Maoni yangu kuhusu Meru Residential Appartments

Samahani mkuu kwa kutotoa informations zote.
Najua demand imekuwa met huko Arusha. Nyumba hiyo ipo Toledo, OH ambapo sio kijjini sana ila siyo rahisi kuipangisha.Pamoja na hayo nini hakika kuwa huu mji upo industrialized kuliko Arusha, umbasli wa social services,etc, kuhusu winter, sijui sehemu nyingine duniani, ila US snow huwa effects zake kwa mwananchi wa kawaida ni negligibly small.

Barabara zinasafishwa nyumba zina a/c etc. Ila kama ulivyosema, demand inaruhusu bei hiyo. Kama demand inaruhusu bei hiyo, kwanbini unafikiri watu binafsi hawainvest heavily in housing? kwenye mji kama Arusha?

Nadhani NHC wamepunguziwa regulatory constrains( I'm not sure) ili kuwajengea wananchi kama waalim, mapolisi, manesi etc waweze ku afford.
The point I was trying to make was, those apartments were expensive and they look like some projects. Hiyo ni biashara na wengi wataonunua watazipangisha kwa $.

Ofcourse hili ndiyo haswa tatizo naloliona na kulipredict kutokea. Lakini kwa mzingira ya ubepari uchwara na corrupt society kama Tanzania hilo huwezi kulikwepa. Kuhusu kujenga nyumba kwa aaffordable kwa manesi, polisi na general public servants community kiukweli ni lazima serikali i-chip in kwa sababu kwa mishahara ya Tshs 200000, hata kama ni yote inalipia mortgage kila mwezi. Kwa nyumba ya kisasa na nafuu basi unahitaji zaidi ya miaka 20 kulipia with interest.

All in all ni kwamba soko la nyumba Tanzania lipo, sema wabongo na utamaduni tuliozoea wa kutaka kutafutana na fundi Abdala, ufisadi, high interest rates za mikopo sometimes ndiyo vinakwamisha.

Halafu watu wanaona kununua nyumba kwa mortgage kama siyo sahihi vile!!!! Kwa utaratibu wetu siyo siri serikali kwa hizi hatua za mwanzo lazima iingilie kati!
 
hivi zile nyumba za magomeni ziliuzwa kwa bei mbaya namna hii?
 
Babu, kama kuna kiwanja cha namna hiyo hapa Arusha mjini ambapo naweza kufanya vyote hivyo..please nielekeze sasa hivi!1 Arusha kiwanja pekee pale maeneo wanayojenga NHC, si chini ya milioni mia tatu (300)! na hapo ni unanunua gofu halafu ubomoe na kuanza kujenga upya...sasa nyumba gani utajenga kwa milioni 175-200 kama wanavyofanya wao? hebu tusiwaonee jamani!

Ni hayo tu!
 
175 milioni kaka sijui ni mtanzania yupi wanayemtaka anunue hizi nyumba.....

175 ni bei bila VAT,
Ukiiongezea hapo inafika 206.5 Milion kama bei ya kuanzia.
Halafu kumbuka uuzaji wenyewe uko kwenye mfumo wa mnada, so ili uipate inabidi uweke "bid" ya juu zaidi, halafu kumbuka ziko nyumba 30 tu.
Kwa makisio yangu unaweza ukaweka hata 230 Million na bado usiwe katika "Top 30", labda watu wasielewe wajue kua 175 au 206.5 ndio bei, hapo ndo waweza kubahatika kwa hiyo 230 Milioni.
Kwa hiyo unapopiga bei ya hizi nyumba sahau kabisa 175Milion, kitu kinaenda mpaka 230Mil au zaidi.
Kwa hesabu zangu, Sakina au Njiro naweza kupata Kiwanja hata kwa 20Mil kikubwa na Kizuri tu,
Ujenzi wa kisasa utakaoendana na ramani ninayoitaka mimi waweza kufika 100Mil mpaka nahamia.
Hizo 230Mil za kuwapa hao wezi naweza kujenga nyumba mbili saaafi kabisa bila longolongo.
Nlipata kumsikia Mkurugenzi mkuu wa hawa jamaa Kada- Nehemia Mchechu akidai kila anachokifanya ofisini kwake anatekeleza sera za CCM hivyo siwezi kushangaa sana bei zikiwa doubled.
Wajinga ndio waliwao!!!
 
