Maoni ya Wadau Kuhusu Katiba Mpya Kutoka Dodoma - Live Star TV

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Naona Star TV wanarusha Live matangazo ya maoni ya Katiba Mpya kwa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kutoka Dodoma.

Wameanzia Mazungumzo Studio

Jihabarishe.
----------------
Update:
Wamechakachua sio live tena wataonyesha recorded later.
 
Wametangaza wakazi wote wa dom kujitokeza kutoa maoni yao lkn kinacho endelea ni kwamba watu wamezuiwa kuingi..watu wapo toka saa 2.,ss tunashindwa kuelewa mbona kama kuna usiri ktlk suala hili kwanini kila mtu asipewe nafasi kutoa maoni yake..!?
 
Ukusanyaji wa maoni utakuwepo pale Karimjee wkwa watu wa DSM kutoa maoni yao...........na baraza la vyombo vya habari limeaandaa semina ya mambo haya ya katiba kwa waandishi wa habari kongamano hilo linafanyka kule bagamoyo.....profesa shivji atakuwepo
 
Kutoka kongamano la bagamoyo shivji anasema wanakutana na waandishi wa habari ili kuwaelezea historia, umuhimu wa katiba........leo watakuwa wanachamua ule mswaada wenyewe
 
shivji anasema wanataka wananchi waelewe umuhimu wakishiriki tagu mwanzo hadimwisho wa mchakato.....wanawaelimisha waandishi wa habari ili wao kupitia media zao wasambaze elimu kwa umma
 
Mbona ni maoni ya watangazaji na si maoni ya wananchi? Hawa Star TV ni mamluki
 
star tv tena huyo bwana hapo sijui huwa namuona anaitwa nani mabuga sijui mamluki na alaaniwe kabisa wanakula hela za wafadhili bila kufanya malengo yake, mafisadi
 
Du Star TV wamechemsha, eti kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wao watatuletea matangazo haya baadae na hayatakuwa ya moja kwa moja. Sijui wamechimbwa biti. Boring.
 
Siangalii kabisa.....Tunataka LIVE maoni ya wananchi wa kawaida na si watangazaji au wabunge wenyewe.........
 
Siangalii kabisa.....Tunataka LIVE maoni ya wananchi wa kawaida na si watangazaji au wabunge wenyewe.........

vyombo vya habari taznaia magalasa kweli. Star TV sasa wametoweka rasmi hewani, wanarusha kipindi cha 'msanii wa mduara'

big shame!!!
 
vyombo vya habari taznaia magalasa kweli. Star TV sasa wametoweka rasmi hewani, wanarusha kipindi cha 'msanii wa mduara'

big shame!!!

jamani mbona mnasahau kuwa ni ya aliyekuwa mbunge wa ilemela na waziri wa zamani kwa tiketi ya ccm!? Hao ni walewale tu!! Ndio maana mi nipo naangalia citizen tv, wabunge wa kenya ndani ya the Heague. Ya katiba yetu mi nasubiri referendum nikapige kura ya Huko watakuwa wamepanga waongee Kombani, Wasira, Sofia Simba, Makamba and the like. Kukaa kuwasikiliza ni upuuzi kabisa!
 
waache si tunasubiri referendum NO zitakuwa 70%

kaka nakukumbusha kuwa mtu, taaasisi au kikundi chochote kitachopigia debe / chapuo upigaji kura kitaadhibiwa miaka miwili jela na hakuna faini!!! - ndivyo muswaada unasema
 
Back
Top Bottom