Maoni yangu kwa January Makamba na Zitto Z. Kabwe

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kumekuwepo na mjadala mkubwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu Umri na uraisi nami leo ningependa kujadili mada hii kadiri ya uwezo wangu.

Nafasi ya uraisi ni nafasi ya juu kabisa katika uongozi wa Taifa letu.

Nafasi hii inahitaji mtu aliyepevuka kiakili na mwenye hekima na busara atakayejitolea maisha yake kwaajili ya mustakabali wa Taifa letu.

Taifa letu linachangamoto nyingi sana ambazo zinahitaji Raisi shupavu na mwenye busara kuzikabili ni vizuri tukapima uzito wa kazi na kuangalia mtu anayefaa kulivusha Taifa kutoka hapa lilipo.

Ni muhimu tunapozungumzia kuhusu raisi wetu ajaye, tusizungumzie watu au tusifanye ushabiki, ni wazi ya kwamba mustakabali wa Taifa letu utakuwa mikononi mwa raisi ajaye lakini pia si jambo la busara kuzungumza habari za uraisi sasa hivi ikiwa bado miaka mitatu raisi huyu aliyepo madarakani aondoke.

Jambo la msingi hapa ni kujiangalia upya kama Taifa na kama mtu mmoja mmoja, tujiulize ni nini lengo la sisi kuwepo pamoja kama Taifa na nini changamoto zetu.

Taifa letu linakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo zinahitaji akili zilizopevuka.

Umoja wa Taifa letu umetetereka, kuna changamoto ya maadili katika Taifa letu, naamini kabisa pasipo umoja hatutaweza kulitoa Taifa letu hapa lilipo.

Tunahitaji raisi atakayekusanya watu katika lengo moja na nia moja ili kukabiliana na changamoto tulizonazo, tunahitaji raisi atayeinua roho za watu katika kufanya kazi, katika uzalendo na katika kulitumikia Taifa hili bila kuchoka, bila kulipenda Taifa hili kwa dhati na bila unafiki kamwe hatutafanikiwa katika jitihada zetu.

Hatuko Taifa ili kila mtu ajiangalie mwenyewe, kila mtu ana wajibu kwa mwenzake, anawajibu kwa jamii na kwa Taifa lake, kwakuwa sisi ni Taifa na majaliwa yetu ni mamoja. Mwelekeo wa Taifa letu unatutegemea sisi, ni fikra zetu ndizo zilizotufanya tuwe na Taifa la namna hii, lenye maliasili kibao lakini maskini, ni kwasababu ya kiburi chetu cha kutokutaka kufikiri ili kujenga Taifa hili, kwa manufaa yetu sote na kwaajili ya kizazi kijacho.

Kila siku naamini Taifa hili linauwezo wa kuwa kama Taifa lolote lile kubwa ni uamuzi wetu tu, Funguo za maendeleo ya Taifa hili ziko mikononi mwetu ni uamuzi wetu kuamua kuleta mabadiliko katika Taifa letu au kuendelea kuishi kama tulivyo. Tukijipanga vizuri na kama kila mtu akiwa mwaminifu kwa Taifa hili na tukijitolea tutafanikiwa.

Imani ya taifa hili imeshuka, imani ya kwamba tunaweza kuendelea na kuwa Taifa kubwa, matumaini yetu yameyayuka kila mtu anajiangalia mwenyewe tuna sahau kwamba tuko pamoja katika ujenzi wa Taifa hili.

Matumaini ya vijana wengi kwa Taifa lao yameshuka, ni jukumu letu la kuyarudisha matumaini hayo ya kwamba siku moja wataliona Taifa hili likinyanyukia na likiheshimiwa miongoni mwa mataifa mengine. Tumaini hili lazima liwepo kwa kila kijana wa Taifa hili, tumaini hili ndilo litakalofanya Taifa letu liwe hai, Tunahitaji raisi anayejua hili. Lazima tufanye kazi kwaajili ya kuleta heshima kwa Taifa hili, ifike wakati ukimtajia mtu mimi ni mtanzania aogope sababu ya uwezo wetu.

Kwahiyo busara na maono ni kitu cha msingi sana kwa raisi yeyote ni jambo la kwanza kwakuwa raisi ndiye anayebeba dira ya nchi na mwelekeo wa taifa unategemea sana uwezo wake binafsi kwanza khalafu washauri wake, tunahitaji raisi atakayetuliza dhuruba hili lililochochewa na raisi aliyepo na kuliweka Taifa letu katika mstari, kwa kujenga umoja wa kitaifa na kusimamia maadili na utii wa sheria na kujenga misingi mipya ya kisiasa katika taifa letu, bila order Taifa letu halitosonga mbele katika maendeleo yake. Order katika familia zetu, katika vyama vya siasa na katika serikali. Tujenge upya misingi ya kuheshimiana na kufanya kazi kwa pamoja bila kutafuta sifa bali katika utumishi uliotukuka na tusisite kuwapa heshima yao watu waliojitolea kwaajili ya Taifa hili kwa dhati ya nafsi zao bila kutafuta sifa.

Watu wote walioingia kwenye siasa lazima wajue wana dhamana na maisha ya watu na watahukumiwa kwa kile walichotenda na wajue pia mwelekeo wa Taifa hili una wategemea wao na cheo sio kutafuta sifa au mali bali ni utumishi uliotukuka kwa wanadamu kama ''yesu alivyosema na anayetaka kuwa mkubwa awe mtumishi wa wote''.
Tunachoona sasa hivi ni utawala wa kibwanyenye wa baba kibonge na mtoto mwenye utapiamlo, ili Taifa hili liendelee lazima tufanye kazi pamoja kulijenga tofali baada ya tofali, na faraja ya Taifa lolote lile ni mafanikio yake ya pamoja. Hakuna sehemu yeyote ile duniani watu walipokuja pamoja katika nguvu moja na roho moja wakashindwa katika jitihada zao na tuwe na sauti moja bila unafiki bila kujikweza na bila kutafuta sifa kila mtu ajishushe tujenge Taifa hili.

Katika babylon ya zamani kipindi cha nimrod watu walikuwa na sauti moja na nia moja wakaamua kujenga mnara unaofika mbinguni mungu alijua watafanikiwa hakutaka wafanye hivyo akawatawanya, stori hii inaonyesha ni jinsi gani watu wakiunganisha nguvu kuwa wamoja watakavyofanya, watu wanapokuja pamoja hakuna kipingamizi wana uwezo wa kusawazisha milima. Kuna nguvu iliyopo ndani yetu iliyolemaa inabidi iamshwe na akili zetu ziamini ya kwamba tunaweza, tunauwezo wa kuandika historia katika dunia.

Kama taifa lazima tuwe na dira na dira hii tuirithishe kizazi baada ya kizazi, ya kwamba kama Taifa mwelekeo wetu ni huu na matumaini yetu haya, ni lazima tutambue ni nini tunataka katika dunia hii na ni aina gani ya Taifa tunataka kulijenga.

Taifa lazima lijengwa kwa faida ya wote na tusipotendeana haki Taifa letu litakosa furaha, siamini kwamba tumekuwa Taifa ili tunyonyane au mmoja amuone duni mtu mwingine, tumekuwa Taifa ili tulete maendeleo ya umma na viongozi ndio wanaoshika matumaini ya Taifa hili, maneno ya matumaini yasiyo ya uongo lazima yatoke midomoni mwao. Taifa hili lina uhaba wa viongozi ambao watoto watajifunza kutoka kwao na vijana watafuata mwelekeo wao kama maji yanavyofuata mkondo wa mto.

Roho ya Taifa hili lazima inyanyuke na ni lazima tuanze kulipenda Taifa hili na kulitumikia kwakuwa bila kulipenda kamwe hatutaweza kujitolea kulitumikia. Lazima tuwe na viongozi wanaoheshimiwa na wananchi sababu ya maadili yao na misingi yao wanayosimamia, hatutaweza kuendelea kujenga Taifa katika unafiki, Taifa hili lazima lijengwe katika ukweli.

Kuna kundi la wanasiasa ambao wanatumia ujinga wa watu kujinufaisha kwa maslahi binafsi hii si sahihi na wananchi wawe makini kutenganisha kati ya kondoo na mbuzi, Kazi ya mwanasiasa ni kuamsha mwamko wa wananchi wa kulipenda Taifa lao na kulitumikia, kuwaambia ukweli wananchi na sio kuwaongopea, kuwa kiongozi ni kuonyesha njia, hatutaweza kuendelea kuwa na viongozi wanaopotosha umma ni lazima turudishe mwelekeo wa Taifa hili. Taifa hili halitoweza kuendelea kuwa salama katika misingi ya ubinafsi, katika misingi ya watu kugombea uongozi kwa manufaa binafsi tusitegemee tutafika popote zaidi ya kuwa na vurugu na vita. Lazima tuwe wenye busara na kuamua mambo yetu kwa busara ili Taifa hili liendelee kuwa salama.

Watu wowote wale kabla ya kumpa mtu majukumu humpima uwezo wake kama ana uwezo wa kupewa majukumu hayo, na katika Taifa letu uraisi ni jukumu kubwa zaidi mtu kupewa ingawaje wengine hawaoni hilo kama jukumu bali ni nafasi ya umaarufu na kula, kwasababu hawajali maisha ya watu wengine. Na hii imetusababishia matatizo makubwa mno katika Afrika ijapokuwa mataifa mengi ya kiafrika ni matajiri yametopea katika umaskini kwasababu ya kuchagua watu wasiostahili kuwepo madarakani hivyohivyo kwa Taifa letu.

Tumekuwa watu wa ushabiki kuliko kutafakari changamoto zinazotukabili na kukabidhi majukumu hayo kwa mtu anayestahili. Katika uongozi wa nchi kusiwe na urafiki wala kujuana bali kumpa mtu anayestahili kutuongoza kutokana na maono yake, busara zake na uzalendo wake. Kwahiyo Hoja ya kiongozi wetu kuwa kijana au mzee haina mantiki hapa. Mtu Huyo lazima awe na uwezo wa kiafya na kiakili, awe na maono, busara na uzalendo na nia yake ithibitike ni kuliondoa Taifa hili hapa lilipo na kuliweka katika nafasi ya juu, na hii lazima iwe jitihada ya kiongozi yeyote yule sio kufikiria kutajirika au kupata umaarufu kupitia uongozi.

Nimesikia habari ya kina January makamba na Zitto kabwe kutaka uongozi wa nchi hii katika nafasi ya juu kabisa ya utumishi wa Taifa letu, majukumu ambayo ni makubwa sana kwao kwa sasa. Sijui nia na dhamira yao ni nini ikiwa ni kwamba wanaumizwa na matatizo ya nchi hii na wanaamua kujitolea kuliokoa Taifa hili ni ishara nzuri kwa kijana wa Taifa hili, lakini pia lazima wasubiri wakomae na ujana wote utoke ndani yao ili waivae busara itakayowafanya waiongoze nchi hii vyema, kuwa raisi wa nchi inahitaji maadili na busara ya hali ya juu bila self discipline hauwezi kuwa Raisi mzuri kama wao wanataka kuwa viongozi watakaokumbukwa katika Taifa hili wasubiri na watafute busara kwa udi na uvumba, waache anasa na maisha mengine ambayo vijana wengine wanaishi na akili zao zifikirie katika kujenga tabia zao na katika kutafakari masuala ya msingi yanayohusu Taifa hili, uraisi hauhitaji kuukimbilia ukijijenga vizuri uraisi utakufaa wenyewe utakuwa na vigezo vyote vya kuwa raisi na kwakuwa wao wako kwenye nafasi nzuri ya ubunge wana nafasi kubwa sana kuliko mie ambaye siko katika siasa kwa sasa, Wasikubali kila kitu wanachoambiwa na wafuasi wao wajipime na wajiangalie uwezo wao kama wanaweza kuwa raisi wa nchi hii, jukumu ambalo ni kubwa na linalobeba maisha ya watu. Nawashauri wajenge character zao kwanza wakue katika maarifa na busara zaidi ya yote wajitahidi kusoma falsafa na kutafakari kila wakati.

Lakini kama wameamua kutaka kugombea uraisi kwasababu ya kutaka umaarufu na kujinufaisha binafsi kamwe sitoweza kuwaweka miongoni mwa vijana ambao nitawaheshimu, namuheshimu kijana yeyote kulingana na virtues of his or her character, na ndio maana nasema tuangalie upya misingi katika vyama vyetu kwakuwa huko ndiko kunakozalisha viongozi, tukifanya vyama vya siasa kuwa ni ujasiliamali ni tabu tupu, kwahiyo wakati wote na sisitiza maadili na maadili ndio yatakayojenga misingi ya Taifa hili. Vyama vyote vya CCM na CDM ni vyama vya Taifa hili na vyama vingine, lazima tujenge misingi ya uzalendo katika vyama vyote hivyo na kuheshimiana, Vyama hivi vikionekana vinagombania tu madaraka na sio kujenga misingi ya Taifa hili changa inanipa tabu sana, kuna mambo kama Taifa lazima tuje pamoja bila unafiki ili kuyasimamia. Kitu ambacho ninaomba ni tubadilishe mwelekeo wa fikra zetu na tufikirie sasa kuhusu ujenzi wa Taifa letu kuliko ubinafsi na uchama.

Kwa maoni yangu CCM kama chama kikongwe Tanzania kinawajibika katika Demockrasia na mendeleo ya vyama vya siasa vya Taifa hili , ili Taifa hili liendelee kwasababu bila kujenga vyama imara vya upinzani, Taifa hili halitoweza kupiga hatua. kama CCM ina nia ya dhati kwa Taifa hili lazima ijenge democrasia sio kuibomoa ndani ya vyama vingine vya siasa, misingi ya kuaminiana na kuheshimiana ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.
Lakini pia kujenga maadili ya vijana wetu ambao baadae watakuja kuwa viongozi wa Taifa hili, sasa hivi kuna wimbi kubwa la vijana wanaoingia katika siasa lakini sina uhakika na maadili yao kama ni stahili na busara zao kama ni stahili kuongoza watu wa Taifa hili.

