sasa hivi wengi wao wanaoenda ualimu ni wale walioshindwa kuchukuliwa katika fani zingine.
 
Tume yataka wenyewe.Muda umewadia wa kutumia kiswahili kufundisha shule zetu za sekondari.
 
Back
Top Bottom