Wadau na watanzania wenzangu jf, ebu tupeane mawazo hizi nyumba nini malengo yake? Kama lengo ni kuwasaidia wananchi wapate makazi kwa nini bei iwe hiyo? Au wamekosea tarakimu? Kwa nini wasijenge nyumba simple na rahisi? na kwanini tangazo linasema hata ambao sio wakazi wa tanzania? Karibu wawekezaji...



SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

KUKARIBISHWA MAOMBI YA KUNUNUA NYUMBA 30 ZILIZOKO MJINI ARUSHA
Shirika la Nyumba la Taifa linawakaribisha watanzania wakazi na wasio wakazi kuleta maombi ya kununua nyumba
zake zilizojengwa mjini Arusha. Nyumba hizo ambazo zinaitwa “Meru Residential Apartments” zinatarajiwa
kukamilika ndani ya miezi mitatu (siku 90) kuanzia tarehe 1 Oktoba,2011.

MRADI WENYEWE:

Meru Residential Apartments zimejengwa kwenye mandhari murua inayokupatia maisha bora katika jamii yenye
usalama. Zimepewa jina hilo kama ishara ya kuuenzi Mlima wa Meru ambao ni mlima wenye Volcano hai nchini
Tanzania wenye urefu wa mita 4,566 (futi 14,980), ukiwa ni mlima wa kumi kwa urefu barani Afrika.

MAHALI ZILIPO:

Meru Residential Apartments ziko mjini Arusha kwenye eneo la katikati kabisa, kwenye mtaa wa Wachaga, Kiwanja
Na. 565/I. Eneo hilo liko umbali usiozidi kilomita mbili toka ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Arusha (AICC), nyumba hizo zimepakana na hospitali ya Selian na Chuo cha Ufundi, na kwa upande
wa mashariki inakupatia muonekano mzuri wa Mlima Meru.

MAELEZO YA NYUMBA HIZO.

Idadi ya Nyumba 30
Ukubwa eneo la nyumba 169.45
Idadi ya Majengo 2
Idadi ya ghorofa kwa kila jingo Ghorofa nne
Idadi ya vyumba kwa kila nyumba 3 (kimoja kinajitegemea)
Sifa nyingine za nyumba hizo Sebule kubwa, chumba cha kulia, jiko,stoo,bafu na
choo [ Nyumba zinauzwa bila samani (furniture)]
Kila nyumba ina maegesho maalum ya gari, pamoja
na tanki la maji la lita 1000.

BEI ZA NYUMBA HIZO:

Bei ya chini kabisa ya kila nyumba ni shilingi za Kitanzania 175,314,366.48 bila kujumlisha kodi ya ongezeko la
thamani. Mwombaji atakayetoa bei ya juu zaidi na kutimiza masharti yote yaliyoelezwa hapo chini ana nafasi kubwa
zaidi ya kuuziwa.

TARATIBU ZA KUOMBA:

Waombaji wanatakiwa kuzingatia utaratibu ufuatao:
1. Wanaopenda kununua nyumba wachukue fomu za maombi kutoka Makao Makuu ya Shirika, kwenye ofisi
za Shirika zilizopo Arusha, au kwenye ofisi yoyote iliyo karibu nao. Fomu zinapatikana pia kwenye tovuti wa
Shirika (Welcome to NHC: "Your Partner in Real Estate Development and Management").
2. Fomu za kuomba kununua zijazwe na kuwekwa saini na kurejeshwa kwenye ofisi za Shirika pamoja na
barua ya kuonyesha kiasi ambacho mwombaji yuko tayari kulipa. Shirika litahitaji pia ushahidi wa malipo ya
shilingi 10,000/=(Malipo yasiyorejeshwa) kama ada ya maombi na malipo ya asilimia kumi (10%) ya awali
zilizolipwa kupitia benki kulingana na thamani ya nyumba uliyochagua.
3. Waombaji wote waliofanikiwa wataandikiwa barua kujulishwa hivyo. Watapewa siku 90 toka tarehe ya barua
hiyo kukamilisha malipo ya asilimia tisini (90%) iliyosalia kulipia nyumba husika. Utaratibu wa kulipa
unaweza kuthibitishwa kwa kulipa pesa kwenye akaunti ya mradi au kuonyesha hati ya mkopo toka benki.
4. Kama uthibitisho wa malipo hautawasilishwandani ya siku 90, mnunuzi atanyang’anywa na nyumba hiyo
kuuziwa mtu mwingine toka kwenye orodha ya waombaji. Mnunuzi aliyeshindwa kulipa hiyo asilimia tisini
(90%) ataruhusiwa kutumia asilimia kumi (10%) ya awali kulipia nyumba kwenye mradi mwingine. Aweza
pia kurejeshewa fedha zake kwa kukatwa asilimia mbili (2%) ya kiasi hicho.
5. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni Jumatano tarehe 4 November, 2011 saa 4:00 asubuhi.
6. Maombi yapelekwe ndani ya bahasha yenye rangi ya hudhurungi/kahawia iliyoandikwa juu;”Maombi ya
Kununua Nyumba za Meru-Arusha”.
7. Maombi yote yapelekwe kwa: Meneja wa Mkoa, Shirika la Nyumba la Taifa, S. L. P 883, ARUSHA


Tafakari...
 
Vp mlizania milioni tano nini!!achn kulalamika bana ndo hali halisi wafanyeje!!
 
Hiyo Pesa nanunua nyumba cash tena hapa Texas ambayo ina vyumba vinne, kwenye community nzuri, barabara ya lami, swimming pool kwenye community, na American standard lkama AC n.k. Tanzania mnaibiwa sana wa hawa jamaa!!
 
Vp mlizania milioni tano nini!!achn kulalamika bana ndo hali halisi wafanyeje!!

Nini malengo yao kujenga hizo nyumba? kama ni kusaidia wananchi ambao hawana makazi wamefeli na kama ni biashara basi watapata ial 175ml? na hapo ni bila VAT
 
Hiyo Pesa nanunua nyumba cash tena hapa Texas ambayo ina vyumba vinne, kwenye community nzuri, barabara ya lami, swimming pool kwenye community, na American standard lkama AC n.k. Tanzania mnaibiwa sana wa hawa jamaa!!

Na ninachoshangaa ni kuwa serikali ilijotoa ktk biashara zote lakin hii ni kama biashara kwa wananchi, kweli wajinga ndo waliwao
 
Hiyo Pesa nanunua nyumba cash tena hapa Texas ambayo ina vyumba vinne, kwenye community nzuri, barabara ya lami, swimming pool kwenye community, na American standard lkama AC n.k. Tanzania mnaibiwa sana wa hawa jamaa!!

Kamundu,

Asante sana mie nimeuliza bei ya appartments milioni 175 wasiofahamu bei za nyumba duniani wamekurupuka tu kuwa hiyo bei halali.

Tukiigawanya Milioni 175 kwa $97,222 au sawa na £60, 344. Hiyo bei unanunua nyumba nzuri tu Marekani au Uingereza ambapo bei za nyumba ni ghali sana. Unanunua bungalow Spain, cyprus, Italy la kuishi wewe na mkeo mkiangalia madhari ya bahari. Kweli watanzania tunaibiana jamani duh!!!
 
Vp mlizania milioni tano nini!!achn kulalamika bana ndo hali halisi wafanyeje!!

Hali halisi kivipi: milioni 175 unafikili ni mchezo kwa vyumba vitatu!!!, pesa zilizotumika kujengea ni makato ya wafanyazi ambao hawatozi riba wakati wa kuzirudisha kwanini sasa ziwe expensive kiasi hivyo.
 
Back
Top Bottom