Kwa maoni yangu hatuna haja ya kupunguza umri wa uraisi kusudi vijana wagombee, umri wa miaka arobaini ulioanishwa kwenye katiba yetu unafaa kwakukuwa ni umri wa umakamo na mara nyingi binadamu hupevuka katikati ya umri huo na itakuwa ni rahisi zaidi hata kukubalika kwa wazee ni umri ambao uko katikati uzee na ujana, watu walio chini ya umri huo wasubiri au katiba isiweke limit ya mtu kugombea uraisi kwakuwa kushushwa kwa umri wa kugombea mpaka miaka 35 bado katiba haitakuwa imemtendea haki mtu wa miaka ya chini ya hapo ambaye pia kuna uwezekano akawa kiongozi mzuri pia, nachukulilia jambo hili ni jambo la utaratibu na subira hatuna haja ya kuvunja utaratibu huu hasa katika kipindi hiki ambacho viongozi wengi katika Taifa letu hawapishani uwezo sana na katika vijana hakuna mtu aliyeonyesha extra ordinary talent katika uongozi ambaye angestahili kushushiwa umri katika katiba ili agombee. Maombi yangu kwa akina zitto kabwe wasubiri na wajijenge zaidi wasitafute nafasi za juu za mamlaka haraka haraka.
 
... WaTanzania sote TUMESHAAMUA kwamba mambo yote ya ukombozi wa MTANZANIA kuondokana na MAFISADI ni kwa CHADEMA.

Je ni nani tena wa kutuzuia?????????????
 
Du Mzee Mwanakijiji amewa inspire wengi!, sasa vijana sio tuu wanashuka post, bali makala nzima humu jf!.

Keep it up, kufikia 2015, tutakuwa na kina Mzee Mwanakijiji wengi wa kumwaga.
 
Mtoa Mada bwana Shayu umesema vyema! Miaka 40 ni umri muafaka! Mtu mwenye kipaji cha uongozi hapo anakuwa mkomavu kabisa(msinitajie failure wenye zaidi ya umri huo kuwa reason ya kubeza huo umri!)
 
Udhaifu wa CHADEMA ndo unajidhihirisha hapo. wakivuruana wenyewe mchawi wao ni CCM , udhaifu mkubwa sana ambao unasababisha mimi sitaki kuwa mfuasi wa Chama chochote, bora nisubiri kuburuzwa na yoyote, Hivi ZITTO kutangaza kugombea Urais CCM inahusika vipi kama siyo kuishiwa kisiasa, je wakati ZITTO anaichachafia Serikali mbona huwa hatusikiii lolote zaidi ya kusikia ZITTO aishika pabaya CCM?
Mtu unajikunja kuandika Thread gazeti zima ukisoma ndani imejaa usingizi mtupu. MODS tusaidieni hili ili tusiwe bored humu JF. Humu sehemu ya kujifunzia kuandika Insha.
 
is simply our brain my dear! tukiambiwa IQ zetu ndogo tunaona matusi

hata watoto wana dreams za kuwa marais...Zito kasema simple, tena kasema akipewa ridhaa ya chama na wananchi!!! whats wrong with thats

asante umeliona hilo
 
Zitto this, Zitto that, kila mkiamka huku siku zinasonga... Hiyo miekspiriens mnayoitaka imetusaidia nini miaka 50 hii ya Uhuru. Maisha ya mtanzania yamezidi kuwa duni. Tazama maji safi na salama chini ya 30%, vifo vya kinamama kwa uzazi ni zaidi ya 500 kwa kila laki, umeme ni chini ya 20%,UFISADI NI ZAIDI YA 30% Ya bajeti ya maendeleo,vipaumbele vyetu vipo shagala bagala, halafu linatoka jitu linaongelea KUKOMAA KWANZA.

Nakereka sana wanaoshupalia MIEKSPIRIENS YA KIFISADI!
 
Mimi sidhani hata kwenye kikao cha familia unakaribishwaga unakosa busara na busara ndiyo itakayokomboa Taifa hili, mimi nimechambua vizuri hapo, ni ushauri wangu kwake na pili naomba uisome vizuri na ufikirie kabla hujanijibu ama sivyo watu kama wewe sitokuwa na muda wa kujiangaisha kuwajibu.
 
Rudia notes zako za Form three kiswahili ujifunze tena ku summarize!
 
Kwa faida ya mwelekeo wako katika maisha tafadhali acha mizaha na uzingatie mambo muhimu na yenye manufaa katika maisha yatakayokujenga.
 
Back
Top Bottom