MAONI ya Upinzani Bungeni, Ofisi ya Makamu wa Rais; Muungano; A MUST READ

FJM kama kawaida serikali itakuja na majibu mepesi kwenye maswali magumu. Mark my words, wataijibu hii hotuba kirahisi kwamba kama una shida na muungano basi peleka kero zako kwenye tume ya katiba. Wakati tatizo kuu lipo sasa na ambalo inawezekana hata hiyo tume isiweze kulirekebisha.

Wabunge wa Zanzibar wasipotumia fursa hii kufunguka kuhusu matatizo ya muungano, basi wakae kimya milele na wasitusumbue tena na kelele zao za kila siku kuhusu kero za Muungano.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: FJM
Mtego huo subiri tuwasikie...je wanapenda chama au Nchi,wapi MABUMBA????
vox populi,vox dei
 
Mzee wangu alikuwa ni mongoni Mwa wabunge waliokuwa wanaunda kundi la wabunge kutoka bara waliokuwa wanadai Tanganyika yaani kundi la G-55' Balozi Nhigula ambaye aliwahi Kuwa Mbunge wa Kwimba huko Mwanza na pia aliwahi kuwa Naibu Speaker Kabla ya Mzee Msekwa,

hii ilimletea matatizo Makubwa waziri mkuu wa wakati ule mzee Malecela nA Mwalimu Nyerere.

Ni wakati sasa kuondoa utata huu wa muungano kwa dhamira ya dhati na uhalisia wa hali ya nchi, naunga mkono hotuba nA Maoni ya kambi ya upinzani yamejaa facts nA nia njema kwa taifa letu.
Ccm waache mara moja hila za kujifanya watetezi wa muungano mchana wakati behind closed doors nA matendo yao yamekwisha uvunja muungano nA wamevunja katiba ya nchi ambayo wameapa kulinda nA kuitetea.

Wekeni kura ya Maoni tumalize hiki kiini macho
 
JK hakuwa mjinga.. alisema ni bora yeye akose ikulu lakini sio hii kichwa kuingia bungeni.
Bravoo Lissu = Wabunge wote wa magamba + Wake zao + Waume zao + arawaham zao.
 
Hii ni changamoto nyingine kwa Watanzania wote (watanganyika na wazanzibar). Ni safari ndefu ambayo inahitaji busara na umakini wa hali ya juu katika kuamua kwa maslahi ya waliowengi. Hakuna siasa hapa bali ukweli.
 
...QUOTE...
[Mheshimiwa Spika,

Kama ilivyo kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano umejitangazia uhuru kama ambavyo tumeonyesha hapa, huu ni wakati muafaka kuanzishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika.

Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano sio tu una Serikali kamili, Bunge kamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya. Katika mazingira kama haya, Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa Muungano unatakiwa kuwa na vitu vyote hivyo pia ili uweze kujadiliana na upande wa kwanza katika hali ya usawa.

Huu ni wakati wa kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika kama ilivyopendekezwa na Tume ya Rais ya Chama Kimoja au Vyama vingi mwaka 1991 na Tume ya Kissanga mwaka 1998, na kama ilivyopendekezwa na Kundi la Wabunge 55 wa Bunge hili tukufu na kuungwa mkono na Serikali ya Rais Ali Hassan Mwinyi kabla ya hoja hiyo kutunguliwa na Baba wa Taifa mwaka 1993!]
....QUOTE...

My Take: Hio Quote hapo juu kutoka katika Hotuba ya Lissu, inanifanya nianze ku-connect dots toka kwenye last thread ya member anaeitwa HUTAKI UNAACHA humu jamvini, Kwamba Rais Kikwete alikutana na Mbowe(M/kiti Chadema), Kwamba tume ya Jaji Warioba hatimaye itapendekeza kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na itapitishwa hio 2015, Kwamba Rais Shein ataendelea kuongoza SMZ kama Rais hio 2015, Kwamba Lowassa atakuwa Rais wa Muungano hio 2015, Kwamba Dr.Slaa atakuwa Rais wa Serikali ya Tanganyika ambayo haina maamuzi hio 2015.....Just my thought...


 
Tutaichambua hotuba hii.
Maoni mengi yamewakilishwa na kuwakumbusha wanaJF, rejeeni thread mbali mbali ikiwemo ile ya Let ZBAR GO!

Tutaendelea kuichambua.
 
Mambo siayo bwana sasa uamsho shindweni wenyewe ngoma imewekwa hadharani tena peupe maana mkichoma makanisa mwisho mtauwa na polisi wa Magamba maana sisi wenyewe tangu zamani tuanawaonea huruma kutokana na ukoloni huu mlimowekwa na Ccm. Sasa fuatilieni michango ya wabunge wenu atakayeunga mkono muungano kachomeni nyumba yake maana huyo ndo analeta muungano!

