...QUOTE...
[Mheshimiwa Spika,
Kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangazia uhuru kama ambavyo tumeonyesha hapa, huu ni wakati muafaka kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika.
Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano sio tu una Serikali kamili, Bunge kamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya. Katika mazingira kama haya, Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa Muungano unatakiwa kuwa na vitu vyote hivyo pia ili uweze kujadiliana na upande wa kwanza katika hali ya usawa.
Huu ni wakati wa kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika kama ilivyopendekezwa na Tume ya Rais ya Chama Kimoja au Vyama vingi mwaka 1991 na Tume ya Kissanga mwaka 1998, na kama ilivyopendekezwa na Kundi la Wabunge 55 wa Bunge hili tukufu na kuungwa mkono na Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi kabla ya hoja hiyo kutunguliwa na Baba wa Taifa mwaka 1993!] ....QUOTE...
My Take: Hio Quote hapo juu kutoka katika Hotuba ya Lissu, inanifanya nianze ku-connect dots toka kwenye last thread ya member anaeitwa HUTAKI UNAACHA humu jamvini, Kwamba Rais Kikwete alikutana na Mbowe(M/kiti Chadema), Kwamba tume ya Jaji Warioba hatimaye itapendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na itapitishwa hio 2015, Kwamba Rais Shein ataendelea kuongoza SMZ kama Rais hio 2015, Kwamba Lowassa atakuwa Rais wa Muungano hio 2015, Kwamba Dr.Slaa atakuwa Rais wa Serikali ya Tanganyika ambayo haina maamuzi hio 2015.....Just my thought...