Maoni ya ulimwengu kuhusu katiba mpya

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
318
kuna maneno mengi aliyoyaongea Jenerari; mojawapo ni kuwa wakati wakiwa kwenye peak na Mkapa walibadilisha kipengere cha katiba kuhusu ushindi wa rais uwe hata kwa kura moja tu (simple majority) kwa ajili ya kukwepa wimbi la Mrema.

Japo ulimwengu hakuongelea suala hili kwa undani lakini bila shaka mkono wake ulikuwa mkubwa sana katika kuhakikisha ubadilishaji huo unafanyika japo kama kawaida yake anasema ni Chenge ndo alifanya hivyo.

Kama yeye aliweza kushiriki kufanya ''uhalifu'' huo mkubwa kwa ajili ya mshirika wake, je ni kweli leo anaweza kuwa na nia ya dhati ya kubadili katiba?. Nina wasiwasi na wanaharakati na wasomi wanaomtumia huyu bwana kuamsha mjadala wa katiba mpya hana nia ya kweli' mikono yake bado haijatakasika kwa 'dhulmati'' hiyo aliyoifanyia demokrasia ya TZ

Kauli nyingine aliyonishangaza ni kuwa "Ukuu wa wilaya siku hizi wanapewa wachumba zao" samahani hiii sio nukuu ya moja kwa moja ingawa alimaanisha hivyo).

Sasa huyu bwana amekuwa serikalini muda mrefu sana na mbaya zaidi amewahi kuwa mkuu wa wilaya, na mfumo unaotumika leo kuteua wakuu wa wilaya ndio ule ule uliotumika hata wakati yeye anateuliwa ukuu wa wilaya, na kwa kuwa hajawahi kuulalamikia mfumo huo, je ina maana hata yeye aliteuliwa kimtindo huo? Je tuangalie makabrasha kujua nani alipendekeza jina lake............je hakuwa ndugu yake, kabila lake, dini yake, mshkaji?

Kama mwandishi msomi, mzoeefu na mzeefu anajua msemo ule unaosema usisiseme kama huna uthibitisho, je yupo tayari kututajia majina ya hao ''wachumba''. Wasomi lazima wawe tofauti na watu wa kawaida huwezi kusema jambo hewani tu halafu tukakuacha tu bila kutaka ushahidi.

Pia kwa kuwa Ben Mkapa alikuwa mtu wako wa karibu kiasi hicho kisha mkagombana na umemuandika saaaaaaaaaaaaana kumponda, ingekuwa vyema kama ungetueleza chanzo cha ugomvi wenu. Maana kama jana mtu unamuandika au kumsema vizuri ghafla kesho unaanza kumponda ni vizuru sisi hadhira ukatufahamisha kwanini umebadili kibwagizo. Nini chanzo cha ugomvi wenu na Mkapa maana tumechoka kila siku kumponda tuuuuu wakati alikuwa rafiki yako.

Nashauri hizo tofauti zetu mmbaki nazo wenyewe sirini sio kurushiana madongo maana mwingine amefungwa mikono hawezi kujitetea na madongo yako
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom