Maoni yangu juu ya 'Nani aruhusu mikutano, mihadhara na maandamano ya kisiasa au maandamano yoyote'

katalina

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
262
55
Jana katika kipima joto cha ITV, yalitolewa mapendekezo au maoni kutoka kwa wanajopo wa kipindi hicho kwamba kutokana na usumbufu wa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano, yawe ya kisiasa au ya namna yoyote pamoja na mahakama kuruhusu, walipendekeza taarifa ya masaa 48 ambayo ilikuwa inatolewa kwa Polisi sasa itolewe kwa msajili wa vyama vya siasa na msajili atoe go ahead.

MAONI YANGU:
Bado naona urasimu waweza kuwa palepale hata kama msajili akifanya kazi hiyo, mimi napendekeza kazi hii ibaki kazi ya mahakama kama ilivyo sasa na kusiwe na kutoa taarifa Polisi na kama Polisi wana sababu yoyote ya kuzuia shughuli hiyo waende mahakamani.

Wewe una maoni gani?
 
tukitaka mabadiliko na demokrasia yakweli yatupasa tutumie vyema nafasi hii ya uundwaji wa katiba mpya...lazima tupunguze madaraka ya rais lasivyo tutaendelea kulalamika kwani hata huyo msajili wa vyama vya siasa ni mteule wa rais lazima alinde maslahi ya ccm na serikali yake hawezi kutenda haki kwa vyama vya upinzani....!
 
Jana katika kipima joto cha ITV, yalitolewa mapendekezo au maoni kutoka kwa wanajopo wa kipindi hicho kwamba kutokana na usumbufu wa kuruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara au maandamano, yawe ya kisiasa au ya namna yoyote pamoja na mahakama kuruhusu, walipendekeza taarifa ya masaa 48 ambayo ilikuwa inatolewa kwa Polisi sasa itolewe kwa msajili wa vyama vya siasa na msajili atoe go ahead.

MAONI YANGU:
Bado naona urasimu waweza kuwa palepale hata kama msajili akifanya kazi hiyo, mimi napendekeza kazi hii ibaki kazi ya mahakama kama ilivyo sasa na kusiwe na kutoa taarifa Polisi na kama Polisi wana sababu yoyote ya kuzuia shughuli hiyo waende mahakamani.

Wewe una maoni gani?

Soma katiba kwanza ndipo ujue kazi za mahakama ni zipi, kazi za mahakama si kutoa vibali vya maandamano, nenda kajipange upya na mada yako kwa kusoma katiba kwanza
 
Polisi lazima wapewe taarifa ili waweke ulinzi tu! Tatizo si sheria hata hizi zilizopo,tatizo la msingi ni kushindwa kutenganisha Dola na siasa za chama cha mapinduzi.Labda ningeshauri katiba mpya itoe adhabu kali sana ikibainika mwanasiasa anatumia dola kwa maslahi yake au chama fulani.
 
Sidhani kama polisi wanatoa vibali. Nijuavyo hawa wanatakiwa wapewe taarifa kwa ajili us ulinzi tu. Kuzuia mikutano ya kisiasa ni kinyume na katiba. Wanafikiri hii ni chama majina. Au wanafanya maksudi kwa kudhani utaratibu haujulikani
 
Hivi huwa wezi/majambazi au vita wanatoaga ripoti wapi vile?

Mimi nasema, kusiwepo na suala la kutoa taarifa ya saa 48 popote, ili hiyo intelijensia yao uchwara irekebishwe. Hiyo itaweka sense akilini mwao ili waone umuhimu wa kuwa na serious training na serious intelligence unit kulinda mali na usalama wa raia maana muda huu wamekalia majungu na uonevu tu.

Ndio mchango wangu huo
 
Soma katiba kwanza ndipo ujue kazi za mahakama ni zipi, kazi za mahakama si kutoa vibali vya maandamano, nenda kajipange upya na mada yako kwa kusoma katiba kwanza

Wewe unataka kuharibu mada kwa malengo yako binafsi,mleta uzi ameuliza wewe una maoni gani juu ya jambo hilo,ndio maana kuna kubadilisha katiba,kwa maoni ya mleta uzi ni kwamba inaweza kutamkwa kwenye katiba kwamba hiyo ni moja ya kazi yake,samahani kwa hayo niliyosema
 
Back
Top Bottom