Someni vizuri hiyo hotuba ya upinzani acheni jazba tulizeni mawazo na akili ili mukomboe zanzibar kama mnavyotaka maana kuna watu wanawasubiri mkiitoa tu watie maguu wawaletee maendeleo toka uarabuni.Pia sisi huku bara pia hatujazoea kubaguana au kuchomeana makanisa,misikiti au miti ya kuabudia hivyo hata sisi mtakua mmetusaidia maana kwakweli hatuwapendi kiivyo kama mnavyodhani ila kwa hili tutawasaidia mpaka dakika ya mwisho,labda mtuangushe nyinyi menyewe! Ashukuliwe mungu aliyeileta chadema hapa Tanzania ituepusha na Kuchomeana nyumba za ibada na jirani zetu zenji kwa kutudanganya eti sisi ni nchi moja! Yani kweli Mbeya na Kusini Pemba ni Nchi moja?Alaaniwe Magamba kwa utapeli wa akili aliyeuleta kwa kiasi hiki! Best wishes uamsho na waislamu kwa ujumla kazeni misuli jamani mfanikiwe na mungu atawaongoza!Aaaaamina
 
Du! vichwa vimeenda shule hivyo, Mwigulu hatakuwa na jipya kwenye hii hotuba

Kama kawaida yake atatafuta kaneno kamoja kalikokosewa na kuifanya hoja. Mfano; Palipoandikwa Tanzania Zanzibar atadai Tanzania ni moja tu, hivyo wapinzani (CDM) wameonyesha kuigawa nchi katika vipande.
 
Ni speech yenye uchambuzi makini kweli. Watakaochangia hoja hapa ni wabunge wachache maana inahitaji usomi na kujipanga vizuri kutoa hoja za kueleweka. Sidhani kama akina Lusinde watatia mguu hapa. Wapo vichwamaji wengine wa CCM watakaoibuka na maneno ya mipasho kwenye hoja makini kama hii. Akina Mwigulu Nchemba hawakosi.
 
Huu mchango wa CDM umesimama vibaya mno Ngoja tusubiri wakina Mwigulu wakati wa kuchangia tuone Kama wataitupa tena na kusema rubbish

Mkuu huyo atatafuta spelling error tu hana cha kuchangia hapa maana "a spade has been called spade and not otherwise" !
 
''Katika mazingira ambayo upande mmoja wa Muungano sio tu una Serikali kamili, Bunge kamili, Mahakama kamili, wimbo wa taifa, bendera ya taifa, na sasa una nchi kamili yenye mipaka na eneo la bahari linalojulikana, una majeshi yake na Amiri Jeshi Mkuu wake, huu ni muda mzuri kwa Serikali ya Tanganyika kuzaliwa upya. Katika mazingira kama haya, Mheshimiwa Spika, upande wa pili wa Muungano unatakiwa kuwa na vitu vyote hivyo pia ili uweze kujadiliana na upande wa kwanza katika hali ya usawa''
Hapa tu pantosha! Maana ya hii ni kuwa Tanganyika ikirudi kila kitu kitawekwa mezani kama ikibidi. Hapa uwezekano wa serikali 3, mkataba n.k haupo kwa sababu Tanganyika itauliza ZNZ inaweka nini mezani. ( Thread- Duru za siasa, bandiko# 118)
 
Hapa tu pantosha! Maana ya hii ni kuwa Tanganyika ikirudi kila kitu kitawekwa mezani kama ikibidi. Hapa uwezekano wa serikali 3, mkataba n.k haupo kwa sababu Tanganyika itauliza ZNZ inaweka nini mezani. ( Thread- Duru za siasa, bandiko# 118)


Jioni hii tutapata majibu ya hiyo speech, ila nadhani muda umefika sasa tuanze kupeperusha bendera na kuvaa t-shirt. Hakuna cha serikali moja, mbili au hata tatu. Na kama ni mkataba tukutane Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
'Kitu' kiko makini sana hiki. Bila chadema nchi hii itakuwa na 'mbumbumbu' wengi sana!

Hii hotuba nilikuwa naisoma kwa makini sana utafikiri najiandaa na paper ya mwisho kumalizia degree. kitu kimeenda shule na kimepengiliwa kwa makini wanasheria vihiyo kama Ngeleja sijui watachangia nini hapo wakati kila kitu kiko wazi. Na mchumi wetu first class fake Mwigulu Mchemba atachangia nini hapo? maana hakuna bla bla ni shule tupu hapo ndani
 
Msiwe na papara wala msivamie mambongwa , nafikiri sana wakuu wa CDM wananisoma hapa JF na wananifahamu vilivyo ,na sasa wameamka na kuuelezea umma wa WaTanganyika ni wapi WaZanzibari walipofikia.

Mimi msimamo wangu ni kuwepo kwa Tanganyika ,Je CCM wapo tayari ??? Kwani kuwepo au ujio wa Tanganyika ni kifo cha CCM ,kurudi kwa Tanganyika ni kuvunjika serikali iliyopo ya Muungano ,kwa maana hiyo upande wa Tanganyika kutahitajika kuundwa serikali ya mpito na kufanyika kwa uchaguzi ili kumpata Raisi wa Tanganyika.

Sasa mmeona eei ,turufu ya kuidai Tanganyika ,anzeni kupeperusha bendera za Tanganyika kama mnazikumbuka ili kumuunga mkono shujaa huyu. :spy:
 
Dodoma umeme umekatwa tena jioni hii, ili watu tusione michango ya wabunge ktk mjadala wa hotuba ya ofisi ya VPO Muungano na Mazingira
 
Back
Top Bottom