Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Zitto katoa hoja yake na kaijenga; jukumu la wengine wasiokubaliana naye ni kuonesha mapungufu ya hoja hiyo pasipo ulazima wa kumuita majina mbalimbali kwani kwa kuitana majina hakuthibishi nguvu ya hoja bali udhaifu wake. Je, hoja ya Zitto ina nguvu kiasi gani au ina upungufu kiasi gani? Kusema "Zitto hana credibility" haisemi lolote juu ya uzito wa hoja yake. Hoja hujibiwa kwa hoja.