Maoni ya katiba- wahafidhina wanavyoteseka zanzibar

jamesbond007

Member
Jun 27, 2012
36
8
WANAOGOPA KUDHURIWA NA VIAPO VYAO
TUWAOMBEE DUA KWANZA
WASIPOBADILIKA TUWAZOMEE KWA ZAMU.
By Zdaima.

Mwenyezimungu wafunguwe waja wako hawa waweze kutambua wema na ubaya Amiin. Ndivyo ninavyoweza kuanza maelezo yangu haya.
Naaam wazalendo. Kwa kweli hali ya ndugu zetu hawa wahafidhina inasikitisha sana na jinsi wanavyohaha inafika wakati wanatia huruma sana. Katika suala hilila maoni ya katiba na Muungano wa Tanganyika na zanzibar hawa jamaa utadhani ni kesho tu watakosa uluwa wao kwa jinsi walivyo .Baada ya Kuona dalili za kufifia ile agenda yao ya kibaguzi katika kufikia malengo yao binafsi na kimaslahi wameendeleza njia ile ile katika kutaka kujinusuru. Wanadhani bado tuko kule kule tulikotoka .fitina zao zinaendelea lakini inaonekana zimegonga mwamba hadi sasa.Hebu angalia hapa.

Baada ya Wazanzibari waliowengi kuonesha nia ya kutaka mabadiliko katika mfumo wa muungano ili uwe wa mkataba kwa maslahi ya nchi zetu mbili ikiwemo Zanzibar ,wamefanya vitimbi vingi sana kutaka kuzuwiya hilo na kadri siku zikiendelea wanaanza kufedheheka. Wallianza kutumia Polisi wahafidhina kutaka kuzuwiya harakati za uamsho mara kadhaa na wameambulia fedheha kwa uongo wao na kutaka kuwabambikizia kesi zisizo na miguu wala kichwa wale wanaowaona ni maadui zao.Mahafidhina hawa wa kipolisi walitaka kutumia vyeo vyao ama kwa kulazimishwa kujitutumua au kwa utashi wao wakidhani wangefanikiwa hatima yake hawakupata kitu zaidi ya kupoteza muda mahakamani kwa zile kesi uzushi . baada ya kufeli hili wakataka kutumia mwevuli wa Chama wa kihafidhina kupambana na UAMSHO bila yamafanikio baada ya kukemewa na SERIKALI katika kikao cha wanasiasa, masheikh na serikali kilichofanyika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilshi walikwama.
baada ya kuzidi vugu vugu la mijadala ya wazi na katika Baraza la wawakilishi kwa wajumbe kutoa maoni yanayotaka zanzoibar kuwa na mamlaka yake ya kimaamuzi na kiuchumi katika muungano safari hii wakaja na gia nyengine ya kichama kwa wtu wa kada za chama kuwashtumu baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM kuwatuhumu hadharani na hata wengine kulaaniwa cha kushangaza walitumia mwavuli wa ngazi ya wilaya kutaka kuwangoa vogogo jee ngazi husika hawakuzijuwa ? walikuwa wanaendelea kutapatapa tu wakidhani ule utamaduni wa zamani ungefaa.vile vile walitumia UVCCM baadhi ya viongozi wao ambao wamegawanyika kutaka kufanikisha agenda zao bado wanatapatapa. Ni hivi majunzi tu wabunde wa CCM wahafidhina kutoka zanzibar walitoa madai yale yale ya ngazi ya wilaya ya mjini ya kutaka wanachama wenzao wafukuzwe.

