Maoni wakuuu

bigjeff

Senior Member
Oct 25, 2009
111
22
Ebwanaa habari wakuu nilikuwa kimya kidogo miangaiko ya hapa na pale sasa mi naomba mawazo na pia mtu mwenye interest yoyote ya kitu chochote kutoka UK,najipanga nije nyumbani baada ya muda kidogo kutokuwepo nyumbani kama miaka mitano sasa ninakikontena changu nataka nikijaze kidogo bidhaa ambazo naweza kuleta hapo nyumbani nikapata hela ya mafuta maana nasikia mafuta hayagusiki sasa kama naweza nikapata mawazo ya bidhaa zenye soko kutoka huku UK ningeshukuru au mwenye kutaka kitu kutoka huku UK humu jamvini angenipa order e-mail yangu ni ( jeff15tz@yahoo.com).AKHASANTENI.
 
Mkuu.Nakushauri ulete vitu vilivyokwisha tumika Yaani Used, km vile TV,RADIO,FIRIJI,MAJAGI YA UMEME,PASI,NK.make wabongo wengi sana wanapenda vitu km hivyo, Hapo hautalala njaa Mkuu.Pia vipuri vya magari ni deal tu,.e-mail mackman242001@yahoo.com
 
Kama unaweza leta consumables za magari saloon, 4WD, ambazo ni genuine. Ni deal kama price iko right. Anything that get replaced in a car on a regular basis like filters, brake pads, shock absorbers, etc.
 
Usisahau hata tu-laptop tulitotumika kidogo, ni deal sana kwa madenti wa vyuo.
karibu sana nyumbani, ila mafuta ndiyo hivyo siku hizi TZ tumeendelea tunayachanganya na maji na gari zinatembea.
 
1.kama mara ya pili hii unaandika hivi je ni wewe au nachanganya?
2.usisahau kuna import duty,we leta mali zako halafu ukifika pale custom utashaa.
3.watafute dealers wa vifaa vya kilimo wakupe oda,uje navyo,kodi kidogo faida kubwa
 
ndio mimi mkuu Tall kipindi kile nilipata order nikafanya najamaa fulani biashara kidogo ndio kuangaika, kupata kujua kina endelea nini hapo nyumbani nashukuru kwa maoni yako unaweza ukanipa details za madealers plz wa kilimo
 
hilo contena unaloletea mzigo ni futi ngapi? limeshapata mtu, kama halijapata mtu utaniuzia shilingi ngapi?
 
TALL ......Nakitu kingine vipi biashara za hardware nikimaanisha vitu vya kufanyia wiring nyumba kama sockets,earth wire, kuna auctions nyingi uku vitu hivyo vinapatikana kwa wingi
 
laptop zinalipa kimtindo. tahadhari; check na watu wanaojua mambo ya ushuru bandarini
 
Laptop zitakulipa - kama utapata HP itakuwa nzuri zaidi or Jitahidi kupata Compaq, Dell, IBM - Duo Core 2.0Ghz, atleast 2GB memory na 160HDD. hapa unaweza uza kwa dola 450 hadi 500. hakuna ushuru kwa hiyo we angalia bei ya huko.

Usinunue desktop - hazina soko, unless kama unataka kufungua internet cafee ingawa si biashara nzuri bongo. karibu home, umejenga? kama hujajenga kupanga nyumba 3 bedroom fanced, middle class ni laki 4 mpaka 5 kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom