maoni yangu kwa ZITTO na POAC kuhusu KUPEPELEA BAJETI!

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,066
1,535
Hi all!

nimekuwa nikisoma gazeti la mwananchi leo na kuona nia ya mheshimiwa Zitto Kabwe kupitia kamati yake ya umma inayosimamia mashirika ya umma POAC kukagua juu ya fedha zilizokuwa zikitumika na wizara ya nishati na madini kuhonga ili bajeti zipite kwa miaka kadhaa iliyopita...

Rushwa hizi zinazoliwa kwa njia ya rushwa hata hivyo hazipo katika wizara hii pekee. hii imekuwa ni DESTURI ya miaka mingi ya serekali kupitia mashirika yake kupepelea ili bajeti zisizokuwa na mashiko zipite....

wito wanhu kwa mheshimiwa Zitto Kabwe ni kwamba kuna haja ya kulaunch SERIOUS FRAUD INVESTIGATION kwa wizara zote kwani zimekuwa zikila mabilioni ya shilingi kwa kupitia taasisi zake kila wakati wa bunge la bajeti kwa madai ya KUPEPELEA BAJETI ZA WIZARA ZAO!

naamini kabisa mkifanya utafiti huu kwa kushirikiana na mabank yaliyo na matawi dodoma na wafanyakazi kadhaa walio katika taasisi hizi za umma na wenye mapenzi mema na mama TANZANIA mtakuja na findings za AJABU SANA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
wizara ya nishati na madini haikaguliwi na POAC wewe bana mbona huelewi
 
wizara ya nishati na madini haikaguliwi na POAC wewe bana mbona huelewi

HAPANA nazungumzia taasisi na mashirika ya umma yanayotumiwa kuzungusha hela za kupepelea bajeti? - anyway, labda nimepotea protocol lakini wizara zimekuwa ikitumia taasisi, idara na mamlaka zake kupata hela za kupepelea bajeti!
 
Kamati inayosimamia hesabu za serikali kuu inaongozwa na Mh. Cheyo mbunge pekee na mwenyekiti wa UDP Taifa
 
Nina uhakika uchunguzi 'huru' ukifanyika kwenye kamati za bunge hasa inayosimamia mashirika ya umma, na ile ya serikali za mitaa pamoja na mahesabu ya serikali, watakuta maajabu kushinda haya Jairo. There is no way mashirika ya umma yanapeta all these years despite the obvious scandal. PPF, NSSF, PSPF, LAPF, NIC na wengine.
 
Back
Top Bottom