Hapa kuna masuali mengi hivi kelele zote hizo zina maana gani kuna tafsiri kuu mbili hapa. ya kwanza wameanza kugwaya hawa wanaona mbona chama ngazi ya Taifa bado wako kimya. kwani haaifahamu hilo. si ni chama hiki taifa kilikubali agenda ya katiba mpya na suala la muungano likakubaluwa uhafidhina wao umewafunika maccho hata hili hawalikumbuki. sasa kelele zote hizo zinaashiria wanapigia kelele maslahi yao ambapo kwao wao zanzibar kuwa huru katika kuamua na kuwa na mamlaka yake watakosa maslahi na wataapizwa na viapo vyao walivyokula vya kuhakikisha zanzibar inadidimia ili kulinda maslahi yao binafsi.
Baada ya hatua zao hizo kuonekana kugwaya mpaka sasa ( sijuwi labda chama chao kitawawajibisha wanachama wao) wameigeukia SUK na viongozi wa kitaifa kwa kuwakashifu sana na kupandikiza migogoro isiyokuwepo wakidhani watafanikiwa. jitihada zao zote hizo inaonekana bado.Wanatumia vyombo vya habari vya kihafidshina na vile vya tanganyika visivyo na maslahi na zanzibay kupotosha ukweli. mkakati wa vyombo vya habari unaendelea lakini bado hawajafanikiwa.na kwa sasa wameamua hata kutaka kuwafitinisha viongozin wa vyama vyengine (CUF)baada ya kuona wale wa chama chao hawajawajibishwa kama walivyotarajia.kwa nini njama zote hizo zinakuja kuna walakinikatika mipango yao wanaelekea kufel,. bado tunakumbuka enzi zile
mwavuli wa chama ukitoa shutuma tu serikali inatii na kuchukua hatua hgata kama haina ukweli hili ndani ya suk halina nafasi licha ya kuwatumia wahafidhina wachache ndani ya suk. Jamaa wanataabika kwa kupiga makelele yasiyosikilizwa na mtu ndani ya chama chao na hata katika serikali ambapo hapo awali walitiiwa. hapa kunani? na kwa nini sasa waamuwe kuwashambulia viongozi waSUK na kutaka kuwafitinisha ( CUF ) eti sera ya chama hicho ni serlkali 3 na wanachama wake wanatoa maoni yanayokinzana na sera za chama Mhhh leo hii wahafidhina na vyombo vyao vya habari wamekuwa CUF? au ndio wanahuruma sana na hiki chama huko ndiko kugwaya na kutaabika.

Nini kifanyike ili tuwasaidie ? mimi naona kwanza tuwaombee dua maana wanaonekana wanasumbuka pengine hivyo viapo vyao na ahadi walizokula za kuwa madalali na wapiga debe wa kuipoteza Zanzibar vinaelekea kuanza kuwageuka na wanahofu ya kuja kuadhirika. – tuwaombee dua hii kwa ha tua ya kwanza.MUNGU WAFUNGUWE WAJA WAKO HAWA ILI WAITAMBUWE HAKI AMIIN.
Hatuwa ya pili wasipojirudi basi tupange siku ya kuja kuwazomea huko siku za mbele napendekeza tuwazomee kama hivi
NYI,NYI,NYI. WA,WA,WA. TU,TU,TU. MWA, MWA,MWA
WA,WA,WA. MA,Ma,Ma. SI,SI,SI. LA,LA,LA. HI,Hi,Hi PWAAAAAAA.
Napendekeza vizomeo hivi vipigwe mara 3 na tuongozwe na (Mfarosty ufundi, Asheikh na Bosco akitaka) mimi na Mkarafuu tutakuwa na jukumu la kuwasubukuwa vichwa wakati wa kuwazomea. tetetehhhhhh.(masihara kidogo).

MWISHO.
Jamani huu si muda wa kuendekeza sera ambazo hazina maslahi na nchi iwe kwa chama chochote kile. Tusiwe watumwa wa kutawaliwa na sera za vyama na tuipe nafasi sera ya nchi itawale- hili la katiba mpya na muungano wa mkataba linajadilika na linawezekana. ZANZIBAR DAIMA.
 
Mbona hueleweki? Muungano wa mkataba wa nini? Hatuwataki wazanzibar,ondokeni mtuachie Tanganyika yetu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom